Viongozi wa kuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Toka shoto ni Marais Yoweri Museveni wa Uganda, Mwai Kibaki wa Kenya, Paul Kagame wa Rwanda, Jakaya Kikwete wa Tanzania na Pierre Nkurunzinza wa Burundi.
Ijumaa ilopita Jumuiya ya Afrika Mashariki ilitimiza miaka 10 ya uhai wake na viongozi wakuu watano wote walikuwa jijini Arusha katika hitimisho la sherehe hizo zilizoambatana na utiwaji saini makubaliano ya kuwa na soko la pamoja na pia kuwekwa kwa jiwe la msingi la makao makuu ya jumuiya hiyo yanayojengwa jijini humo.
Wadau si vibaya tukajadili umuhimu wa tukio hilo la kihistoria la kuwa na soko la pamoja kwa nchi hizo tano utaoanza kutumika rasmi Januari 1, 2010, hatua ambayo itafuatia kuwa na sarafu ya pamoja na, endapo pande zote zitakubaliana, hatimaye shirikisho la Afrika Mashariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Wizi mtupu. Nabii Yohanna Mashaka mwaga razi hapa kabla US Blobber hajafika kuchafua Hali ya hela. Hakuna cha soko wala nini vinakuja kuvuluga Amani yetu tu

    ReplyDelete
  2. Wanameremeta. Wakiamua tusiwepo hatupo basi na tuombe watuamulie mema ili tunufaike sisi na vizazi vyetu na vyao pia.

    ReplyDelete
  3. Ukifika ulaya utapenda regional cooperation. Yaani unatua Amsterdam na mzungu, tuseme anatoka Germany, anapita kilaiini, bila kugongewa passport, wewe unakaguliwa, ilizwa mialiko, una pesa ngapi, etc. Mzungu kutoka EU akiingia Holland anaruhusiwa kufanya kazi, kuishi, kutanua mpaka mwisho na sisi Africa Mashariki tumeweza. Alafu sisi ni ndugu, watanzania wenye akili finyu, kwa mfano wanawachulia Rwanda na Burundi kama outsiders. Kwa taarifa yenu: Kigoma na Burundi ni nchi moja, lugha moja na utamaduni mmoja! Bihalahulo, Ngara na Rwanda is copy and paste. Kwahiyo Kilontsi Mpologomyi na Pieere Nkurunziza wanaweza kuongea na kucheka utani bila tatizo. Pia lugha hizi ni saw na Kifumbila cha Uganda!.
    Tuje wajaluo: Tarime, Kisumu na wacholi wa Uganda ni copy and paste.
    wahaya, Wanyambo, Wakiga, Wanyankore, watoro, wanyoro na Wanyambo wa Rwanda ni copy and paste.
    Hapa ni ushindani na kuchapa kazi, Mo Ibrahim kasema baadhi ya nchi hazifai kuwa nchi, kwni haziwezi kujitosheleza.
    Kuna watu kama Matinyi na Mashaka, etc. wanaogopa. Maskini, hawajui Kimombo! watanzania tutaendelea kunungunika, kuwa mediocre kama hatutapata changamoto kutoka nje. Tutaendelea kuzalisha bidhaa feki kama hakuna ushindani! newton's law of motion inasema: An object will maintain a constant motion unless there is an external force acting up on it. watanzania tutabaki na poor English, poor products kama Sweetheart lotion, poor work ethics until we join the EAC.
    Long live our unity, bring on Kenyans! competent Tanzanians will prevail, while mediocres will be suffocated.

    ReplyDelete
  4. Mahojiano ya mtangazaji wa BBC na mkulu mmoja wa Kenya katika kipindi cha wiki hii jumamosi.

    Mkenya: Uingizaji bidhaa nchini Kenya kutoka Tanzania na Uganda imekua kwa asilimia kubwa (140%Tz, ...%) Uganda

    Mtangazaji: Watanzania wanauza nini?

    Mkenya: Wanuza Mahindi, Nyanya, ...eee...., zaidi zaidi vyakula.

    Matngazaji: Na Waganda wanauza nini?

    Mkenya: ..eeee...Na wao wanauza hizohizo..., vyakula.

