mkurugenzi mtendaji wa tanesco dk. idris rashid akiwasili kuongea na vyombo vya habari jana makao makuu ya shirika hilo huko ubungo dar, ambapo . dk. rashid alitangaza uamuzi wa kujitoa kwa shirika hilo katika nia ya kununua mitambo ya kufua umeme ya Dowans.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya kutolewa taarifa alizodai kuwa ni za uongo na zilizojaa utashi wa kisiasa zaidi, dhidi ya utaalamu wa Tanesco na kwamba zimechangia kuvunja nguvu ya mamia ya wafanyakazi wa shirika hilo wanaofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha nchi inapata umeme wa uhakika.
ndugu mdau hebu toa maoni yako juu ya uamuzi huo wa tanesco.
habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. ...uvundo mtupu. Bora wangehacha kazi na kutoa nafasi kwa wengine wenye mapenzi na nchi waendeshe TANESCO. Wamefikia kiwango chao cha mwisho cha utendaji kazi, ubunifu wao umefika mwisho na hawana la ziada zaidi ya kuangalia maslahi binafsi. Waondoke tumechoka!

    ReplyDelete
  2. Mkurugenzi mkuu angejiuzulu ili kuweka msisitizo kwenye nia yake njema ya kulinda nchi isiingie kwenye kiza.

    ReplyDelete
  3. Msimamo na maneno ya Mweneykiti wa kamati ya Nishati bungeni, eti bora tukae giza ni kama yale ya wti bora tule majani.
    Naona mafahari wakigomaba ziumiazo ni nyasi

    ReplyDelete
  4. Kama kanuni za manunuzi ya vifaa vya serikali ni kununua vitu vipya, sioni sababu wala mantiki ya tanesco kung'ang'ania kununua mitambo ya dowans, tena mjukuu wa mzee richmonduli ambaye kesi yake bado haijapatiwa ufumbuzi. Hawa wamangimeza akina dr idris rashid wamekalia madaraka muda mrefu na kufikia kujisahau. ni vizuri washutuliwe. bongo hadanganywi mtu siku hizi!!!!

    ReplyDelete
  5. Richmond na Dowans ni kampuni moja tu...mbona hatukupata maelezo ya vipi huu mkataba wa Richmond ukapelekwa kwa Dowans...

    Halafu na huyo Dr Idrisa kweli ana Ph.D ya kuwa dokta au ni cheti cha feki??? Mafisadi hao wote tunawaona wazi wazi..lakini badi wanaendelea na wizi wao..

    ReplyDelete
  6. WIZI MTUPU.

    Siyo KUJITOA bali wameTOLEWA NJE.
    Baada ya Makelele ya wananchi hasa wanasiasa wasio na Mgao katika huo mshiko, Huyo Boss Idrisa kwa kuona mbali kwa Udaktari wake, ameona kuwa mbele ni KIZA hivyo kajiwahi mapema ... NI ULONGO LONGO tuu!!

    Walishachota kwa funguo za RICHMOND, baada ya kutemwa sasa walijiandaa kuchota za mwisho kufunga kazi.

    Sasa hizo mashine wakakaangie mishkaki.

    MASLAHI YA TAIFA MBELE WANDUGU.

    ReplyDelete
  7. Sikuwahi kujua km huyu mkurugenzi anaweza akatoa statement ya chini ya kiwango kama aliotoa hapa. AJIUZULU TU APISHE WENYE UWEZO.

