uongozi wa juu wa ccm chini ya mwenyekiti wake jk wakiwa katika mkutano mkuu wa kamati kuu ya chama hicho huko dodoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. CCM Oyeeee!!
    Wapinzani hawana nguvu ya kuongoza nchi. Wanasema sana lakini hakuna vitendo!! Hawana sera yoyote amabyo inafafanua jinsi gani wanaweza kumnyanyua mtanzania wa kawaida kutoka hali yake ya sasa na kumweka katika hali nzuri kimaisha. Tuongelee mipango siyo tu kuropoka Fisadi huyoooo, fisadi yuleeeeee!! upuuzi mtupu. Anayetaka kujadili tuwasiliane!! Natanguliza shukrani.
    Michuzi oyeeeeeeeee!!
    Mdau!!

    ReplyDelete
  2. KILA LA KHERI HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM.WATANZANIA TUNA IMANI NANYI KATIKA KUFANYA MAAMUZI YA BUSARA KWA CHAMA NA TAIFA ZIMA LA TANZANIA.

    UMEFIKA WAKATI AMBAO WATANZANIA TUNAJITAFAKARI NA KUHAKIKI MICHANGO YETU KWA TAIFA LETU.

    KAZI YENU IENDELEE KUWA NI KUONYESHA DIRA NA NJIA ILI TUFIKIE MALENGO YETU YA KITAIFA.

    MUNGU IBARIKI TANZANIA,MAPINDUZI DAIMA.
    MAINA ANG'IELA OWINO.

    ReplyDelete
  3. Hongera NEC kuwateua Hasina Mwilima DC wa Hai kuwa Katibu Mkuu wa UWT na mheshimiwa Shigela DC wa Lindi kuwa Katibu Mkuu wa UVCCM. Sasa nina hakika hawa ndiyo watakayoipa ushindi CCM mwakani na mwaka huu uchaguzi wa serikali za mitaa. Ombi langu kwao wawe mstari wa mbele kupambana na propaganda mufilisi za CHADEMA na CUF. Muwahamasishe akina mama na vijana kupigana vita vya CCM. Ushindi ni wetu kwa uhakika.

    ReplyDelete
  4. Top brass ya chama nyepesii,...Nani wa kukemea mtu akasikilizwa hapo?... Wako so thin on character and leadership record. No wonder CCM linameguka 2010 kwa kukumbatia mafisadi kama mama zao.

    ReplyDelete
  5. Hilo Bango linalosomeka hapo ndani ya Mkutano kwamba,"Bila ya CCM madhubuti nchi yetu itayumba!",siyo kauli ya kuidekeza sana ndugu zangu watanzania.Nchi hii inazidi kukua kiakili na kimalengo.Hivi sasa tumedhamiria kuimarisha Demokrasia hapa nchini ya Vyama Vingi vya Siasa kwa nia njema kabisa ya kuharakisha maendeleo nchini na kukabiliana na matumizi mabaya ya madaraka na ufisadi uliozidi kuota mizizi.Ili hilo liwezekane,lazima kila Mtanzania atambue kwamba hatuwezi kuendelea kuishi na kuiongoza nchi yetu kwa fikra zilizo ganda kwamba "bila ya fulani"nchi yetu haiwezi kusonga mbele;"bila ya chama fulani cha siasa"nchi yetu itayumba;"bila ya kikundi fulani cha watu wachache waanzilishi"wa chama chochote kile basi chama hicho hakiwezi kusonga mbele au nchi itayumba!Hakuna Kitu kama hicho ndugu zangu watanzania!Lazima tupambane na mawazo duni na fikra finyu kama hizo zenye lengo la kuzidisha unyonge wa kufikiri na kuthubutu katika kupambana na viongozi ambao wamebakia "majina tu"lakini uwezo wa kufikiri na kuongoza wamechoka ile mbaya.Lazima katika mikutano kama hiyo yawekwe Mabango yatakayo kwenda na wakati na yenye kuhamasisha fikra za maendeleo zaidi na sio kinyume chake!Tuache Siasa za Unafiki!Tuwe Wazalendo kwelikweli,tukiweka mbele maslahi ya Taifa na Vizazi vijavyo!Lakini siyo kumtukuza "mtu fulani"hata pasipo stahili kwa faida na maslahi ya watu wachache!mimi ni ccm damdam!

    ReplyDelete
  6. Naungana na mdau hapo juu,hilo bango hapo juu kama Nyerere angekuwa hai leo hii,angelifuta kwa wino mwekundu!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...