Kaka Michuzi,
Yah: Nyimbo za watoto za kiswahili
Kwanza napenda kukushukuru na kukupongeza kwa kazi yako nzuri ya kutelea habari mbalimbali za huko nyumbani hasa kwa sisi tulio nje ya nchi. Mimi nina ombi moja kwa wasomaji wako.
Ninahitaji kwa yeyote anayejua au kukumbuka nyimbo za kiswahili za wototo, pamoja na hadithi fupi anitumie kwenye email yangu tafadhali. Ninahitaji sana kwa ajili ya project ninayoifanya na pia kumfundisha mwanangu. Natanguliza shukrani zangu.
Email yangu ni
limso2001@yahoo.com.
Asante,
Lina.
Kwa hadithi, nenda pale kwa dada Subi (nuta77.com) utapata za kutosha kama vile mbaramwezi nyota begani n.k.
ReplyDeleteMdau
Cardiff
asiyependa shule ni mjinga kabisa
ReplyDeleteeemwalimu X2 nifundisheX2
asiyependa shule ni mjinga kabisa
ReplyDeleteeemwalimu X2 nifundisheX2
watoto wangu ee ee mimi mama yenu ee
ReplyDeletesinananguvu tena za kumuuwa simba simba ni mkali aliuwa baba akauwa mama sasa wahiwahi
ninanyimbo nyingi sema mtoto wangu anasumbua kidogo akilala nitakutumie usikonde
hesabu ningumu sana wee, nimesahau endelea na wewe
ReplyDeleteandika kwenye google hadithi itakuja web ina hadith za bint chura na nyengine nyingi tu
ReplyDeleteSasa!
ReplyDeleteSasa!
Saa ya kwenda kwetu
Kwa heri mwalimu kwa heeri
Tutaonana KESHO!!!
ULINGE BAIYOYO X4.
ReplyDeleteTUNAMUOMBA DADA ASHA TUYAONE MALINGO YAKE BIGILIBIGILI MPAKA CHINI.
IT IS WHAT IT IS.
KIBANGA AMPIGA MKOLONI...
ReplyDeleteSONGI: GEZA ULOLE...MALIZIA KIBWAGIZO
IT IS WHAT IT IS.
Ingia kwenye site hii utaweza kusikiliza hadithi nzuri za nyumbani kwa ajili yako na watoto.
ReplyDeletehttp://hadithihadithi.podomatic.com/
Mama Ben
Mwimbo
ReplyDeleteChei chie shangazi *2
shangazi shangazi ei shangazi
etc nakumbuka hayo tu
Kihaya
Chwi chwi chwii, omwana nalila
nalizibwaki?
nalizibwa nyina
nyina agile nkaa agile kulima
kulima ebiki?
kulima bwinyobwa
chwi chwi chwii, omwana nalila
nalizibwakii?
nalizibwa mama
mama agile mkaa? agile kuchumba
kuchumba ebikii?
kuchumba matoke.
etc
(unalaza mtoto huu mwimbo, ni mzuri sana hata watoto wangu waliokulia huku ulaya wanaupenda sana ukianza tu kuimba wanalegea na kutulia kusikiliza)
good luck
sasa ukiandikiwa tune ya nyimbo utazijuaje?
mabata madogo mdogo yanaogelea yanaogelea katika bwawa zuri la bustani..........teh teh teh sijui nimepatia wadau endelezeni maana nimesahau.