    ReplyDelete
  8. Mtoa maoni wa 4.24 hapo juu, nilidhani unataka kupendekeza kuwa wawaachie wanasiasa waendeshe Tanesco maana kama wanasiasa hawataki ushauri wa wataalamu hao watu wapya unaotaka waingie kuendesha tanesco watafanyaje kazi? Kwa hali ilivyokuwa ilikuwa lazima Tanesco wajitoe, jambo hili lilifanywa la kisiasa na mnafahamu wanasiasa wakianza kuongea wana ushawishi hata bila hoja ndio maana waandishi nao wakashawishiwa na kuingia ktk mchezo huo. Hakuna aliyetaka tena kufanya utafiti wa kina kwa hiyo wananchi tukaachwa bila kufahamu ukweli ni upi, vyombo vya habari kwa wiki moja iliyopita tayari walikwisha wahukumu Tanesco. Kwa mtu yeyote asiyependa kuharibu jina ni vigumu kuanza kujibizana wa wanasiasa ambao utaalamu wao ktk suala hili ni mdogo au haupo kabisa. Sasa itabidi serikali ifanye uamuzi wa suala hili kwa kushirikiana na wanasiasa maana ndivyo tunavyotaka.

    ReplyDelete
  9. BONGO! dili imeshtukiwa iyoo sio bure

    ReplyDelete
  10. Miaka ya 70 kuelekea 80 kwa vipimo vya world bank TANESCO ilikuwa miongoni mwa makampuni katika kumi bora ya mashirika ya umma Afrika. Enzi hizo za Mwalimu walikuwepo akina Mhavile na Mzee Mosha, Very committed managers na TANESCO ilikuwa na mipango ya muda mrefu na wakati. Hivi kilitokea nini baada ya hapo. Akaja Mwinnyi Mosha akafa. Mhaville akafukuzwa akapata kazi Lesotho baadae akafa. Akaja Baruani Luhanga. Pole pole awamu ya 3 ikaingia na ndoto zake za ubinafsishaji. Ikatengenezwa dili ambalo architect mkuu alikuwa shemeji ya mheshimiwa BWM. Sombody Joe wa BOT. Akaileta Netgroup Solutions. Loo matatizo yakazidi. Mipango ile ikatupwa kapuni TANESCO ikawa sasa inanedeshwa kwa mipnago ya dharura kupitia IPTL, RICHMOND. Na sasa DOWANS. Wanasiasa wengine wanataka na wengine hawataki. Sasa masikini Idrisa Rashid alikuwa amekabidhiwa aiamshe TANESCO sasa anakwamishwa.

    ReplyDelete
  11. Wizi Mtupu!!!

    ReplyDelete
  12. Anony wa 10.11 pm March 07 nakuunga mkono kwa kutukumbusha mbali. Ni vema TANESCO wamejitoa katika hili suala la ununuzi wa mitambo ya DOWANS. Lakini hebu tuangalie repucursions zitakazotokea, ni nchi kukaa gizani kama wanasiasa wanavyotaka. Endapo tatizo hili litatokea watakaolaumiwa ni wataalam au wanasiasa?

    ReplyDelete
  13. Mimi nimeshangazwa sana na zito kabwe na Idrisa Rashid kwa statement zao. Kwa heshma ya Idrisa sikutegemea kama angeweza kutetea jambo kama hilo huku akijua kuwa Dowans imewashtaki na bado kesi inaendelea, na kuwa sheria ya manunuzi imekiukwa kwa asilimia 100, na kwamba Tanesco haikuridhia contract ya richmond tangu mwanzo. Sasa hii unatufanya tuamini kuwa huyu jamaa ni mnafiki tu na yeye hana tofauti na mafisadi wengine. Pili ni uki-geugeu wa zito, hii inaonyesha unafiki alio nao na uchu wa madaraka na pesa. leo anajifanya mpiganaji kwa ajili ya watanzania na kesho mpiganaji kwa ajili ya ufisadi. na huu nahisi ndio utakuwa mwisho wake, kwani njia ya mwongo ni fupi. sasa tunakuona mpiga kelele aliyekosa dira tena.

