Mbunge wa Singida mjini Mh. Mohamed Dewji 'Mo' akijichanganya na wanafunzi
Mo na baadhi ya wanafunzi wa Singida
Mhe Mohammed Dewji akisalimiana na wanafunzi wa shule Singida Mjini.

KakaMichuzi,
tunashukuru kwa kutupa habari moto moto na mabreaking nyuzzzz muda wote. Leo ninataka niongelee sekta ya elimu, sekta nyingi muhimu za Tanzania zipo nyuma sana kimaendeleo, lakini binafsi ningeshauri viongozi wazidi kuwekeza katika sekta muhimu ya Elimu. Iwapo tukiwekeza kwenye elimu basi tutaweza kuwa na vijana wengi wasomi ambao watalisaidia taifa letu hapo baadae.

Hivi karibuni nilitembelea mkoa wa Singida, na nilifurahi kuona jinsi shule mpya za sekondari zilivyojengwa na nikapata kuwadadisi wakazi wa Singida mjini kuhusu majengo hayo mapya, wakanijibu kwa kuniambia kuwa wanawekeza kwa ajili ya watoto wao ili waweze kuwasaidia na kuinua maendeleo mkoani hapo na Taifa kwa ujumla.
Wakisaidiana na mbunge wa Singida mjini Mhe. Mohammed Dewji, tayari wameweza kujenga shule mpya za sekondari kumi na mbili na kufanya jumla ya idadi kuwa kumi na nne mjini Singida ndani ya miaka minne iliyopita kutoka sekondari mbili zilizokuwepo tokea kupatikana kwa uhuru ( Ongezeko la asilimia mia saba kwa idadi za shule za sekondari).

Wakishirikiana na Mhe. Dewji wameweza kuimarisha sekta hiyo ya elimu huku mbunge wao akichangia kujenga madarasa na shule hizo mpya na wananchi wakimpa ushirikiano katika ujenzi wa shule hizo pia.

Naamini iwapo tukiimarisha sekta ya elimu kama Singida, itakuwa mwanzo mzuri wa kupata wataalamu bora miaka ijayo kwa manufaa ya taifa letu, ingawa ujenzi wa shule sio ufumbuzi pekee, inabidi tuangalie suala la upatikanaji wa walimu na vitendea kazi katika sekta hiyo. Ujumbe wangu ni kuwa sekta ya elimu ikiboreshwa itakuwa ndio chachu ya maendeleo kwa taifa letu.
Mdau wa Singida

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mzee Misupu waonyeshe pia website ya Bw Mdogo Mheshimiwa Deawji
    http://mohammedewji.com/

    ReplyDelete
  2. Mohamed Dewji ni mtu makini , ndio maana watu wa Singida wanamkubali kwa sababu he hasn't forgotten where he came from ! In fact, he knows the importance of giving back to the community. It is my hope that other people, especially politicians, are going to emulate what Dewji has done to his constituent

    ReplyDelete
  3. Kama kweli vilee...!

    ReplyDelete
  4. Kwanza niseme hivi, hakuna best investment Tanzania inaweza kufanya kama kuwekeza kwenye elimu. Tanzania ya leo more than 40% ya wananchi wake wako chini ya miaka 19. Lakini swala muhimu sio majengo, swala muhimu ni kusastain that kind of growth. In economics we call it sustainable development.

    Jee tunajenga shule tukiwa na supply ya walimu walo qualify? Jee watoto wanapata elimu ambayo inalingana na 21st century? Jee watato wanaweza kuwa washindani katika soko la ushindani?

    Jee tunatumia mchakato gani katika swala zima la kufundisha? Jee tunatumia methods mpya au za zamani?

    Haya ni maswali ambayo lazima tumuulize mbunge yeyeto yule. Kwani hupimi maendeleo ya eneo kwa kuangalia majengo ya shule, bali unatazama mfumo mzima.

