NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII KUTOA PONGEZI KWA WANA WA DARAJANI KWA USHINDI MWEMBAMBA WA LEO.


INGAWA MMETUFUNGA, NASI CHENGA TUMEWALA, LAKINI KWA UJUMLA MCHEZO ULIKUWA MURUA DAKIKA 120 ZOTE, HASA ALIPOINGIA ANELKA WENU NASI BABEL WETU.


ROHO INGENIUMA SANA KAMA NINGETOLEWA NA MASHETANI AMA WABEBA BUNDUKI. LAKINI NYIE HAIUMI SANA.


TENA PAMOJA NA REFA KUWABEBA KWA KUTUNYIMA HENDBOO MBILI (ZA TERRY, LAIVU!) HAINA NOMA. TUNAJIPANGA UPYA NA INSHAALAH TUTAONANA MWAKANI. NA HUKO MOSKO MKISHINDWA KUMPUNGA SHETANI MTATUUDHI MAANA TUTAKUWA TUNAWASHANGILIA NYIE...


NA WEWE ABDALLAH EZZA NA MWENZIO MTI MKUBWA HUKO MLIKO NENDENI MKALALE SASA. KESHO MAANDAMANO MEI MOSI, EBO! KUSHANGILIA GANI HUKO? MNAKUWA KAMA HAMJAWAHI KUSHINDA BWANA! YAANI MNAKUWA KAMA YANGA...! DAH!


YAANI MPAKA SIMU NIMEZIMA KWA USUMBUFU WENU MTIMKUBWA NA EZZA....
YAANI ANGALAU CHIBIRITI KAKUMBUKA KUNIPA SALAMU ZA POLE. ASANTE MDAU WA CESENA, N'SHAPOA KAKA....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2008

    Well Said Michu....I hope jamaa hawatatupotezea heshima Moscow

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2008

    brother acha unoko,wanaume walishinda jana,sio waliobebwa na refa kuwanyima penalti mbili za wazi,
    chelsea kashazoea kubebwa ndo maana hata muyahudi kapiga magoti anasali uatafikili kachukua kombe lenyewe.
    sasa huyu watamuita special two?maana morinyo walimuita special one.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2008

    MICHUZI BORA UNGEENDA WEWE LEO KUJIDONDOSHA MPATE PENATI.HA HA HA POLE SANA.
    MIMI NINA SWALI MOJA WADAU,KWANINI WASHABIKI WA ARSENAL,LIVERPOOL, NA MAN UNITED KAMA HAWAJAFANIKIWA KUFIKA MBALI WANAONA BORA CHELSEA WACHUKUE?
    Mdau wa imarati hapa yaani hilo swali mpaka mimi nawajibika sema sijui kwanini.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2008

    Shukran Michuzi kwa pongezi zako, kweli asiekubali kushindwa sio mshindani, wewe nimekukubali kama mwanamichezo na nakupa pole kwa fimbo za leo. Hawa mashetani wekundu dawa yao ni ile ile ya jumapili iliyopita, hawajamaliza dozi bado.
    Shukurani kwa wadau wote wa Arsenal kwa pongezi zao.


    Ezza.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2008

    Bwana michuzi poleni sana ila metupa kiburudisho maana mnapigwa risasi hamfi mnaenda tu goli zuri sana la BABEL ILA NDIO HIVYO. Mnakumbuka nimewaambia sitaki kukutana na Chelesea Final nilikuwa na maana yangu mnaona walichowafanya hawa vijana ,na furaha kwajili media imemkandia sana Avram Grant safi sana.upande mwingine nashukuru three weeks from now wachezaj iwote watakuwa wamepimzika kwahiyo mechi inakuwa bomba sana lakini mesikia bei za gharam ya moscow kwa ujumla pamoja na visa,ticket,malazi ni kama £2500
    mh si mchezo. haya kaka poleni mwakani muongeze torres wawili


    William uk (united for life)

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2008

    Oyaa michuzi kama na kuona goli la drogba umetoa mimacho kama fundi saa mara babelkapiga bao imani inarudi mara umeisha! pole ndio foot chelsea ni different class lakini unmejitahidi sana hasa kupata goli mbili pale ambako hata man u kachemsha ni poa. Ila kaka Chelsea wanachukua kombe kataa kubali. Come on Chelsea!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 01, 2008