    Matngazaji: Na wakenya wanauza nini Tanzania na Uganda?

    Mkenya: manufacured goods.

    Hivi soko letu la Mahindi si kubwa zaidi malawi? Kwa nini tunahitaji shirikisho kuuza mahindi na nyanya??

    ReplyDelete
  5. Tatizo languu mimi ninashindwa kuelewa je EAC ilivunjika kutokana na migogoro ya hapo mwanzo je waliweza kupata solution ya hiyooo migogoro maana kama sikosei kipindi kile Kenya waliweza kuchukua sector ya airline,na sisi kuachiwa railways na bandari!nampaka sasahivi wazee badooo hawajapewa fedha zao baadaa ya kufa sasa hiii ya sasahivi sijui tutagawana nini jamani maaana zilikuwa nchi tatu ikawa migogoro na hapo wakiruhusu land basiii Tanzania tumekuwa masikini

    ReplyDelete
  6. Hizi ni habari nzuri sana shirikisho na lije Wabongo tusiogope kitu......hawa wengine kwani wana nini mpaka tuwaogope??Lazima tuwe kama EU unateremka unakotaka ....na rushwa ya kibongobongo itaisha pia tukiwa shirikisho kwani itakuwa ni ushindani tu ukilegea umekwenda.Survival for the fittest,Welcome shirikisho.
    Big up marais wa East Africa.
    Chachandu-UK

    ReplyDelete
  7. Kipenga kimeshapigwa...saini zimeshawekwa...hakuna kurudi nyuma. Wabongo tuamke sasa. Ushindani ndio huo unakuja...

    Badala ya kuuza nyanya na vyakula unpacked, tutengeneze viwanda vya kusindika hivyo vyakula kwa ajili ya soko ambalo limekuwa kubwa sasa.

    Badala ya kulima kitalu kimoja cha mpunga kule Kyela,Shinyanga au Mwanza, tufikirie kulima zaidi kuilisha East Africa....

    Tukikaa kulalamika haitasaidia...kikubwa ni ardhi ambayo bado iko kwa sheria za nchi husika...

    Competition kwenya ajira itatufanya tutachangamke zaidi..

    ReplyDelete
  8. Huu ni muda muafaka sasa kwa watz kutumia fursa mbali mbali zinazokuja na hili soko la pamoja. Kuingia kwa Rwanda na Burundi ni changamoto kubwa sana kwa maendeleo ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Awali zilipokuwa nchi tatu pekee Uganda, Kenya na Tanzania hali ya kutokuaminiana kwa wanajumuia ilikuwa kubwa. Ninachokiona ujio wa hizi nchi mbili utapunguza sana hiyo hali.

    Kwa hiyo soko linapanuka sana, fursa mbali mbali za kibiashara na kazi zinaongeza, ushindani nao pia unaongezeka.

    Watz inabidi tujiweke kwenye hali ya ushindani tuone ni jinsi gani tunaweza kupenya na kuingia kwenye masoko mapya. Kwa mwanzo mwanzo inaweza kuonekana kuwa kazi ngumu lakini kadri tunavyosonga mbele tutaweza kuwa washindani wa kweli. Tuachane na hofu zisizo na msingi kwamba tutamezwa na baadhi ya nchi. Hatutakiwi kukaa na kusubiri, tunatakiwa kutoka na kuanza kufukuzia deals. Tusiwe wachoyo kujulishana.

    ReplyDelete
  9. kuna mdau pia amejaribu kujadili maana ya soko la pamoja ni mtanzania mwenzetu mnawe kumwangalia hapa
    http://www.godnyam23.blogspot.com

    ReplyDelete
  10. Watanzania acheni kuwa short-sighted na kuwa na hii inferiority complex. Mnaweza kushindana, na kama anon wa Mon Nov 23, 05:01:00 PM alivyosema, tunahitaji ushindani, especially kutoka kwa watu ambao, kihistoria ni ndugu zetu, ili tuamke kwa sababu wengi wetu tumelala bado usingizi tororo.