    ReplyDelete
  14. MKUU WA WILAYA KWA NINI WAKEREKETWA HAWAJADILI KUWA SERIKALI ILITAKA KUNUNUA MASHANGINGI ZAIDI YA 700 KWA VIGOGO AMBAYO NI MAPYAAAA!ILI VIGOGO WATESEEE NA SISI WALIPA KODI TUNAKULA VUMBI ILE MBAYAA NA BARABARA ZETU MBOVU,UMEME HAUELEWEKI ,SHULE NZURI HATUNA,HOSPITALI MADAWA HAKUNA,MAWIZARANI HAKUNA COMPUTER ZA KUFANYIA KAZI,NA MAMBO MENGINE MENGI SANA AMBAYO YANATURUDISHA NYUMA KIMAENDELEO WAKATI PESA ZIPO ZA MASHANGINGI NA PESA ZA KUTENGENEZEA VITAMBILISHO AMBAVYO WALA SIO YA KIPAUMBELE?HIVI HAWA WANAOJIITA MA DOCTOR MAWAZIRI HAWAYAONI?HIZO PHD WAMEZIPATIA WAPI?HAWAONI NCHI ZA WENZETU ZA AFRICA ZINAVYOENDELEA FASTA?WAKAE WAKIJUA SISI HUKU NJE WATU TUNA HASIRA SANA,TUNAPIGA BUKU ILE MBAYA TUJE KUCHUKUWA NCHI YETU NA NAAMINI TUTA CHANGE VITU VINGI TUU INSHALLAH!
    MUNGU IBARIKI BONGOLAND!!!!

    ReplyDelete
  15. Kama nilivyosema awali wananchi tumekosa uchambuzi wa kina kujua ukweli ni upi kwa hiyo kila mtu anatoa maoni kutegemea na hisia na wengine wakihukumu kabisa, ninadhani hatuwatendei haki tunaowahukumu na ndio maana ilikuwa muhimu kwa Tanesco kujitoa ili wanasiasa (ambao ni pamoja na serikali)watoe uamuzi ambapo tukikaa gizani au kuingia katika gharama kubwa zaidi watalaumiwa wao kama ambavyo imekuwa kwa miradi mingine.

    ReplyDelete
  16. Bwana Idris, unaheshimika kwa umri, nafasi yako katika jamii, na elimu uliyonayo. Unafahamu fika jukumu lako kwa nchi yetu.

    Taratibu zinazotumika kwa nchi nyingi duniani anapotakiwa mzabuni (supplier), ni kuwa na kampuni zaidi ya moja, ili kuzishindanisha na hatimaye kupata moja iliyobora.

    Lakini unawezaje kutoa kampuni moja tu ijadiliwe na unasisitiza kuwa kama haitachguliwa nchi inaingia kizani?

    Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza hapa, ambayo majibu yake unayo mheshimiwa. Kwanza wewe unasimama upande gani? una mtetea nani? umepokea nini kwa hawa unaowatetea? na kama nchi itaingia kizani kuna umuhimu gani wa wewe kuendelea kukalia kiti hicho, au kuna umuhimu gani wa kuwepo kwa Tanesco.

    Umeme siyo bidhaa kama bidhaa zingine ambazo watu binafsi huweza kujinunulia wenyewe, au kujiagizia wenyewe kutoka nje. Ndiyo maana kukawepo na kampuni maalum iliyopewa jukumu hili.

    Unatakiwa kurudi kuwaomba radhi Watanzania, na kutafuta ufumbuzi sahihi wa tatizo hili na siyo kutishia watu au Wabunge n.k.

    Takriban decade tatu sasa jina lako limekuwa miongoni mwa majina ya viongozi wachache wanaofahamika kwa utendaji wao mzuri, tangu ulipopewa kuongoza NBC, ndiyo maana ukakumbukwa tena na kupewa nafasi hiyo. Lakini sasa inaonekana umeanza kuchoka kufikiri.

    Sasa hivi takwimu zinaonyesha kuwa watanzania wanaopata shahada za Udaktari (PhD), inaongezeka kwa kasi. Na wa uwezo wa kuongoza. Usije kudhani miaka hii ni ile-ile ya 47.

    Ndugu zangu, tenda ni lazima iwe na wazabuni zaidi ya mmoja (ndiyo kawaida), ili kamati husika zione nani ana-record nzuri ya utendaji, gharama nafuu, technolojia inayoendana na karne hii n.k.

    Ukiweka kampuni moja tu, unaishindanisha na nani Wabunge, au Wananchi?

