JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA UMMA

USAJILI WA NAMBA ZA SIMU ZA MKONONI
1. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa agizo kuwa namba
zote za simu za mkononi zisajiliwe kati ya Julai 1 2009 hadi
Desemba 31, 2009; na baadaye muda huo kuongezwa hadi tarehe
30 Juni 2010 ikitamkwa wazi kuwa muda huo wa ujasili
hautaongezwa tena. Sababu za kuanzisha utaratibu wa kusajili
namba za simu zimeelezwa mara kadhaa zikiwemo:
(i) Kuwalinda watumiaji dhidi ya matumizi mabaya ya huduma za
mawasiliano
(ii) Kuwezesha na kurahisisha utambuzi wa wateja watumiapo
huduma mbalimbali kama M – Pesa, Z-pesa, ZAP na huduma
nyingine za malipo ya Ankara kama za Umeme, Maji,
Televisheni n.k.
(iii) Kuimarisha usalama wa nchi.
(iv) Kuyawezesha makampuni ya simu kuwafahamu wateja wao
vizuri zaidi ili kurahisisha na kuboresha utoaji wa huduma
kwao.
2. Wakati tunakaribia tarehe 30 Juni 2010, utaratibu umepangwa
kupitia Makampuni ya simu kuwa kuanzia tarehe 1 Juni 2010
kuhakikisha laini yoyote itakayonunuliwa itatumika kwa kupiga au
kupokea simu na kutuma au kupokea ujumbe ikiwa imesajiliwa
tu na si vinginevyo.
2
3. Baada ya saa sita usiku tarehe 30 Juni yaani saa 00.00 kuanzia
tarehe 1 Julai, 2010 namba yoyote ambayo itakuwa haijasajiliwa
itafungiwa kupiga ,kupokea simu pamoja na ujumbe wa maandishi
(SMS) kwa siku 90 hadi tarehe 30 Septemba 2010. Katika kipindi
hiki cha siku 90 endapo mtumiaji ataisajili namba yake
itafunguliwa. Kwa namba ambazo hazitakuwa zimesajiliwa ifikapo
tarehe 30 Septemba zitafutwa na kuondolewa kwenye mitandao
kabisa.
4. Mamlaka ya Mawasiliano imekubaliana na Makampuni ya simu
kufanya uhakiki wa usajili wa laini za simu za wateja kwa kutumia
namba 106 kupitia simu za mkononi. Kwa wateja wa mitandao
iliyoko katika mifumo ya GSM, kama Zain, Vodacom, MIC (Tigo) na
Zantel, wateja wanatakiwa kuingiza *106# na kwa wateja wa
mitandao inayotumia mfumo wa CDMA kama BOL, TTCL mobile na
SASATEL wateja watatakiwa kupiga namba 106 na watapokea
taarifa za usajili.
5. Hivi karibuni mswada wa sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na
posta ulipitishwa na Bunge kuwa sheria. Sheria hiyo inafanya usajili
wa namba za simu za mkononi kuwa ni wa lazima kwa mujibu wa
sheria hio kuanzia sasa na kutofanya hivyo ni kosa la jinai. Adhabu
ni pamoja na faini au kifungo au vyote pamoja.
6. Mamlaka ya Mawasiliano inapenda kuyashukuru makampuni ya simu
na watumiaji kwa ushirikiano ambao wameonesha mpaka sasa kwa
ajili ya kufanikisha zoezi hili.Tunawasihi wote waendelee kusajili
laini mpya kabla ya matumizi baada ya tarehe 30 juni 2010 na
kuendelea kuhakiki laini zote zilizosajiliwa ili kukamilisha usajili
kama ilivyokusudiwa.
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Anayefanya HafanywiJune 30, 2010

    Ni zoezi litakaloshindwa kwa mara nyingine tena na safari hii siyo kwa watu wenye line za simu pekee bali na makampuni ya simu pia. Inakuwaje mtu awe amejiandikisha tangu mwaka jana na bado awe hajaingizwa kwenye data base.

