spika wa bunge mh. samuel sitta akimwapisha mh. magreth sitta bunge la serikali ya awamu ya nne lilipoanza kazi rasmi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 31, 2006

    Huyu mzee wakati anachaguliwa alikuja na bwebwe kuwa ni mtu wa standard kumbe hakuna kitu. Halafu nilishangaa watz walikuwa wanasema Msekwa ni mzee sana, kumbe huyu nae ni mzee kinoma. Uwezo wa kuwa na mawazo endelevu ulishaisha siku nyingi. Hivi sijui kwa nini watz huwaga hawapendi kustaafu na kujipumzisha UBINAFSI tu. mtu anataka mpaka afie kazini tutafika kweli.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 31, 2006

    naomba watu wanaochangia hoja za umri waseme umri wao kuliko kuchangia maana ............yawezekana.....!!!!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 31, 2006

    Typically Tanzania, yaani mambo yote kwa Sitta, Sitta tu. Mambo ya kuchomekana kuchomekana tu!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 31, 2006

    Nawaunga mkono Trio Kaka na Grill katika kumshangaa huyu anayetaka umri katika kutoa maoni haya. Nashangaa kuwa hawa akina Sitta, Kingunge na Mzee Malecela bado wanajifanya waanatoa mchango katika taifa hili, kwa umri wao ingefaa waachie vijana ili watoe mawazo mapya, sasa utashangaa sheria ya umri wa kustaafu ipo lakini utaona watu bado wanataka nafasi katika utumishi wa umma hata kama wamefikisha umri huo, kwanini wasiwaige akina Kawawa, Msuya na wengine wenye hekima kama hao. Kung'ang'ani kubaki katika nafasi hizo ni kielelezo cha kufanya vibaya wakati wakiwa vijana sasa wanataka kukamua ili wafidie waliyoharibu, sawa katika HRM kuna sera ya kuretain wafanyakazi lakini je kwa hawa kunasababu yoyote ya kuwaretain? Hapa ndipo tunapoona kuwa watu wanapeana vyeo ili kuripa fadhila,kwa mtu aliye serious hata aakipewa cheo akiona umri umemwacha huwa anakuwa mkweli kukataa, lakini hawa thubutu! basi wangeachwa wakuu wa mikoa na wilaya waliofikia umri wa kustaafu si wapo waliochini ya umri wa Sitta na mama Sitta? N a wewe uliyetaka umri mimi niko kati ya 20-25.SAWA MHESHIMIWA MTETEZI WA WAZEE!

    ReplyDelete
  5. Huyo Sitta inavyoonekana hataki kuachia ngazi mpaka aone kuna Sitta kama mia Sitta hivi bungeni ndio ataondoka. Ndio u "Mobutu" wa chini chini huo. Lakini uzembe wa nani anayewachia hayo yote? Sababu hayo waliyosema awali Trio kaka na Grill ni white tupu!
    We Michuzi vitu kama hivyo nitavifikisha vipi bungeni? Ni nani anayehusika na kesi za malalamikaji kama haya? Wewe kama mbuge mtarajia, mimi binafsi ninataka kucomplain hii case kwa vyombo vinavyohusika, naomba tu uniambie ni wapi.
    Asante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...