    Mchumi wa Texas, Safarini Kurudi HOME

    ReplyDelete
  5. mithupu kuwa mkweli hivi unategemea huyu dogo 2010 watambwaga? bwa mdogo mjanja analipa fadhila anatambua wazi toa upewe

    ReplyDelete
  6. Hawa ndo watu wanajua kula na vipofu. Sio mtu unakula na kipofu mpaka unamgusa mkono anashtuka kwamba kuna mtu!

    ReplyDelete
  7. Sasa hapo anaongea nao lugha gani? Si huwa hajuagi kiswahili? Bungeni anaongeaga?
    Maana kuna kipindi wakati hajawa mbunge but alikuwa mtu wa michezo, alishindwa kujibu swali kwa kiswahili, akalijibu kwa kiingereza wakati waandishi walikuwa wale wa michezo, most of them kiingereza hakipandi, ilikuwa patashika, ikabidi aombe msamaha maana lugha ya kiswahili iligoma kupanda kabisaaaaaa, yaani maneno yalikuwa hayatoki mpaka akaamua kuongea kimombo

    ReplyDelete
  8. jamani msipende kusema uongo nidhambi kubwa Dewji mo hajui kiswahili!!!!! mbona mara kibao kasafiri na staz na akirudi anaongea na hata amekuwa mara nyingi akiongele kuhusu klab yake african lyon anaongea kiswahili cha kawaida kabisa acheni ubaguzi wa rangi hao ni wa tz wenzetu

    ReplyDelete
  9. MO knows to express his feelings,in difficult time he got real sad we us and in good time happy with us:) kuna wakati niliona amevua shati na kusakata rumba na Taifa Stars ilipo shinda Burkinafaso! NOt suprised to see him enjoy the moment with kids after school buildings are done:)

    ReplyDelete
  10. Nimeingia ktk webupeji ya Mh. Mbunge Http://mohammedewji.com

    Kwa kweli nimeelewa na kufurahishwa na shughuli zako za kibunge, kibiashara na kijamii.

    Ngoja ni nukuu paragafu moja toka http://mohammeddewji.com: ''Katika kipindi hicho cha masomo katika chuo cha GeorgeTown ndipo Mo alipoanza kubadilika kimaisha na kubadili mtazamo mzima wa kuangalia mambo ambayo binadamu anayafanya kila siku. Chuo hicho kinasifika kuwa na elimu bora na kimetoa viongozi na watu ambao wamefanikiwa sana katika maisha mfano Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, Mfalme Abdullah wa Jordan, Rais Gloria Arroyo wa ufilipino na hata wachezaji wa mpira wa kikapu maarufu nchini Marekani kama Allen Iverson na Patrick Ewing''.

    Hapa naona kiongozi mwenye visheni ya kuiendeleza nchi yake iwe kwa 'kuwawezesha ki-elimu, kiajira, uboreshaji wa uzalishaji mazao mashambani na viwandani n.k ' macho yake akitamani Tanzania ipige hatua kama Philipines, Jordan na hata ikiwezekana Tanzania iwe kama USA.

    Kiongozi mwenye 'ndoto' hizi anatia matumaini kuwa tunaweza kuibadili Tanzania kiuchumi.

    Mdau
    Rocky.

    ReplyDelete
  11. Mimi ki ukweli simjui huyu jamaa(sijui hela yake ni kivipi vipi ,na mambo ka hayo-fisadi,mwizi mwizi au la - mie sijui),lakini kitu kimoja kuhusu huyu bwana anafanya vitu vyake viingi hapa hapa nyumbani tanzania na hata hao waibiwao kiasi wanajisikia faraja,na ndio maana hata wenzetu wa majuu wanaendelea, maana asikuambie mtu hawa wazungu ni wezi kupindukia ila wanafanya ki anaina na kama ni kuwekeza huwezi muona mwizi akipata tu kurupu huyo katoka uingereza kaenda wekeza ufaransa au kwingineko ,anaanzia kule kule kwao alikoiba ,hivyo he is giving back hicho alichoiba kwa kuajiri watu.
    Na jamaa nae anafanya hivyo,hongera dogo!!

