Kaka Michuzi,
 
Yah: Nyimbo za watoto za kiswahili

Kwanza napenda kukushukuru na kukupongeza kwa kazi yako nzuri ya kutelea habari mbalimbali za huko nyumbani hasa kwa sisi tulio nje ya nchi. Mimi nina ombi moja kwa wasomaji wako. 

Ninahitaji kwa yeyote anayejua au kukumbuka nyimbo za kiswahili za wototo, pamoja na hadithi fupi anitumie kwenye email yangu tafadhali. Ninahitaji sana kwa ajili ya project ninayoifanya na pia kumfundisha mwanangu. Natanguliza shukrani zangu.
Email yangu ni 
limso2001@yahoo.com.
 
Asante,
Lina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Kwa hadithi, nenda pale kwa dada Subi (nuta77.com) utapata za kutosha kama vile mbaramwezi nyota begani n.k.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  2. asiyependa shule ni mjinga kabisa
    eemwalimu X2 nifundisheX2

    ReplyDelete
  3. asiyependa shule ni mjinga kabisa
    eemwalimu X2 nifundisheX2

    ReplyDelete
  4. watoto wangu ee ee mimi mama yenu ee
    sinananguvu tena za kumuuwa simba simba ni mkali aliuwa baba akauwa mama sasa wahiwahi

    ninanyimbo nyingi sema mtoto wangu anasumbua kidogo akilala nitakutumie usikonde

    ReplyDelete
  5. hesabu ningumu sana wee, nimesahau endelea na wewe

    ReplyDelete
  6. andika kwenye google hadithi itakuja web ina hadith za bint chura na nyengine nyingi tu

    ReplyDelete
  7. Sasa!
    Sasa!
    Saa ya kwenda kwetu
    Kwa heri mwalimu kwa heeri
    Tutaonana KESHO!!!

    ReplyDelete
  8. ULINGE BAIYOYO X4.
    TUNAMUOMBA DADA ASHA TUYAONE MALINGO YAKE BIGILIBIGILI MPAKA CHINI.

    IT IS WHAT IT IS.

    ReplyDelete
  9. KIBANGA AMPIGA MKOLONI...

    SONGI: GEZA ULOLE...MALIZIA KIBWAGIZO

    IT IS WHAT IT IS.

    ReplyDelete
  10. Ingia kwenye site hii utaweza kusikiliza hadithi nzuri za nyumbani kwa ajili yako na watoto.

    http://hadithihadithi.podomatic.com/


    Mama Ben

    ReplyDelete
  11. Mwimbo

    Chei chie shangazi *2
    shangazi shangazi ei shangazi

    etc nakumbuka hayo tu

    Kihaya

    Chwi chwi chwii, omwana nalila
    nalizibwaki?
    nalizibwa nyina

    nyina agile nkaa agile kulima
    kulima ebiki?
    kulima bwinyobwa

    chwi chwi chwii, omwana nalila
    nalizibwakii?
    nalizibwa mama

    mama agile mkaa? agile kuchumba
    kuchumba ebikii?
    kuchumba matoke.

    etc

    (unalaza mtoto huu mwimbo, ni mzuri sana hata watoto wangu waliokulia huku ulaya wanaupenda sana ukianza tu kuimba wanalegea na kutulia kusikiliza)

    good luck

    sasa ukiandikiwa tune ya nyimbo utazijuaje?

    ReplyDelete
  12. mabata madogo mdogo yanaogelea yanaogelea katika bwawa zuri la bustani..........teh teh teh sijui nimepatia wadau endelezeni maana nimesahau.

