redio ya watu, clouds 88.4fm, imeshakamilisha jengo lake na hivi sasa harakati za kuhamia humo kutoka jengo la kitega uchumi la bima mtaa wa samora avenue zimeshamiri. globu ya jamii inatoa hongera kwa hatua hiyo muhimu iliyofikiwa na redio hii binafsi yenye umri wa muongo mmoja sasa na inaendelea kudunda kwa kwenda mbele. jengo hili jipya la clouds 88.4fm liko sehemu za mikocheni barabara ya old bagamoyo road, jirani na njia ya kuelekea coca cola
Home
Unlabelled
redio ya watu yahamia jengo lake jipya mikocheni
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Safi sana, hii imekaa vizuri nathani na ITV nao itabidi waige mfano wajenge ofisi yenye hadhi kama Clouds maana si siri zile ofisi pale zilikuwa godowns kama sikosei!
ReplyDeleteGood job in reducing the traffic to Dar city center...
ReplyDeletena nyie mashabiki wa bwawa la maini si mhamie Man U tu.
ReplyDeleteEh bwana eh hilo ghorofa kajenga Ruge au amepanga????
ReplyDeleteSafi sana, pongezi nyingi kwa wadau kufanya mambo makubwa kama haya. Inafurahisha kwakweli juhudi hizi, na zaidi hiyo akili ya kutoka mjini na kuhamia maeneo mengine...labda wadau wengine wakifuata nyendo hizi, zile foleni za magari asubuhi zitapungua - maana maofisi yatakuwa sehemu mbalimbali na sio katikati ya jiji pekee.
ReplyDeletePoa sana
ReplyDeletehongera wazee wa nyuki mmeonyesha njia......"eti mkuu wamehamia barabara gani?"
ReplyDeleteHongereni sana kwa kuwa na jengo lenu, mtakuwa mnaishi hapo hapo kwani nafikiri redio tu kwa jengo hilo ni kubwa au nanyie mtawapangisha watu wengine? majibu tafadhali kwani niwahi ofisi hapohapo.
ReplyDeletehongereni sana Clouds Media Group.
ReplyDeletehabari yako issa michuzi. wape hongera na salaam nyingi. kule simu yao ya land line ni ipi?
ReplyDeleteHili jengo kutokuwepo City Center imekuwa vizuri sana...tunaweza kusema magari japo 10 jatapungua kuja mjini kwa siku..
ReplyDeletePamoja na hongera zao, waambie wanede online sasa watu wanataka kuisikia clouds huko majuu
ReplyDeleteHongera pia kwa Joseph, hope he is still managing the firm/group.-fomer classmate 81-83, ughaibuni.
ReplyDeleteBig up Joseph Kusaga and the whole team! Ila pliz boresheni usikivu wa radio yenu kwani sisi tunaishi bunju hatuipati kabisaa clouds. Mpaka ufike maeneo ya tegeta nyaishozi ndio unaanza kuipata kwa kwikwi. Ni hilo tu, otherwise maendeleo yenu yanatia moyo
ReplyDeleteNASIKIA FINA NA KIPANYA KURUDI CLOUDS ITAKUWA BOMBA SANA, TUNAWAMISS WATU WETU, TUNAUOMBA UONGOZI WA CLOUDS UWASAMEHE NA KUWARUDISHA NADHANI KWA SASA WATAKUWA NA NIDHAMU,KWANI WALIKUWA WANACHANGAMSHA RADIO YETU, NO ONE IS PERFECT..
ReplyDeleteMDAU WA CLOUDS
HO CHI MIHN CITY
CAMBODIA.
hongereni kwa jengo jipya..............ila naona bado mko karne ya 19 ....mnatakiwa kuwa online
ReplyDelete