    Wazo la uandikishaji ni zuri sana lakini inavyoonekana hayajakuwepo maandalizi ya kutosha.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2010

    HAYO MAKAMPUNI ILI KUWAPUNGUZIA ADHA WATEJA WAO, MIMI NAOMBA KWA WALE AMBAO TAYARI CMU ZAO ZIMEISHASAJILIWA WAWATUMIE UJUMBE UNAWAHAKIKISHIA KAMA WAMEISHASAJILI KULIKO SASA HIVI MTU UNAHANGAIKA KUPIGA NA.106 LAKINI HAKUNA MAJIBU.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2010

    Ukweli ni kuwa makampuni ya simu yalikuwa ayajajiandaa kabisa, kwa sababu tupo tuliosajili simu zetu mara tu baada ya zoezi ili kuanza lakini cha ajbu mpaka leo eti hatujasajiliwa rasmi!!!! iki ni kichekesho kikubwa!!
    sasa kama sisi wa mwanzoni hatujasajiliwa vipi hawa wa mwishoni si miaka zaidi ya mitatu? mkitufungia ni uonevu mkubwa!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2010

    Mimi nilisajili mwaka jana lakini sasa naambiwa kuwa sijasajiliwa hivi ni vichekesho wakuu. Na namba ya kuangalia kama umesajiliwa imetolewam imechelewa sana sijui itakuwaje?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 30, 2010

    MIMI NILISAJILIWA NA DADA MMOJA AMBAYE NI BAAMEDI ALIAJILIWA KUSAJILI SIMU NA NILIKUWA NA MASHAKA NA UHAKIKA WA USAJILI WAKE HATA HIVYO MAADAMU ALIAJILIWA MIMI NILILAZIMIKA KUMPA TAARIFA ZANGU. HAYA NDIYO MATATIZO TUNAYO WATANZANIA YA KUPEANA ULAJI BILA KUJALI UBORA WA KAZI NA TULIYAONA KWENYE SENSA YA TAIFA AMBAPO MABAAMEDI WALIAJILIWA.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 30, 2010

    1 (iii)&(iv) - crap!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 30, 2010

    HI We regsitered our numbers Long time back but suprisingly we are told to check again in 106. the answer is unregistered, what a system!!!!! What about our confidentiality of records now?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 30, 2010

    Hapo tunaongelea makampuni tu. Sasa, hebu fikiria: Mimi jina langu la kweli ni Saidi Ali Mvungi. Nilinunua simu na lne ya simu bila kuisajili. Leo nataka kujisajili kwa kutumia hiyo njia ya 106 alafu ninadangaya kuwa jina langu ni Elikana Akilimali. Kampuni itahakikishaje kuwa msajili wa simu ndiye mmiliki wa simu? Mfumo wa vitambulisho? Mfumo wa anuani ili kutambua anuani ya mtumiaji? Picha ya mwenye line ya simu? Bado kuna mambo hayako wazi kiasi cha kutosha hapa....Naomba kuelimishwa kidogo hapa tafadhali...

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 30, 2010

    Hii itafail big time. Toka mwanzoni nilivyosoma nilijua kuna mapungufu mengi tu. Sijui ni nani huyu alipewa hii tenda.

    Baada ya hii sheria kupita bado walikua wanatoa number mpya bila kuzisajili hapo hapo.

    Kusumbua bibi zetu tu hapa. Bibi alishasajili siku zote hizo lakini leo tena anaawmbiwa number haijasajiliwa....

    Mlaaniwe kabisa mnaojali matumbo yenu tu bila kufikiria makero mnayowapatia watu wengine

    Mtakua mkaa wa kuchoma wengine nyie ngojeeni tu siku yenu ikifika.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 30, 2010

    Hiyo TCRA na makampuni ya simu wote wameoza, mtu unasajili mara tatu bado unaambiwa hujasajiliwa,

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 30, 2010

    HAMNA SABABU YOYOTE YA MSINGI YA KUSAJILI SIMU KATI YA HIZO ALIZOZITAJA HAPO JUU. NI USUMBUFU TU. KWANI MNASAJILI KWA NANI SERIKALI AU KAMPUNI YA SIMU? KWANI UKIDANGAYA JINA LAKO WATAJUWAJE? KWANI UNAPONUNUWA SIM CARD UNAPOITUMIA KWA MARA YA KWANZA SI UTAKUWA PROMPTED KUISAJILI KWA SERVICE PROVIDER AU INAKUWAJE MAKUMPUNI YA HUKO KWETU. ETI KWA AJLI YA USALAMA TAIFA, KWANI WATU HAWAWEZI KUFANYA MABAYA BILA YA KUTUMIA SIMU? UPWAGUZI MTUPU.MAKAMPUNI YENYEWE HAYAJIANDAA KWA VILE COST IS INVOLVED KATIKA KU-CREATE DATA BASE YA HUO USAJILI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...