Juu ni mdau Hamza Kabelwa akilinda na kutetea nondozzz zake katika fani ya utabiri wa hali ya hewa katika chuo kikuu cha utabiri wa hewa St.Petersburg Russia.
Chini Hamza Kabelwa (Mwenye miwani na suti nyeupe) na Ofisa wa kwanza ubalozi wa Tanzania Russia Mbarouk Nassor Mbarouk wa tatu kutoka kulia mstari wa nyuma pamoja na wadau waliokuja kumuunga mkono.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. ?????!!!???!!^%*&^%$?????!!?!? What for 4?

    ReplyDelete
  2. Hakuna kazi ya kutabiri hali ya hewa bongo. Unatabiri hali hewa ya nini huku?! Sisi tunajua kila kitu mwanzoni mwa mwaka. Isitishe ya hewa bongo ni tarambarale kila siku!

    ReplyDelete
  3. Hongera ndugu yangu. Muwe mnatupa na link tusome hizo tasnifu maana zinaandikwa ili tuzifanyie kazi au tupate ushauri wa utafiti wako kutoka humo kusaidia maendeleo ya nchi yetu na dunia kwa ujumla.

    Kaka michuzi hatushangai mtu kupokea madongo hapa, maana watakao mpongeza ni wachache kuliko kama ungetundika picha akiwa analegeza zipu huko Big Brother Africa!

    ReplyDelete
  4. Mdau ulietangulia naona unaupeo finyu kuhusu hali ya hewa kutokana na watu wente upeo kama wako ngazi za juu serikalini mbali na kufahamishwa na wa wataalam wa hali ya hewa ujio wa ukame walipuuza matokeo yake taifa liliyumba kutokana na umeme lililotokana ukame na kukauka kwa vyanzo vya maji,wataalam hawa mbli na kazi yao kutegemewa na usafiri wa ndege na meli pia wakitumiwa vizuri na kupewa vyombo vya kutosha wanaweza kupunguza maafa yatokanayo na Vimbunga,mafuriko,ukame n.k.HONGERA BWANA KABELWA NA WATAALAM WATE WANAOTOA MCHANGO MKUBWA KATIKA UJENZI WA TAIFA LETU.

    ReplyDelete
  5. Huku Africa hali ya hewa tambarare kila siku. hatuhitaji watalaamu kama wale wa CNN. Kama uamini, maliza shule yako urudi. Uone kama utapata kazi huku!

    ReplyDelete
  6. YAANI HIZI POST ZOTE ZINAASHIRIA UMBUMBUMBU WA WATANZANIA , NATAKA HADI KULIA MACHOZI HII NI SERIOUS ISSUE WE UTASEMAJE TANZANIA HAIHITAJI UTABIRI WA HALI YA HEWA WAKATI WEWE MWENYEWE UNAISHI MABONDENI MVUA IKIJA FAMILIA YAKO IKIFA KWENYE MAFURIKO UNAANZA KUILAUMU SERIKALI AHHHHH!!! MI NALIA MACHOZI NAJUA SIO TATIZO LAKO ELIMU HAUNA ULIKIMBIA SHULE...HABARI NDIO HIYO

    ReplyDelete
  7. Hapa Naona Watu badala ya kupeana moyo katika maendeleo hususan ya Kielimu mnaamua kuandika habari za ajabu ajabu.
    Mimi mwenyewe nilikuwepo katika siku hiyo ndugu yetu huyu amepata PhD. katika fani ya Hali ya Hewa ...au kwa lugha ya kitaalamu sasa Ni Dr. in Physical Mathematical Science ... ni kitu nadra na cha kujivunia sio tu katika nyanja ya Hali ya Hewa bali vile vile kwa nchi yetu kwani mchango wake na elimu aliyoipata ataleta mchango mkubwa sana katika njanya nyingi hususan mazingira, hata kutoa lectures katika Vyuo vyetu vikuu ambavyo vinahitaji wataalamu kama hawa.
    Mwisho kwa maoni yangu naona wote hao ambao wanaandika negative comments sidhani hata kama Degree moja ndio maana wanakosa la kusema maana hawaelewi maana ya Elimu
    HONGERA SANA NDUGU YANGU DR. HAMZA KABELWA kwa kutunukiwa shahada ya Juu kabisa kimasomo(PhD) jana

    ReplyDelete
  8. MDAU ALIYEPONDA NAMSHAURI AKAANGALIE SINEMA INAYOITWA "DAY AFTER TOMORROW" NI HAYO TU.

