Da' Aisha ambae anaishi mji wa kusoma (yaani Reading) nchini UK, amelamba nondozzz ya pili ya business administration wiki iliyopita, na kuamua kusheherekea na ndugu pamoja na marafiki zake kwa juhudi na mfano mkubwa aliouonyesha kwa watanzania wengine, na wanawake kwa ujumla. Hongera sana dada Aisha Mkassi, kwa kutudhihirishia watu tulioko ughaibuni kwamba, tusikazane na kubeba maboxi tu bali pia tukumbuke kilichotuleta huku ughaibuni. Mungu akubariki na akupe maisha bora zaidi Da'Aisha..
Da' Aisha na Shangazi yake pamoja na rafiki yake Kubra
Da' Aisha na shangazi yake baada ya kulamba nondozzz ya MBA
Da' Aisha akila pozi baada ya kulamba nondozzzz yake ya Master ya Business Administration
HONGERA,MUDA WA KUWEKA CHETI DARINI NA KUREJEA KUBEBA BOXI.
ReplyDeleteNi kweli hongera kwake ila pia usimkatishe tamaa, hapohapo pia kubeba box sio kubaya kama mtu anauwezo wakubeba hilo box, Kuliko kwenda kubeba maunga au kuuza banGi na kufanya wizi usiokuwa na msingi, Elimu muhimu sana, unapopata kazi pia muhimu bila ya wabeba box tuliokuwa juu(maofisi ya makaratasi na kutype) wapi tungepata vyakula? Bila hao wabeba box? kila mtu anamsaidia mwenzake kazi zetu pia zisingeenda.
DeleteSio wote walioenda nje nia yao kusoma na iwe kupiga box au kutokupiga box muhimu kwamba mtu anafanya kazi ambayo si ya wizi wala ya kimagendo ww shukuru na mungu aliokupa uwezo nalo sizani kama mtu akipiga box kuna ubaya kwa mungu au akipata pia degree kunaubaya kwa mungu inategemea na Degree kaipata kwa njia zipi na box analopiga ni la njia ipi msiwawekee watu zarau mkipata degree hata muuza nyanya hapa kwetu ni anafanya kazi bora kuliko anayeiba wizi mdogo au mkubwa ni wizi. Ushauri tu ungesema tusome na hasa Elimu ya Dunia na ya Dini zaidi ndio itayofikisha watu kwa muumba kuliko chochote na bidii ya kujituma inavyotakiwa kwa muenendo anaoutaka mungu. Hongera na Allah akuzidishie Elimu zaidi na zaidi ya hiyo unayoisoma na akujalie kupata kazi yenye manufaa itayokusaidia mbele ya safari Ameen.
ReplyDeleteTatizo leno Watanzania manafikiri ukimaliza shule uajiliwe. Elimu au degree ni kitu ambacho kinakupa tu uwezo wa kufikiri, kwa hiyo tumia uwezo huo kujiajili au kufanya mambo mengine. Huku ughaibuni degree is nothing. kuna PHD holders wengi tu wana beba box lakini pia wana mitikasi yao. Poleni sana kwa hizi fikira zenu but you need u people ni exposure. Tembea muone mambo msiige tu au kufanya manayo hadithiwa bila kuhakikisha.
ReplyDeletehao wenye dharau ndiyo wajinga na inawezekana wanaujua ukweli ila wivu tu kwanini wengine waishi nje, kwanza huku viwanja hata wazoa taka na mavi wanathaminiwa ili mradi wanafanya kazi yao halali, acheni dharau kwa kuwa mungu ndiye anayetoa na ndiye aliyewezesha mtu kupata visa na kufanikiwa kuja kiwanja. Bora ukose kazi bongo uwe mwizi au ubahatike uje kiwanja na kupiga box.
ReplyDeleteout upoleum
Chukua tano ww smart bila degree.
DeleteHongera dada Aisha usiwajali walimwengu na yawalimwengu. Ikiwa umepata uwezo engezea na DBA ama PHD. Anaesema na asema shauri lake.Hana jipya kijiba cha roho tu basi.
ReplyDelete