    Hii imenikumbusha watu wanaosema, 'ooh fulani siyo mmarekani mweusi, hata kama amezaliwa huko kwa sababu siyo descendant wa watumwa', wanasahau kwamba hao watumwa walivyochukuliwa hazikubebwa familia na koo nzima, kuna kaka, dada na wazazi walioachwa. Anyway niishie hapo ili nisiende nje ya mada, lakini nadhani kuweka emphasize kwenye bishara kuhusu hii kitu ndiyo inaleta kutoelewana huku, lakini tutafika tu.

    ReplyDelete
  11. Nikisema naomba hiki kitu kisitokee katika uhai wangu nitakua ni mchoyo maana vizazi vijavyo hiki kitu kitatokea, ila ukweli ni kwamba sababu zilizovunja ule umoja wa kitambo kile bado zipo. Nakumbuka enzi zile za yale malori toka Kenya yalivyokua yakibomoa barabara safarini kwenda Zambia ilikua ni balaa! Mwalim Nyerere wakati ule aliamua kuyapiga marufuku baada ya Wakenya kupuuzia agizo la kupunguza uzito. Ni kwa kua walinufaika sana ndio maana waling'ang'ania na walifanya hivyo sababu ya patriotism yao. Binafsi nilishawalaani maana waliniulia kaka yangu kipenzi aliyekua daktari kwenye hospitali ( nadhani ni Kenyata Hosp) kipindi cha muungano ati kisa alikua bosi wao na wao walikua chini yao. Ile roho yao ya chuki wakenya bado haijafutika na kama kunayeyote anayefanya kazi au kuishi na hawa jamaa ataniambia. Karibuni hapa imetokea mgongano wa kibiashara kati ya Serengeti na TBL sababu kubwa hasa(mtizamo wangu) ni kufifia kwa mauzo ya bia za Kenya kwenye soko letu kutokana na TBL kuuza sana bia zake za Kilimanjaro Safari,Ndovu. Sasa wenzetu umoja wa wauzaji walitukumbusha kuhusu zile dhihaka zikionesha ati bia yetu inanywewa na nyani,enzi za kukuta condom iliyotumika,viwembe kwenye bia zetu. Ni nani amesahau kuhusu propaganda za makusudi kabisa ati mlima Kilimanjaro upo Kenya! Kuna aliyesahau wanyama walivyokufa baada ya wakenya kutandaza fensi ili kuzuia wanyama wasirudi Tanzania sehemu wanapozalia na kukuzia wanyama wasirudi Serengeti toka Masai mara? Watu hawa waliozuia mabasi ya Watanzania yasiingie Kenya yakiwa na makondakta wa kitanzania ati leo tuungane nao tuwe kama Morogoro na Iringa au Arusha na Kilimanjaro? Binafsi naomba Mungu atuepushie,sijui kuhusu Rwanda na Burundi lakini kwa namna DRC wanavyoteseka na hawa Intarahamwe ambao ni wahutu, narudia tena Mungu atuepushie na janga hili

    ReplyDelete
  12. ETI LIMEFIKISHA MIAKA KUMI LILIANZA LINI? MBONA HATUNA HABARI! WALE WALIKULA MAGUNIA YA CHUMVI NAHISI WANAJUWA SHIRIKISHO LILIVYOKUWA YAANI LILE LILOKUFA, WATU WALIKUWA HURU KWENDA KUFANYA KAZI MAHALA POPOTE PALE TULIKUWA NA WATANZANIA KIBAO KENYA NA UGANDA WAKIFANYA KAZI POSTA, BANDARI, RELI, EAA NA KAZI NYINGI TU, KINACHOFANYIKA SASA NI KUWA WAKENYA NA WAGANDA WANAKIMBILIA KAZI TANZANIA HATA ZA SHOP ASSISTANT, HOUSE GIRLS, SHAMA BOYS LAKINI WATANZANIA HATA ILE YA KUZOWA MAVI BARABARANI HUPATA SI KENYA WALA UGANDA SASA SHIRIKISHO HILI LINA MAANA GANI, MTASEMA WAFANYABIASHARA WANAUZA NYANYA KENYA, SO THAT IS IT? TUWEKANE WAZI TUSINEANE HAYA, TUAMBIWE SHIRIKISHO HILI MAANA YAKE NINI NA MIPAKA YAKE NI IPI NA LITATUKWAMUAJE SISI WANANCHI WA KAWAIDA. WE WANNA NOT POLICAL GIMMICK, WE WANNA REAL THINGS TO REAL PEOPLE. SASA HIVI MTU AKIENDA SOMA NCHI INGINE NDANI YA SHIRIKISHO UNATOZWA ADA KAMA INTERNATIONAL STUDENT YAANI MARA 4 YA WANAYOLIPA LOCAL SASA NINI MAANA YA SHIRIKISHO?