    Mama T wa A city

    ReplyDelete
  13. zum zum zum ee mama nyuki lia wee*2
    toka mbali kutafuta ua zuri la chakula
    zum zum ee mama nyuki lia wee

    ReplyDelete
  14. maua mazuri yapendeza*2
    ukiyatizama utafurahia
    hakuna mmoja asiyependeza

    ReplyDelete
  15. yai bovu yai bovu
    linanuka linanuka
    linanukaje linanukaje
    bwii bwii sambwela
    nina ndoo yangu
    eeh
    ya kuchota maji
    eeh
    watoto msistizame nyuma
    yai bovu linapita
    watoto msiangalie
    yai bovu linapita

    ReplyDelete
  16. ukuti ukuti
    wa mnazi mnazi
    ingia upepo
    wa msesema
    ingia upepo
    wa msemo

    ReplyDelete
  17. bibi
    kanyabwela
    tumbo
    lamsokota
    ka' tumbaku

    ReplyDelete
  18. bai sho i lavu yu bebi
    ze bebi tu ze sa aaah
    zesa tu ze yona
    ze yona tu ze mii
    ze mi tu ze pull zea
    sela wan tu silii fo
    sela wan tu silii fo
    tantakoma
    sela wan tu
    sela wan tu
    tantakoma
    sela wan sela wan baishooooooooo

    (hapo usiniulize maana, maana hata mimi sijui maana yake. ila hiyo unakuwa unacheza kwa mikono kama vile amina kadala, si unaikumbuka)

    amina
    amina kadala
    si no ea amina dulishot kalinge
    e noe enoe
    tumpepeee
    tumpepeee
    amina modelesta modelesta
    amina dush dush kama daa (weka alama ya dole gumba kwa mikono yote halafu unakuwa unairudisha kwa nyuma pale unaposema dush dush kama daaaa)
    kama dada wanipenda
    kaninunulie zeze
    nikilala kitandani
    zeze lanibembeleza
    aaah amina
    kuchovya chovya ni vibaya
    utakuja kumchovya mkweo
    aliyekuzalia mumeo
    ...huku kwingine nimesahau. long taimu kitambo, jamani, nimesahau...ila nimejitahidi

    ReplyDelete
  19. Simama kaaaa,, simama kaaaa, luka luka luka, simama kaaa, tembea tembea tembea.. luka luka simama kaaa

    ReplyDelete
  20. Pole sana mdau nakumbuka nilipokuwa secondary mwalimu alitupa project ya kiswahili kuandika beti 300 za nyimbo za kubembeleza mtoto na alizitaka baada ya mwezi mmoja tu, baadae tulikuja gundua alikuwa anataka yeye tungo hizo azitumie, ah! ila haikuwa noma sisi tulijikombea vijimaksi vyetu tukasonga mbele. Ukweli sitakisahau kipindi kile ilibidi twende mpaka kwenye maeneo ya wanakotunzwa kina bibi wakongwe Uwelezo) ili walau tupate beti tofauti tofauti, kwa leo nitakupa chache ninazozipenda sana na huwa nawachombezea wanangu wadogo na wakubwa husikiliza kwa makini na kurudia, huku nikijua nawapa ujumbe na juifunza:-

    Owani mwana owani kitunguu na ubani
    Nyoka kalala tumkanyage kichwani
    tuwapishe wenda kuni na wendao kisimani
    :/: Ooo mtotoo ooo mtotoo

    Ukimpenda mwanao na wa mwenzio mpendee
    wako ukimpa chengaa wamwenzio chenjegelee
    :/: Ooo mtotoo ooo mtotoo.

    Kilengelenge cha boga kutia nazi kunoga
    Mkono wataka kulaa maungo yaona wogaa
    :/: Ooo mtotoo ooo mtotoo

    Mama aliponiza kanizaa mbiombio kanambia toka nje ukacheze na wenzioo
    :/: Ooo mtotoo ooo mtotoo

    Sikumwita sikumwita wala sikumtafuta
    Mungu akitakakupa hakuna wa kulifutaa
    :/: Ooo mtotoo ooo mtotoo

    ReplyDelete
  21. Eeeh vijanaa..vijaaanaa vijana vijana tumikia..tumikia taifaa taifaa taifaa.Tumikia..Taifa Taifa TANZANIAAAAAAA

    ReplyDelete
  22. ana ana anadooo kachanika pastoo aspiringi mapingo kaj*mbaaaa, ushuzi unanuka, tena sana, sana kabisa, matikiti kudondoka, kudongokea, matikiti kudondoka, kudondokea!

    ReplyDelete
  23. Mko wapi jamani tupe vitu watoto wetu wanataka nyimbo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...