    Mdau
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  17. Kuna mijadala aina mbili. Mmoja ni suala la taratibu za ununuzi. Bunge sio kazi yake kuchambua au kutathmini manunuzi. Pia utendaji wa kamati za bunge unaingiliana wenyewe na kushindania maamuzi. Umauzi ni wa serikali huku kamati ya fedha ya (Zitto) na kamati ya Madini (Mwakyembe)zinatoana jasho na kuna mambo ya wanamtandao.
    Sasa inakuaje kutafuta Bunguliso? Tanesco wametoa ushauri wa kitaalamu, wanaoshauriwa ni serikali, ni juu yao kukubali au kukataa ushauri.

    Sasa hizo kamati zinatafuta pia sifa kuita watu mafisi au mafuso. Kitu chochote kinachofanywa bayana kama walivyofanya TANESCO hakina kificho na wametoa tahadhari. Eti tahadhari ni kitisho. Sasa tahadhari anazotoa Mhita juu ya vimbunga au mafuriko kwa watu wa mabondeni kwa nini hatuoni shinikizo? Ila hili la giza ndio liwe la shinikizo?

    Sasa hivi nchi inakabiliwa na njaa, watu watunze chakula cha akiba, wafanyi biashara wanaruhusiwa kuagiza chakula bila ushuru, je kwa nini tusiseme nacho ni kitisho, cha mafisadi waagizao chakula?

    Ukame unaoleta upungufu wa chakula ndio huo huo ukame utakao kausha mabwawa na kuleta upungufu wa maji ya kuzualisha umeme?

    Sasa bunge linataka kuendesha mahakama, kutafsiri sheria, kuendesha mashatka na kuhukumu. Pia linataka kuendesha serikali na mashirika yake kwa gear ya eti ni wazalendo. Wapewe kazi ya kununua hio genereta mpya kutoka huko Houston na kuifunga kwa muda wa wiki 2 kama wanavyosema.

    Msomi na msema kweli kama Rashidi hawawezi kufanya kazi nchi hii. kwa sbabau nchi hii na wanasiasa wao wanataka kudanganywa na kupewa bahasha. hawataki kuambiwa ukweli.
    Dr. Rashidi ni bureacrat, sio mwanasiasa ni bora kujiuzulu ufanye kazi zingine kwani unahitajika sehemu nyingi. Kwani ni lazima kwako kufanya kazi ya umma?

    ReplyDelete
  18. Aina ya pili ya mjadala inahusu watu an hulka ya watu. Haihusu umeme, giza au taratibu za umeme. Zinahusu majina ya watu na dhana ya kuwa kuna ufisadi au harufu ya ufisadi.

    Wanaojadili wanafuata kambi ya Zitto (mahesabu ya umma/tija na mapato ya serikali.Kambi hii pia inasimamia sheria ya ugavi.

    Lakini kambi ya pili ni ile ya kamati ya nishati. yenyewe ni ile kamati ya Richmomd. Ununuzi wa mitambo ya Dowans hata kama ingekuwa mipya ni kukubali kushindwa na kubariki yale yalio mtoa lowasa na kuvunjwa kwa serikali.

    Hili kundi la pili, ni bora nchi iwe gizani kuleta hoja ya Richmond bungeni wakati hoja ilikwishwa fungwa. Ni kufungua majadala ambao RA alitaka kuuibua akazimishwa. Spika nae naona bora mjadala ule uzimwe tu kwa nia yoote ile hata kama tutakaa giza kwa sababu mjadala ulisha zimwa.

    Njia rahisi ni kuitisha serikali, kuitisha TANESCO na kuwapa majina kina Rashidi, Ngeleja na Zitto kuwa ni mafisadi na tukikaa giza si kitu kwani tulishaambia tutakula majani.

    Mimi namuunga mkono Rashidi kunawa mikono na kuwa suala sasa ni la kisiasa. Pia angefanya maadalizi ya kutafuta zabuni ya mtambo mpya na halafu kupeleka options mbili. Moja ya kununa Dowans na ya pili kununua hio mipya akionyesha faida na gharama za kila options.