    ReplyDelete
  12. Jamaa hatujasikia akihusishwa na tuhuma za ufisadi wala malumbano ya kung'ang'ania ubunge. Tukisikia habari zake ni kama hivi anasaidia kuinua elimu jimboni kwake, amedhamini timu ya soka inayoendeshwa kisasa nk. Ndivyo inavyotakiwa. Watanzania tutaweza kuendelea tukiimarisha elimu.
    Endeleza juhudi zako Dewji.

    ReplyDelete
  13. atendaye mema abarikiwe na apewe sifa anazostahili. japo pia kama mtu aliye elimika anafahamu nini anafanya! ukitaka ku-win moyo wa mzazi,basi onyesha kupenda na kujali mwanawe! hii ni saikolojia inatumika. hongera kijana.MO chahee!!!!

    ReplyDelete
  14. kameni tu hizo mbona hakufanya mwaka mwaka juzi aafanya leo.kweli 2010 ngumu!

    ReplyDelete
  15. Mchumi wa Texas,

    Kiasi fulani napingana na kile ulichosema, huwezi kufikiria suala la mtaala au Quality ya elimu wakati hauna majengo. Kama ukishajenga majengo hivyo vitu vingine vitakuwa rahisi kuvifanya. Mimi nadhani huyu mbunge is heading in the right direction. First thing first, you have to build schools and then worry about the other stuffs that you have mentioned. I read on his website that so far he has spent a fortune, 1.5 billion shillings, for development projects in his constituency.

    Instead of critiquing and ridiculing him, this should be commended for what he has accomplished. I wish Tanzanian had many legislators like him, who understand that government is not always the solution to our problems. Lastly, let me salute him by saying , MO you not only rock but also you are the MAN.

    ReplyDelete
  16. sasa nadhani kwa upande mmoja au mwingine naona haki hakuan katika kutoa maoni katika mjadala husika nini ? maana ya maoni haiwezekani michuzi ukaanika upande mmoja tu ambao unamsifu muhusika upende mwingine usiweke !!

    kaka kila mtu anamtazamo wake na uchungu kwa nchi yake kama viongozi watakuwa hawakosolewi hakuna haja ya kuweka ukurasa wa jamii ......

    roho inaniuma na nina uchungu wa nchi yangu kama mtazania na mpenda maendeleo ..

    bahati mbaya nilisoma kipindi cha Ruksa raisi mstaafu wa awamu ya pili..
    1. tulikuwa tukisoma kwa kuchangia UPE na EK sidhani kama unakumbuka hayo kuanzia darasa la kwanza hadi la saba bahati mbaya hatukuona zile pesa tunazochanga zinafanya nn wala kuambiawa hadi namaliza elimu ya msingi..

    2.Nilikuwa nachangia mafuta ya mwenge kila kipindi unapopita mwenge sasa sijui kwa tanzania wanachangia watu wangapi na shilingi ngapi ?

    3.nilichangia school bus kwa shilingi mia 500 za kitania mbaya na ambayo siwezi kuisahau kaka nilisukumwa mlangoni mwa magari ambayo tulichangia yaliyokuwa yanaitwa school wakidai kwamba tusubiri wakubwa wapande ilikuwa mwaka 1993 hiyo kaka !

    4. kubwa kuliko zote wakati niko katika maanadalizi ya kuja ng'ambo nilichangia kama 20,000/= kwa ajili ya ujenzi wa sekondari sijui kama zimejengwa maana hiyo ni lazima utoe katika serikali za mitaa bila hivyo hakuna msaada..

    SWALI : je pesa hizo zote zinakwenda wapi kaka ? au ndio za kampeni ? 2. hao viongozi wanaotoa misaada wanajihusisha na shughuli gani za kiuchumi au wanafata sheria za biashara nchini pamoja na ulipaji wa kodi ? Samahani sana kaka kaka nimekosea roho inaniuma kuona nauli shilingi 500 na hakuna usafiri jamii ya serikari au public transport

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...