    Kusema kweli hakuna timu nayo iogopa kama bwawa la maini japo najiamini mtoto wa darajani ngoma huwa nzito napo kutana na bwawa anyway pole sana michu ngoja tukawape dozi No mbili mashetani by Edo.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 01, 2008

    aisee mwenye kuweza kulipua bomu siku ya fainal pale moscow wakati hizi team zinagombania kuchukua kikombe cha ubingwa wa ulaya au kama vipi anayejua ndege watazokodisha kuendea moscow aseme mapeme tuanze kutafakari jinsi ya kuzihack...itakua safi sana wakalipuliwa yaani imagine ronaldo na drogba kufa siku hio hio moja si itakua furaha sana kwa mashabiki wa liverpool? tutakua hatuna mpinzani tena duniani

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2008

    Angalau mmevunja mwiko mana tangu aliyekua winger wenu Bruno alipofunga mwaka 2004 hamjatikisa nyavu tena pale darajani hadi leo,Ila mshika kibendela alikua na ajenda ya siri kutoka Italy,maana Drogba hakua mbele ya Reina ye akamnyima Essieni bao lake murua!.Sasa tunakwenda Moscow nyumbani kwetu.Usiwe na shaka shetani atapungika tu kwani msimu ndio kwaanza umeanza! Tuombe mshahara upande leo....hahahaaa,au PAYE ipungue!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2008

    Hivi miaka yote hamjui "Babu" aka Alex ni nani? Hata siku moja hawezi kufungwa mechi kama hii.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 01, 2008

    LIVERPOLL UWEZO WAO KISOKA NI MDOGO KULINGANISHA NA CHELSEA

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2008

    leo umefungwa si visababu mbona ulipotufunga immarat hatukusema mpira ndo ulivyo usijali sana -mdau

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2008

    BRO MICHUZI HAMNA NOMA WALA NINI KWASISI BWAWAZ KUFUNGWA JANA..ILA KITU KIMOJA TUMEUDHIHIRISHIA ULIMWENGU KUWA SISI NI WANAUME TMK..SHENZ TAIP SIO KAMA WACHOVU MAN NA ARSENAL HUO WANAFUNGWA NA CHELSEA KAMA WAMESIMAMA!!

    KUMBUKENI TOKA THE REAL SPECIAL ONE JM AICHUKUE CHELSEA 2004 ARSENAL NA MAN U HUWA NI KICHAPO TU HASA MAN U YAANI WANAKUA UBWETE TU. MAN WAMEIFUNGA CHELSEA MARA MOJA TU NAYO ILIKUA NI KWENYE LIGI YA MWAKA HUU MECHI YA KWANZA PALE OT TENA WKT HUO NDO JM ALIKUA ANAONDOKA NA A. GRANT NDO ANAINGIA NA WACHEZAJI WA CHELSEA WALIKUA NA KAMGOMO KWANI WALIKUA WANAMTAKA JMWAKATI LIVA NDO TIMU PEKEE AMBAYO CHELSEA WANAIOGOPA NDO MAANA JANA WACHEZAJI WOOTE WA CHELSEA WAMEFURAHI UTADHANI WANAENDA MBINGUNI NA YULE MYAUDI WAO GRANT MPAKA KASALI KIYAHUDI MAANA ALIJUA ANAKUTANA NA WANAUME SHENZ TAIP..!!

    its me SMALL BENITEZ

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2008

    SABABU 10 ZA CHELSEA KUIFUNGA MAN U MOSCOW 21 MAY 2008

    1. MAN DAIMA NI VIBONDE WA CHELSEA
    2. CHELSEA WANACHEZA MPIRA MZURI KULIKO MAN
    3. ABROMANVIC ATATUMIA UWEZO WAKE WOTE WA PESA KUHAKIKISHA USHIND
    4. KWA KUCHEZEA MOSCO NYUMBANI KWA ABROMAVIC CHELSEA WATAKUA NYUMBANI
    5.CHELSEA WAMEFUNGA GOLI KILA UWANJA SIO KAMA WACHOVU MAN

    SABABU ZINGINE BAADAE..TEH TEH

    its me SMALL BENITEZ

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2008

    sawa wazee wa Bwawa la maini kwa kutukandamiza,mnaonyesha ni jinsi gani hamtupendi kwa maendeleo yetu ya maushindi but mkae mkijua huko moscow tunarudi na ubigwa,tulikuwa tunawataka sana hawa jamaa tukutane final...tontonny

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 01, 2008

    Kaka Issa wewe kama hujaumia kufungwa na chelsea ni wewe mkuu, mimi na wadau wengine wanaoisupport liverpool tumeumia sana tena sana, kufungwa ni kufungwa tu iwe na Man au Arsenal yote ni kufungungwa tu na inauma.

    Mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba Rise hakutakiwa kucheza kabisa maana kiwango chake kwa sasa kimeshuka sana na jana wadau watakuwa wamethibitisha maana goli la pili la drogba limeanzia kwake yeye mwenyewe badala ya kumkaba Anelka yeye anaanza kuomba asaidiwe na refa akifikiria kuwa Anelka alikuwa ameotea ni upuuzi mtupu. HUYU RISE NDO AMETUTOA SISI KAWAPA GOLI PALE ANFIELD NA STANFORD BRIDGE KAWAPA KIENYEJI ENYEJI TENA NIMEUMIA SANA ASEE TENA SANA.

    NA HUYU KOCHA WETU NAYE NI WAKUTANDIKA VIBOKO, ILE TIMU ILISHAELEMEWA SANA KWA KIPINDI CHOTE CHA KWANZA YEYE BADALA YA KUFANYA MABADILIKO ANARUDISHA TIMU ILE ILE WE UNAFIKIRI BABEL ANGEKUWEPO TOKA KIPINDI CHA PILI KINAANZA WALE WANGEWEZA KUTUTOA?? BABEL NI MPIGANAJI HASWA NA ANA FURUKU SANA ANAPOKUWA KARIBU NA GOLI SASA YEYE ANAKUJA KUMWINGIZA DAKIKA ZA LALA SALAMA AH HAYA BWANA WACHA TUWE WAPOLE SASA HATUNA CHA KUNGANGILIA MWAKA HUU.
    NA MI NITAKUWA AGAINST NA WEWE NITAWAPA SUPPORT MAN U KWA SABABU HAWA CHELSEA WANAJIDAI WAJUAJI SANA GAME 66 WASIFUNGWE KWAO WAO AKINA NANI??

    U WILL NEVER WALK ALONE.
    WILLY

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 01, 2008

    Kwanza kabisa nawapa hongera Chelsea kwa kuingia final.Watu kama Small Benitez(kama anavyojiita) sijui kama wanaelewa mpira au ni watu wa kukaa kilabuni na baadae kuulizia game imekwendaje? Moja, Chelsea huko Moscow watakutana na timu tofauti kabisa na ile waliyochza nayo majuzi. SAF aliipa uzito mechi ya Barca na alijua hata itokee lolote lile ubingwa bado uko mikononi mwetu. Wachezaji wafuatao watacheza Moscow,Tevez, Ronaldo, Evra,Rooney(atakuwa amepona), Vidic vilevile.Huyo Drogpa(jitu kubwa halafu linajiangushaangusha) hatafurukuta siku hiyo! Sisi tuliwafungeni 2 bila, nyie mmetufunga 2:1, sijui kwanini mko carried away, mambo baaaaaado. Madau William,mimi naona nimeshashindwa kwenda Moscow, kwanza hiyo bei na gharama sio mchezo. Mwaka huu nimeziona mechi 2 tu Old Trafford, nikija tena ntakutafuteni Wadau. Mimi naishi Prague, centre of Europe... Tutawasiliana zaidi. Nafurahi kuona Man Utd supporters tuko sehemu zote duniani! Glory Glory Man Utd, Viva Ronaldo.. Asante Bw. Michuzi.blog yako idumu na pole sana kwa ya jana, ndo ukubwa huo ati!Red devils will do you a favour, believe me. Have a great day wadau wote! Enjoy May day.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 01, 2008

    Mdau wa Prague nashukuru sana kwa kufafanua ,naenda jumamosi old trafford kuangalia Hammers hope fully tutawapiga maana wanarecord ya kutuharibia ubingwa kwama unakumbuka 95 nadhani blackburn walishinda na sisi tulikuwa tuna hitaji ushindi wakatubana ,any way ukija huku tutafutane tukacheki game au sio ?Michuzi tatizo la team ambayo inalenga kombe moja matokeo yake mkifungwa mechi muhimu kama ya jana mnabakia kukamilisha idadi za mechi ,i am sure mejifunza na msimu ujao mtakuwa makini ,liverpool mnahitaji wachezaji kama 3 tu strikers wawili alafu muuze vronin,crouch kwajili hapendwi mimi nampenda sana maana he is profolic sema ndio hivyo, mnunueni Ibrahimovic wa inter milan alafu muanze kucheza 4-4-2 hapo mtawamaliza ok

    William uk(united for life)