    ReplyDelete
  9. hongera hongera kaka kwa kuchukua nondo yako..tunakupongeza kwa kila hali na mali
    kwa kukuhusia kaka nakuomba ujitayarishe vizuri utakapo rudi nyumbani ili uweze kuitumia elimu yako vizuri na kutoa mchango wako vyema...nikiwa nina maana..wengi waliopta nondo za fani ya juu kama yako,punde wanaporudi nyumbani wanakosa kupewa ushirikiano na ngazi zinazohusika.kuhitimisha fani zao za kielimu..matokeao yake wanaangukia kwenye ufisadi au kuwa wala rushwa wakuu.wanasahau kutoa mchango wao wa kielimu,na hii yote inatokana na mfumo wa wanasiasa wetu wa tanzania!!!!nina chokushauri kama wewe utaweza kupata ajira nchi za jirani kama botswana au namibia.wewe nenda ukaitumie elimu yako vizuri...mimi sitaki kukukatisha tamaa..lakini hiyo ndio hali halisi ya tanganyika..elimu haina mahala pake..wasomi wananyimwa nafasi za kuendeleza nchi,matokeo yake labda uwe mpambe wa wanasiasa au ccm..upate ulaji wako..habari ndio hiyo..nakutakia kila la kheri katika fani yako ya elimu...

    ReplyDelete
  10. Hongera sana kaka. Hapo namuona Kaka Pascal, dada Vero Mgalula... dada vero hilo gongo kulikoni??

    ReplyDelete
  11. WAcha wewe! Kuishi mabondeni bila TV wala radio na hiyo degree yako hakuwezi kunisaidia kukwepa mafuriko. Pia hata kama ukitabiri kuwa yanakuja, siwezi hama maana hapa ndipo babu na bibi zangu wote walipozaliwa na kufa! Ndiyo maana nikakwambia kuwa wewe hiyo shule yako huku hatuihitaji kabisa na unaweza usipate kazi daima!. Unasomea hali ya hewa?!!? For what? CNN na BBC huko, bongo kila mtu anajua mambo ya kesho.

    Na annon wa 3:18 day after tommorow hakuna anajua. Tunajua leo tu. Achana na methali zako hizo. Huwezi uakapanga issues za kesho wakati leo jioni huna uhakika wa kuishi!

    ReplyDelete
  12. PK-one, hapa bongo uhitaji degree kuwa na hela. Unahitaji kichwa tu. ndiyo maana wasomi wote ni mafisadi wakati wasio na shule ni matajiri bila ufisadi! Na 90% ya wenye hela hapa ni wasio na shule. Kalaga bao na shule yako huko!

    ReplyDelete
  13. Kwanza kabisa ninamshuruku Bro Michuzi kwa kutoa nafasi hii watu kujadili masuala yanayowahusu wao wenywe, hali ya hewa.

    Kwanza kabisa napenda kuwafahamisha kuwa, kwa wale wasiojua, HALI YA HEWA HAINA MIPAKA, madhara yake yanaweza yakaathiri popote pale duniani, ikiwemo Tanzania.

    Nimefurahi kuona kuwa watu wana hamu ya kujadili na hii inasaidia kujua takwimu za uweleo wa watu. Hii infurahisha sana

    Mabadiliko ya joto duniani (global warming-climate change) ni masula ambayo sasa hivi dunia inaitambua na madhara yake ni makubwa sana. Hali ya hewa kama iliivyo, inajihusisha na mambo mengi, karibuni maisha yote ya vuimbe hai.
    Mazingira: Moshi chafu kutoka viwandani (Viwanda vinaweza kuzuiwa kufanya kazi) na magari chakavu katika miji mikubwa (afya)) yanaweza kusababisha kuporomoka kwa uchumi wa viwanda na kuyumba kwa afya kwa ujumla.
    Usafiri: Kukosa kujua hali ya hewa baharini, angani inaweza kusababisha kupoteza kwa kiasi kikubwa kipato cha nchi yeyote ile duniani. Hapa nadhani kuwa inaeleweka wazi kuwa usafiri wa anga na majini (pamoja na uvuvi hihiyaji saaaaana taarifa ya hali ya hewa).
    Majanga: Moto katika misitu, mafuriko, ukame pamoja na mambo mengine madhara yake hupungua endapo hali ya hewa itajulikana kabla (utabiri). Mtoa hoja aliyetangulia aliguzia kuhusu pointi hii

    NGUVU (ENERGY); na Mipango miji na miundombinuni: Inategemeana sana kwa kiasi kikubwa taarifa ya hali ya hewa
    Vinginevyo: Utalii, burdani, michezo, n.k. Mafano ni mechi ya Taifa Stars na Msumbiji ambayo haikufanyika siku za nyuma kwa ajili ya mvua kubwa, TFF ilipoteza kiasi kikubwa sana cha fedha.