    Hoja yake ingeishia kusema wametoa ushauri kwa options mbili. Ziada ya maelezo kuwa hawapaswi kulaumiwa zilikuwa ni nyongeza ambayo watu wa mijadala ndio wataona kuwa ni mada kuu. Huu nao ni ufinyu wa wadau wengi wanaotoa comment zao.

    ReplyDelete
  19. taratibu za ununuzi ziko nyingi. Hii nayo pia ni taratibu chini ya Sheria husika. Sasa hebu tujiulize hizo machine zilifungwa tayari pale dar ziko ngapi hata iwe kuna ushindani hata kuwe na zabuni? Direct purchase ni moja ya njia za ununuzi.

    Sheria inakataza kunua bidhaa isio kuwa mpya. Sasa, mitambo ilijengwa ni biadhaa? Hiyo serikali ingeomba tafsiri ya mahakama. sasa bunge kuvamia kutoa tafsiri ni kuingilia kazi ya mahakama. Hii sasa ni hatari zaidi hata kama Sita na mwakyembe ni wanasheria.

    ReplyDelete
  20. Wadau inaonekana Dr. alitaka kuwa mwanasiasa lakini hajafanikiwa, anadai kuwa yeye na timu yake ya 'wataalamu' lakini vitu vidogo sana vimewashinda kuelezea, aidha wamechoka au ilikuwa kweli bomu au kushinikizwa na wakapata kigugumizi. Vitu vyenyewe ni kama ifuatavyo.

    1. Kuwahakikishia wananchi mitambo hiyo mitumba inaweza ikafanya kazi kwa muda mrefu bila kuharibika.(Plant worthness)Ikiwapo kumuita independent technical auditor aidhinishe.

    2. Wameshindwa kusema kwa kipindi hicho itakapokuwa inafanya kazi itasaidia vipi kuboresha makali ya LUKU (tariff) ya Tanesco

    3. Watanunua vipi huku kesi ya arbitration inanguruma majuu (france)mwisho, si watalipa ma damage kibao na hatimaye LUKU zitazidi kupanda?

    kwa hiyo ni wazi kabisa wameishiwa busara, dira na mwelekeo na inabidi uongozi na timu yote ungatuke uwarudishe wahandisi umeme wenye uwezo,busara, dira na mwelekeo, hata kama ni wazalendo kutoka nje ya nchi wafanye mambo kama Mosha na mhaville.

    Hili shirika linatia aibu...muda mrefu.. kama vile humo ndani hamna watu wenye kufikiri au wachache wasioweza kufikiri wanawagandamiza wenzao wenye kufikiri.

    Hebu angalia directoreate zake kibao, mameneja kibao, eti generation ina mameneja kadhaa, generation ni moja tu, iwe gas, maji, makaa,...ungo... etc. linganisha na kampuni nyingi za umeme africa ulaya na marekani utaona hii ya kwetu ina mushkeli.

    Mdau wa 6.03 pm aliyesema kuwa inabidi iitishwe tenda na kampuni zaidi ya moja zitende, sio lazima kwenye case zote, case kama hii inathibitika kuwa ina manufaa kwa taifa waziri au raisi anaweza akawaive procedure zote za central tender body, aid agencies wametufanyia brain washing kuwa tenda with shortlisted companies ndio only route for procurement, sio kweli zipo njia nyingi kutokana na situation tofauti.

    mhandisi umeme ughaibuni,

    anayekeretwa kuona makali ya LUKU yanaongezeka bila sababu za msingi.

    ReplyDelete
  21. Kuna kampuni moja inaitwa Kawasaki inamitambo mipya kabisa na ya kisasa na price ni almost half ya ile ya Richmond ipo Houston-Texas.
    Kabla hiyo mitambo mibovu ya Richmond kununuliwa wakubwa walienda pale na kwa sababu hawakukatiwa kidogodo na hapakuwa na longolongo wala cha juu kwa yeyote yule ndipo walipoikimbia hii Kawasaki.
    Sasa kwanini hawa wakubwa wasirudi tena pale kupata mitambo ya uhakika na wananchi wakaondokana na hili tatizo sugu miaka nenda miaka rudi.
    Ni maoni yangu tu.