ReplyDeleteMama T wa A city
zum zum zum ee mama nyuki lia wee*2
ReplyDeletetoka mbali kutafuta ua zuri la chakula
zum zum ee mama nyuki lia wee
maua mazuri yapendeza*2
ReplyDeleteukiyatizama utafurahia
hakuna mmoja asiyependeza
yai bovu yai bovu
ReplyDeletelinanuka linanuka
linanukaje linanukaje
bwii bwii sambwela
nina ndoo yangu
eeh
ya kuchota maji
eeh
watoto msistizame nyuma
yai bovu linapita
watoto msiangalie
yai bovu linapita
ukuti ukuti
ReplyDeletewa mnazi mnazi
ingia upepo
wa msesema
ingia upepo
wa msemo
bibi
ReplyDeletekanyabwela
tumbo
lamsokota
ka' tumbaku
bai sho i lavu yu bebi
ReplyDeleteze bebi tu ze sa aaah
zesa tu ze yona
ze yona tu ze mii
ze mi tu ze pull zea
sela wan tu silii fo
sela wan tu silii fo
tantakoma
sela wan tu
sela wan tu
tantakoma
sela wan sela wan baishooooooooo
(hapo usiniulize maana, maana hata mimi sijui maana yake. ila hiyo unakuwa unacheza kwa mikono kama vile amina kadala, si unaikumbuka)
amina
amina kadala
si no ea amina dulishot kalinge
e noe enoe
tumpepeee
tumpepeee
amina modelesta modelesta
amina dush dush kama daa (weka alama ya dole gumba kwa mikono yote halafu unakuwa unairudisha kwa nyuma pale unaposema dush dush kama daaaa)
kama dada wanipenda
kaninunulie zeze
nikilala kitandani
zeze lanibembeleza
aaah amina
kuchovya chovya ni vibaya
utakuja kumchovya mkweo
aliyekuzalia mumeo
...huku kwingine nimesahau. long taimu kitambo, jamani, nimesahau...ila nimejitahidi
Simama kaaaa,, simama kaaaa, luka luka luka, simama kaaa, tembea tembea tembea.. luka luka simama kaaa
ReplyDeletePole sana mdau nakumbuka nilipokuwa secondary mwalimu alitupa project ya kiswahili kuandika beti 300 za nyimbo za kubembeleza mtoto na alizitaka baada ya mwezi mmoja tu, baadae tulikuja gundua alikuwa anataka yeye tungo hizo azitumie, ah! ila haikuwa noma sisi tulijikombea vijimaksi vyetu tukasonga mbele. Ukweli sitakisahau kipindi kile ilibidi twende mpaka kwenye maeneo ya wanakotunzwa kina bibi wakongwe Uwelezo) ili walau tupate beti tofauti tofauti, kwa leo nitakupa chache ninazozipenda sana na huwa nawachombezea wanangu wadogo na wakubwa husikiliza kwa makini na kurudia, huku nikijua nawapa ujumbe na juifunza:-
ReplyDeleteOwani mwana owani kitunguu na ubani
Nyoka kalala tumkanyage kichwani
tuwapishe wenda kuni na wendao kisimani
:/: Ooo mtotoo ooo mtotoo
Ukimpenda mwanao na wa mwenzio mpendee
wako ukimpa chengaa wamwenzio chenjegelee
:/: Ooo mtotoo ooo mtotoo.
Kilengelenge cha boga kutia nazi kunoga
Mkono wataka kulaa maungo yaona wogaa
:/: Ooo mtotoo ooo mtotoo
Mama aliponiza kanizaa mbiombio kanambia toka nje ukacheze na wenzioo
:/: Ooo mtotoo ooo mtotoo
Sikumwita sikumwita wala sikumtafuta
Mungu akitakakupa hakuna wa kulifutaa
:/: Ooo mtotoo ooo mtotoo
Eeeh vijanaa..vijaaanaa vijana vijana tumikia..tumikia taifaa taifaa taifaa.Tumikia..Taifa Taifa TANZANIAAAAAAA
ReplyDeleteana ana anadooo kachanika pastoo aspiringi mapingo kaj*mbaaaa, ushuzi unanuka, tena sana, sana kabisa, matikiti kudondoka, kudongokea, matikiti kudondoka, kudondokea!
ReplyDeleteMko wapi jamani tupe vitu watoto wetu wanataka nyimbo
ReplyDelete