    UCHUMI: Kutokana na vipengele vichache vilivyotajwa hapo juu, uchumi wa nchi yeyote ile duniani unategemeana sana taarifa ya hali ya hewa.

    USHAURI. Kwa wale watakaokuwa na hamu ya kujua zaidi na wapo Tanzania, wanakaribishwa Ubungo Plaza ghorofa ya 3 kwa ushauri zaidi.

    ReplyDelete
  14. Kanemba kapata mpinzani.

    ReplyDelete
  15. Ahaaaaa ndiyo watu wangu wa Piter naona watu mnaiva tu..vipi winter...hongera bwana Hamza umevuta pumzi ...naona Piscal nyuma hapo naye anachukua PhD nini?? ee bwana huyu chini si Masatu karudi lini Petersburg...? halafu mwenye suti nyeusi si Bob huyu du uwezi kuamini jamaa alivyokuwa mtu wa ma-jens(nasikia jamaa ni Doctor tayari ) safi sana lakini jamani mrudi nyumbani wanawasubiri sana PhD -graduate, hila kwenye list hii sijamuona Shabani na Nurdin wazee wa Piter vipi wakina Natasha jamani mie nawa-miss sana
    Mdau wa Denmark

    ReplyDelete
  16. Hongera sana Kubelwa, achana na hawa mambumbumbu wakubwa ambao ndio wanaididimiza tanzania, eti mtabiri wa hali ya hewa hahitajiki CNN inatosha...nini? hiyo inaonyesha wazi umbumbumbu uliotukuka, fani hii sasa inahitajika kupita kiasi, ..na si lazima uje kufanya kazi tanzania ..kama hawatakuhitaji kuna sehemu kibao duniani zitakuhitaji..wenzetu wanasema do not expose your ignorancy...poleni mambumbumbu!

    ReplyDelete
  17. Hongera sana Dr.!

    ReplyDelete
  18. Nasikitika kwa baadhi ya watu kutoelewa ni jinsi gani mtandao wa hali ya hewa jinsi gani unafanya kazi niushirikiano wa hawa wataalam wa hali ya hewa kutoka katika vituo mbalimbali vilivyosamba kote ulimwenguni setelite ndiyo zinzotoa matokeo kamili ya hali ya hewa katika sehemu mbalimbali ulimwenguni hivyo jamaa anaesema CNN au BBC inatosha namfananisha na jamaa anaesema hakuna aja ya kulima pamba kwani kiwanda cha nguo mwatex kinatosha au hamna haja ya kulima kahawa kwani Bukop kipo!!!!!!!

    ReplyDelete
  19. We anon unayesema 90% ya wenye hela hapa ni wasio na shule. acha kudanganya umma hizo data umezipata wapi? Pili, acha umbumbumbu kuwa na shule siyo kuwa na pesa, huo ni wivu na umbumbumbu unafikiri america ingeendelea bila kuwa na wasomi? Nenda kasome angalau kakozi kadogo upunguze umbumbumbu.

    ReplyDelete
  20. My dear brothers and sisters. It is easier to make ten millions TShs. illegally than ten TShs. legally. But it is safer to make ten ten millions Tsh. legally than ten Tsh. illegally.Education is not for richness. This has been attributing to many students to parsue degrees, diplomans, certificates and so on but not knowledge. They 'desa' and forge extremely to get those things and to acquire knowledge. Furthermore, forged leaders are many in governments with fake degrees and certifaicates.Who will point finger to others?. The contributions on this topic show exactly what is happening and where are we going.Giant man or beatiful woman seriously argue that there are many rich people without education meaning eduacation is richness.We need to chnage Tanzanians, yes We can.Every body should taught if not reminded the difference between richness and education.Newton,Einsten,Planck and others great scientists did well on this world. I dont think that they richest people on their era.If they had looked for richness through their sciences, I hope we would have not enjoying this marvelous of technology.Please Tanzanians invest in education. We need changes in economic,politics and social things. I heartly congratulate those have been sacrifing their time and resources in education for benefit of our beloved country and world in general include the above mentioned person.Thank you very much and God bless each one.