    Wakumbuke fadhila za nchi iliyowasomesha na kuwapa nafasi hizi wananazozitumia vibaya na kuwanyima haki wananchi waliowachagua.

    Mwenyezi mungu awalaani wote waliosomeshwa na serikali na bado wanaidhulumu serikali na walipa kodi wake.....aaaamin rabil-aalamin

    ReplyDelete
  22. Wandugu pamoja na kujadili yoote tusisahau kwamba huyu mtu 'dk Idris ' ametajwa kwenye sakata la ununuzi wa rada ambayo ilinunuliwa yeye akiwa gavana wa benki kuu sasa huo uchungu wa nchi leo hii anutoa wapi , ninachoamini mimi anatafuta njia ya kuchomoka hapo alipo aishie zake ughaibuni kisha tuje tuambiwe kabalali

    ReplyDelete
  23. Na Muumba wetu na asimame katika hili
    tumechoka sana na aya mambo

    yan its so crazy,everything ni mchezo wa kishenzi

    ReplyDelete
  24. hii nchi inaendeshwa kisiasa sana tanesco walikuwa sahihi isipokuwa kuna wana siasa wanatafuta umaarufu mana wanajua 2010 inakuja,haiwezekani wataalam waliobobea wakashauri halafu mbunge ambaye hana ata alifu ya mambo ya umeme aje kupinga huu ni udhalilishaji wa taaluma za watu,itafikia watu watashindwa kufanya maamuz kwa kuhofia wanasiasa bunge lazima liwe na m,ipaka yake isije ikawa kamati bunge za bunge ndo zinarule huku ni kuikosea heshima serikali,waziri anashindwa kufanya maamuzi akifanya ufisadi sio haki kabisa lazima tutenganishe siasa na wataalam,waachiwe wataalam wafanye mambo yao tuone kama nchi hii haitoendelea,huku ni kurudishana kule tulipotoka,maana inafikia kamat za bunge ndo zina endesha serikali,na kama tuenda hivi hata ashuke issa au m,uhamad hii nchi haindelei na tutyaendelea na ujinga wetu na kutoheshimiana.DK RASHID yupo sahuhi kabisa yeye kama mkurugenzi ana mamllaka ya kuongea lolote linalohusu tanesco na kujitoa ni uamuzi sahihi. mdau kifaa

    ReplyDelete
  25. DR Rashidi is very right, you have to acknowledge the fact that TANESCO was expecting 300 MG from artumas, this company is now closing and trading under Umoja Light company all major financiers have pulled out, Kiwira is also engulfed with politics, you have to also acknowledge the fact that you havent given Tanesco a chance to show you its long and short term plans just buying in from politicians; i nearly fall off my chair when one prominent politician was quoted saying all these faulty tanesco generators if they are revived would produce 1,000MG guys, those generators produce under 1MG , the DEWA ( dubai Electric and Water Supply ) have standby of 1,000MG (as reserves ) and that is one of the most advanced countries in the world how then can you even imagine tanesco has those 1,000MG one anonymous says he knows of cheaper mitambo than dowans, OK do you know you just cant buy mitambo off shelf ?? do you know you have to provide specifications and mitambo be made under those specs?? then it has to be brought in teh country and start test runs ?? those runs could last 6 months shippinng additional 6 hahah how could you bring it one week?? how do you know its cheaper than dowans, ?? please guys leave politiki to politicians and i think you have to swallow the pill and told hard truth yes we can have all rain we want but our combines hydros are beyond the maximum demand ; how can investors invest without knowing if we have relieable electricity??
    now food for thought, anyone who has better ideas channel them thru the right channels and dont just glorify politicians who wants assurance of their seats next year
    traitor?? on this case so BE IT!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...