    ReplyDelete
  13. free market ndio mwanzo wa mwisho wa dar empire, lake zone tutafanya biashara zaidi na hizo nchi wanachama mf vifaa vya ujenzi kama simenti ni bei rahisi sana kuliko dar, bandari mombasa, mazao na mifugo ya lake zone vitaenda kwa hao wenye njaa na huko vyakula bei ni juu mkulima wa huku atapanda chati(ni kweli sisi tunauza raw materials)

    kanda ya ziwa tunapenda sana hii kitu

    ReplyDelete
  14. Our Politicians are the reason why Tanzania is poor and will continue to be poor. They don't care about Tanzania's the long-term interest! With leaders like Mwapachu, Tanzania doesn't need enemies; these people are selfish, and worst of all, self centered. No wonder they have failed to find solution to our muungano (Zanzibar and Tanganyika).

    Have we asked ourselves , what will happen if one of the member state government will be overthrown? My take , this muungano is doomed for failure because of its porous foundation.

    ReplyDelete
  15. Most of us afraiding this unit because of the perception we had on former Kenya and those days when we embraced Ujamaa na Kujitegemea. Today's Kenya is not that one we used to know. After sacking Ujamaa na Kijitegemea, Tanzania has hugely improved in terms of education and people's awareness on international businesses.I lives with kenyans in UK and for your information they see Tanzania as a very big threat to take them out from what it is used to be their reigning status around East Africa. Infact we have leapfrogged Kenya and people are not aware on this. Mfano mdogo sana, angalia celebrities toka ulaya wanavyokanyaga TZ sasa hivi kuja kutalii Bongo. Hii ina maana Wizara husika zinafanya kazi vizuri au hospitality industry yetu ipo juu zaidi ya kenya kwa sasa. Miaka kumi tu iliyopita masupa staa wote walikuwa wanaishia Kenya. Tuache Uoga, Soko la pamoja ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu, it should't be an issue nani anapata maendeleo makubwa zaidi ya mwenzake, hicho kisiwe kipimo cha mtu kuona soko la pamoja ni baya. Swala ni Umejengewa uwanja kupata maendeleo ila umeshindwa kucheza mwenyewe. Wacha uwanja ujengwe, na madini tuliyonayo Kenya watasoma namba tu.

    ReplyDelete
  16. Maskini wasiwasi wa wabongo humesababishwa na viongozi waliopita madarakani na waliopo madarakani hivyo si walaumu. Ila mimi ninawapa moyo kwa kusema hivi:
    Kwanza east Africa si tutakuwa tunatumia kiswahili?eheeeee!!!!!wabongo twaweza kuanzisha misamiahati ambayo si mkenya wala mganda ataelewa na hii itatupa kuuza vitabu vya kiswahili bei maradufu.Pili pandisha kodi ya vyumba maana inaonekana tukialalisha,Tanzania ndo tambalale kila mmoja anakimbilia huku sasa tubanda twangu huko kijichi si tutapata soko? Haya tena kwa wale waganga wa kienyeji zidisheni mbwembwe maana wakenya wanaamini kwamba mganga halisi hupatikana TZ.Na mengine mengi.

    ReplyDelete
  17. Hii itafanya Mwanza kuwa jiji kubwa la kibiashara kuliko Dar na Nairobi kama mnabisha subirini,Mwanza watakuwa na biashara na nchi tano kwa wakati mmoja na bandari itawasaidia sana,wajanja wote Mwanza inaita hapo..

    ReplyDelete
  18. Wabongo wasisahau issue kubwa ya quality kwenye products watakazokuwa wanaingiza sokoni!