    kahama

    ReplyDelete
  21. hatuhitaji kuwa na utaalamu wa hali ya hewa kwetu TZ. Kuna issue muhimu zaidi za kushughulikia. Hali ya hewa ya nini? Watu vijijini huko kama jamaa alivyosema hapo juu hawana umeme wala radio. Hali ya hewa yako wataisikia wapi!? Tunajitaji vitu vya maana nchi hii na si hali ya hewa. Hali ya hewa ya kufanya nini?
    Miaka ya nyuma pale Kibaha secondary kulikuwa na mtaalamu aliyebobea wa Electronic. Miaka ya 80. Aliishia kufundisha secondary kwa kuwa hiyo electronics angeifanyia wapi! KWa ILIKUWA ni wrong choice ya taalum kwa wrong time.
    Hivyo hivyo jamaa wa Hali ya Hewa wewe. Labda ukanyie kazi aiport kuongoza ndege, ambazo, anyway, siku hizi kabla haijaruka inakuwa imesoma route nzima hata kama ni km 20,000. Kwa hiyo usije ukawashawishi vijana waje wasome hali ya hewa wakati future yako itakuwa blink!

    Namuunga mkono jamaa pia kuhusu watu wenye pesa bongo. Kwa taarifa yako kuwa na pesa na shule ni vitu tofauti. Marekani iliendelea kutokana na wakulima. Mambo ya shule ya juzi tu. Wewe kama unasoma ili uwe jaribu, forget about!

    ReplyDelete
  22. Jamaa aliyetoa maoni yake sasa hivi naona anachanganya vitu lengo au majukumu ya kitengo cha hali ya hewa sio kumtaarifu mwana kijiji leo kutakua na joto kali au mvua au baridi ingawa hilo nimoja ya majukumu yake na umuhimu wake.Nyuma ya wataalamu haw kunakazi kubwa kufuatilia mabadiliko ya hali ya hewa na athari au manufaa yake katika mazingira.Mfano Kama taifa au viongozi wa taifa watafahamishwa mapema ujio wa ukame katika kipindi kijacho na ukame huo utakua kwa kiasi gani unawapa viongozi hao uwezo wa kupanga mikakati yao kuhusu ifadhi yachakula matumizi mazuri ya chakula tulichonacho n.k.Chukulia ya kua mwakajana au miaka mitano mavuno ya ya chakula yalikua mazuri hamna taarifa yoyote nini kitakuwepo mwaka ujao tukamua kuuza idadi kubwa ya chakula tulichovuna tukiwa tunategemea mwaka ujao utakua kama mwaka jana ghafla ukame au mafuriko! Unaposema marubani wanaweza kusoma route nzima hata kama KM 20,000 nani anaandaa hiyo taarifa inayomfanya rubani aisome route hiyo?!Ni hao hao wataalamu wanaoandaa taarifa hiyo.Kila taaluma inaumuhimu wake katika jamii.Kwa bahati mbaya wengi wetu maswala haya tunayachukulia kwa upeo mfinyu au kotoelewa.ili uandike hayo unayoyandika katika mtandao huo wa Mbunde wa nanii lazima afanye kazi yeye na timu yake mafundi wa kumpyuta,website,setelitte na wataalam chungu nzima ikiwemo wataalaam wa hali ya hewa.Hivyo ndugu yangu hilo unapaswa ulielewe sio kwamba vitu vinazuka tu.

    ReplyDelete
  23. Hapa hatuongelei umuhimu wa kitu. Kila kitu kina umuhimu, iwapo ukikijengea hoja. Ndiyo chuo kama hicho kinatoa taaluma hiyo! In fact tunaongelea kuhusu future ya hiyo fani kwa Tanzania. Hatujazoea mambo ya planning kwa kuangalia hali ya hewa hapa. Ndiyo maana hata taarifa zetu za habari kwenye TV, inapofika hatua ya utabiri wa hali ya hewa watu karibu wote wanabadilisha channel! Ni kitu ambzchi hakipo kwa maisha ya kawaida ya mmbongo!

    ReplyDelete
  24. Ni kweli jamani, hizi fani zingine tuwe waangalifu sana. Labda kama katumwa na idara ya hali ya hewa, mimi sioni sababu ya kumruhusu mwanangu au kumshauri ndugu yangu kusomea mambo ya hali ya hewa! Sawa sawa na mtu aende akasomee Nuclear physics! Juu ya nini yote hapo kwa bongo?!