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 01, 2008

    inside information inasema mechi kati ya chelsea na liverpool matokeo yalipangwa.the government,viewed it as a recipe for disaster if liverpool went through,sources have confirmed,moscow could never been able to cope with fifty thousand liverpool and man u fans in the city,hours before the game,20 thousand fans would have been drinking in the city,the aftermath,war in the streets of moscow as a result english teams would be banned from competitions worldwide,to avoid this scenario it was decided chelsea should go through

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 01, 2008

    Wee Hatchet man acha uzushi, hio information umeipata wapi?, nyie kubalini mmefungwa tu.
    Na wewe William Uk na huyo mwenzio wa prague mnatangaza sana kuenda old traford kuangalia mechi kila post mnayotuma, hivyo vijisenti vya kubeba maboxi mkawatumie wazee wenu vijijimi kwenu wana shida, msijifanyo ubishoo saana kutaka kuwapunga watu hapa. Kuna watu hapa season´s ticket holders na hawajitangazi. Kawaongopeeni mafala wenzenu huko.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 02, 2008

    ok william tunaomba utuletee picha moja tu yako wewe ukiwa old traford usiogope kuhusu kubaniwa kwani michu karuhusu tangu jana picha za salaam. naomba uwaja uwe umejaa na isiwe adobe tafadhali. michu kama hujaruhusu naomba uiachie hii ya up coming celeb. juu kitabu chake kinatoka soon. na hints ya tittle ni FROM PAUL PARKER TO WILLY BLACK MANCUNIAN.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 02, 2008

    MIMI NINACHOJUA LIVERPOOL 4(KUYT,RIISE,TORES,BABEL)CHELSEA 3 (DROGBA 2 NA LAMPARD 1) AU NIMEKOSEA WADAU?

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 02, 2008

    Hii blog naona karibu itakuwa kama Tribal football, maneno yenye chuki yanazidi. Kwanza, mimi mdau wa Prague (kama unataka picha yangu ntakutumia,hata kama unataka nikiwa Old Trafford ntakutumia vilevile.Kwangu mimi kwenda Old Trafford it's not a big deal, sijui hiyo chuki dhidi yangu mimi na Mdau mwenzangu William inatoka wapi.Kwasababu gharama za kwenda Moscow ni kubwa sana, nimeshatangaza kwamba siendi,(labda nikufurahishe,nimeshindwa!). Mimi sijakushauri wewe umtumie mamako pesa ( and I don't give a dam where you are),unaweza kuwa Dar na ukawa husaidii wazazi wako sio lazima uwe Ulaya). Unataka copy ya cheque vilevile? Tuanze kutumia majina yetu halali,unasemaje? Hivyo nisingeshauri tuwalete mama zetu kwenye blog hii, upo hapo? Hivyo Bw. William, tutaonana tu, the world is so small. Kwanza kazi ni kesho Westham, kama unavyosema, lakini ukiumwa na nyoka... Nafikiri this time around we have all matters in our hands! Glory Glory Man Utd! Bw. Michuzi, samahani, lakini ndo hivyo, tuvumiliane kidogo.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 02, 2008

    Unajua inafurahisha sana ,wabongo wanafikiria kila mtu mbeba boxi,hi inaonesha upeo wa mawazo ulivyo mfinyu kuna wengine wanakazi zao nzuri za office na sio kitoto ,sasa wewe endelea kujipa moyo hivyo hivyo kwamba mimi ni mbeba box ila najua nachofanya na cha muhimu ni malengo yangu niyafikie, siwezi kuweka picha hapa maana itakuwa balaa maana wabongo wanavyojua kuchonga ,unajua mtu hulazimishwi kuamini kitu kama hutaki basi yaache maana haikudhuru chochote chukuliwa ni story au sio

    William uk(united for life)

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 04, 2008

    woh woh WILLIAM na mwezako camon! slow down dude . tunatakiwa tu enzi box and we are proud of it.kama hupendi box basi wewe hufai kuwa ulaya rudi bongo tu. kwa wenye kuelewa wanajua naonelea nini. mimi nafanya kazi nyumba ya maiti na mshikaji angu ni meneja wa nyumba ya wazee . zote hizi ni box. hatutofautishi. kazi ni kazi na hii mentality tunatakiwa kuipeleka bongo. tumegundua ndo siri za maendeleo ulaya. watu wana enzi kazi zao na nafasi zao. siyo bongo unakuta mfagia choo cha city anajidharau mwenyewe kama public haijamuhujumu. halafu mnataka miji iwe safi. kuna mengi mazuri ya kuiga toka huku especially work ethics. so willy feel proud man .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...