    ReplyDelete
  19. uwwwwwwwiiiiii jamamni uwiiiii jamani watanzania kweli kabisa kila kitu tulicho nacho ndo ivyo tena kinakwenda kwisha habari yetu kwisha kwisha.wakenya hapa moshi ndani ya miezi miwili tu hii wamefungua benki yao ya KCB na wanatarajia kufungaua supermarket yao ya nakumatt yaani jamani uwiii kweli nahitaaji mmtu wa kunibembeleza!!1

    ReplyDelete
  20. Faida za soko la pamoja Afrika. Hebu tuangalie:

    1.INVESTMENT: Kutanua soko kama walivyofanya akina JK na wenzie kutahamasisha wawekezaji toka nje kuinvest Tanzania wakitafuta cheap labour, ardhi nzuri kwa kilimo, na political stability. Hii ni nzuri kwa Tanzania. lakini miundombinu ni lazima tufanye kipaumbele. On this, I think tusipoangalia, tutakuwa tunauza embe na kuimport radio na pikipiki toka Kenya.

    2. SOKO: Walivyosema hao juu ni sawa. Kwa watakaoweza zalisha, EA itawapa soko kubwa sana kwa products zao. Kwa watakaozembea, watafunga biashara na viwanda vyao.

    As things stand now, hii ni nzuri kwa Kenya, but I am not sure if our infrastructure is ready to accommodate any serious expansion of industrial activity. Umeme taabu, maji safi tatizo, shortage ya skilled labour ndio haisemeki; hii situation itatufanya tu-attract viwanda vya sabuni na vitenge India tu. Serikali ni lazima itangaze a master plan that will streamline our strategies ili tuweze ku- take advantage ya hii investment potential. Otherwise EA itakuwa ni black spot on JK's record... As if the National soccer team has not caused him a severe enough headache!

    3. ELIMU Na WATAALAMU: Haya makubaliano ya soko la pamoja ni lazima yaangalie mbinu za kupunguza BRAIN DRAIN toka EA kuelekea ughaibuni. Mojawapo ya hizi mbinu ni ku-adjust employment laws ili zisaidie free movement of expert workers within EA, na kutoa mishahara based on local market demands. Vinginevyo huu Muungano wa EA tutakuwa tunawatandikia mkeka ma-TX feki toka Ulaya na pengine China(?) wakati wataalamu wetu wazuri tu wakiendelea kukimbilia nchi za nje.

    4. UJASIRIAMALI: Tanzania tutafaidika tu na soko hili kama Mabenki na financial sector yetu itaweza kusapoti wananchi wasio matajiri lakini wenye nia ya kupanua biashara zao ili wafaidike na soko la jumuiya ya EA. Vinginevyo, ni viwanda vichache tu vya akina mafisadi papa ndivyo vitakavyofaidika na hili soko tanuzi la EA. Nawasilisha.

    ReplyDelete
  21. Kuungana jamani ni siri ya Urembo!!

    Wamarekani waliishitukia hii wakaanza kuungana tangu karne zilizopita, zamani zile states zote zilikuwa nchi tofauti,angalia sasa wanavyopeta.

    European union ndio recent example wanapeta sana, tena kuwa na common currency kumewasaidia sana kuwa stable. Vita zilizokuwa zinatokea miaka ya 1940s within Europe leo hii haziwezi kutokea tena kwa sababu hizi nchi zimeungana,Mjerumani ataanzia wapi kumpiga muholanzi?labda kimichezo tu nani anapiga boli zaidi.

    Watanzania kazeni buti msiogope wakenya wanapembe?

    ReplyDelete
  22. ilianza miaka 10 ilopita????sielewi

    sasa km sie wasomi hatujui sijui yaweje kwa mtanzania wa chini zaidi,aya ngoja twende umo then tuone yaweje,kwani lazima tuiishinao milele?km ilopita ilivunjika na hii si tutaona tuuu??

    shime watanzania lets join them n see the benefits or else we call it quit!!!

    asa sula la ardhi eti wageni watamiliki ardhi kwa masharti maalumu cjui ni yapi hayo???

    ebu nyie viongozi tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha mtutanabaishe kwa umakini tuelewe

    ni hayo tu

    ReplyDelete
  23. mdau hapo juu...kweli mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla tuko juu

    me nilikuja huku na nimewekeza ardhi adi kieleweke

    dar mapumziko tuuuu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...