    ReplyDelete
  25. yote hapo kwa bongo?!
    Bado inasikitisha na inafurahisha kuelewa kuwa bado sisi watazania kuna baadhi ya vitu sisi umuhimu wake hatujaujua.
    Watanzania wengi wanapobadilisha TV baada ya taarifa ya habari ni kwa vile hawajakuwa na haja ya hiyo taarifa ya hali ya hewa. Kwa watu wenye sherehe na ujenzi wa bara bara huwa wanafuatilia sana hizi taarifa, wajezi wa maghorofa vile vile huwa wanfuatilia sana, kwa mfano kama kuna RADI hawarushusiwi kuwa katika high points, n.k.
    Kuhusu Nuclear physics, hapa tena ndio unapoteza umma kabisa mtoa hoja uliyepita. Sasa hivi Tanzania tumekwama, umeme wetu unategemea saaaana maji tu. Sasa hivi nchi nyingi zinatumia Uranium ili kuzalisha umme, ambao ni bei nafuu sana. Gharama za uzalishaji umeme zikiwa ndogo, basi ni faida kwa wananchi. Taiafa limetumia fedha nyingi ili kuleta wataalam toka nje ili kuweka mitambo ya kuzalishia umeme kwa mfano GAS. Mimi nadhani kama kuna kitu hatukielewi ni vizuri tupate ushauri kwa wataalam wanohusika.

    Kama alivyosema mtoa hoja aliyepita kuwa Kila kitu kina umuhimu wake.

    ReplyDelete
  26. hahahaaa inafurahisha sana kuona mjadara wa taaluma unavyokwenda hapa na kwa kuheshimu mchango wa kila mtu mawazo haya ni mazuri sana kwani yanaonyesha ukweli kuhusu mawazo ya watz na kwa nini tz masikini.
    Taaluma ya hali ya hewa na taarifa zake ni muhimu sana kwa kila nchi ila kwa watz au nchi nyingi ambazo wananchi wake bado hawajaelewa umuhimu wa hali ya hewa kwa ujumla ni zile nchi masikini,ambapo mara nyingi wananchi sisi wa nchi hizi badala ya kujifunza ni kwanini huwa tunasema hili halitufai na kupiga porojo nyingi vijiweni! Kiuharisia wa mambo siwezi kumlaumu mtz kwakutoelewa au kwa kuhoji ni wa nini wataalam hawa hapa nchini ila nikumpa changamoto ya kuongeza kidogo uwezo wakufikiri na kunza kufuatalia taarifa hizo ili tuweze kufikia kule tunakotaka taifa lifike( taifa lenye maendeleo)!! Elimu itolewe kwa watz kuhusu umuhimu wakupangalia mambo na kufuatilia taarifa za hali ya hewa, na ni changamoto hata kwa Idara inayohusika na mambo haya ya hali ya hewa hapa nchini kwasababu watz tuliowengi tunadhani hali ya hewa ni utabiri tu!.tuangalie utabiri natupende kujifunza kama vipi serikali igawe zile pesa zetu za EPA NA KILA KIJIJI KITOE MTZ MMOJA(ZINATOSHA NA NYINGINE ZITABAKI) AKAELIMISHWE KUHUSU HALI YA HEWA NA UMUHIMU WAKE ALAFU AKIRUDI KIJIJINI ILE KUSIMULIA TU WENZAKE BASI MWAMKO UTAPATIKANA NA KWA HAKIKA BAADA YA MIAKA 100 WATZ TUTAKUWA(WATOTO NA WAJUKUU WETU) NA MAENDELEO HASA KWA KUWA BADO TUNASEMA KILIMO NDIO UTI WAMGONGO WANCHI HII,KILIMO KINACHOTEGEMEA MVUA NA WATZ HATUFUATILII TAARIFA ZA HALI YA HEWA NI KAZI SANA KUELEWA SERA ZA SERIKALI NA MTAZAMO WAWANCHI ILA LAZIMA TUWEKEZE KWENYE MIPANGO ENDELEVU! taalumu zote na wataalam wake ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi, kila mtu kwa mchango nanafasi yake atachangia maendeleo!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  27. Achana na hali ya hewa wewe! Soma Kilimo na uvuvi. Hali ya hewa haina mpango.
    Wewe wa nuclear physics nadhani ndiyo uko nje kabisa ya mstari. Wapi Africa hapa nchi inatumia hiyo Technology?!! Wa-Iran wanasisitiza kuwa wanataka umeme kwa hiyo technologia, lakini Israel na Marekani wanataka kuwashughulikia! Unajua sababu!!? Au wewe ndiyo umekariri tu kuwa nuclear reaction inaweza toa nishati, basi inatosha?!!
    Hapo Congo wana Iranium kibao. Thubutu kanunue uone kilimchomponza kuku kwa mwewe!

    Kalaga bao na hali ya hewa yako!

    ReplyDelete
  28. hahahaha! Unasema hela za EPA zikasomeshe hali ya hewa?!! Unacheza wewe! hali ya hewa ukienda kwa Mganga wa kienyeji anakupa full zoom ya week nzima! Usome nini hapo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...