Majengo ya shule ya msingi Nkenja, kulia na kushoto ni vyumba vya madarasa, katikati ni ofisi ya mwalimu mkuu.
Uongozi wa CCM wilaya ya makete ukishangaa kuona jinsi wanafunzi wanavyopata tabu kusomea kwenye pagale.
Madarasa ambayo hayajakamilika lakini yanatumiaka kwa ajili ya darasa la kwanza na la pili.
Turubai likining'inia kwenye chumba ambacho wanasomea wanafuzni wa darasa la kwanza na la pili ambalo hulitumia kama bati kuzuia jua.

Na Edwin Moshi, Makete
Mazingira magumu hasa kwa elimu ya msingi nchini bado yanazidi kuonekana baada ya shule ya msingi Nkenja iliyopo kata ya Kitulo wilayani Makete mkoani Njombe kuonekana ina vyumba viwili tu vya madarasa ambavyo vina hadhi ya kutumiwa kama madarasa


Hali hiyo si imeacha hoi mtandao huu tu bali pia viongozi mbalimbali waliofanya ziara ya kukagua shule hiyo ambayo ilijengwa kwa makusudi ya kuwapunguzia wanafunzi mwendo mrefu wa kilomita 14 wanaotembea kwenda kusoma shule ya msingi Ujuni iliyopo kijiji cha jirani cha Ujuni

Mbali na shule hiyo kuwa na vyumba viwili vya madarasa, chuma kimoja wanasomea wanafunzi wa darasa la tatu na la nne kwa kuchanganywa pamoja, na chumba kimoja wanatumia darasa la tano tu peke yao

Hayo yamebainika baada ya ziara ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula kufanya ziara katika shule hiyo kukagua hali ya ujenzi na maendeleo kwa ujumla katika shule hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika kata mbalimbali wilayani hapo

Viongozi hao wa CCM wamezidi kushuhudia maajabu katika shule hiyo kwa kujionea chumba ambacho wanasomea wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kikiwa hakina paa, bati wala sakafu ambapo wakati mwingine waalimu hukifunika kwa turubai ili kuwakinga na jua na wakati wa mvua havitumiki

"kama mnavyojionea ndugu viongozi wa CCM hali ni ngumu kwa kweli, tunaupungufu wa vyumba vitano vya madarasa, watoto wa darasa la kwana na la pili wanasomea kwenye chumba hiki ambacho hakina bati muda wote, wakati wa mvua hakitumiki kabisa, na wote tunawachanganya kwenye chumba hiki kimoja" alisema mwalimu mkuu Hester Mahenge

Viongozi hao ambao walikagua vyumba vyote vya shule hiyo pia waligundua shule hiyo ina upungufu wa madawati 50

Akizungumza shuleni hapo katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu amewapongeza wananchi wa Nkenja kwa kujitoa kwa gharama zao hadi hapo madarasa mawili yanayojengwa yalipofikia, na kuwaomba kushirikiana na kutilia mkazo suala hilo ili ujenzi huo ukamilike ndani ya mwaka huu

Amesema pamoja na wananchi hao kukabiliwa na michango mingi lakini watoe kipaumbele kwa ujenzi huo ili wanafunzi hao wasome kwa raha ukizingatia wanafunzi wanaosomea pagalani ni wa darasa la kwanza na pili ambao ndio wachanga wanaohitaji msaada kwa ukaribu zaidi

Naye mwenyekiti wa CCM wilayani hapo Francis Chaula amewataka kuandika bajeti ya vitu vinavyohitajika na gharama zake ili kukamilisha miradi hiyo na waipeleke kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya na nakala kwa chama chake ili kutilia mkazo zaidi namna ya kuboresha mazingira ya shule hiyo

Diwani wa kata ya Kitulo ilipo shule hiyo Mbosa Tweve amesema serikali kupitia halmashauri ya wilaya kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 imetoa sh. milioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na muda wowote kuanzia sasa zitapelekwa shuleni hapo na kuahidi kushirikiana kukamilisha ujenzi huo

baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wamelalamikia michango ya ujenzi huo kuchangwa na kitongoji kimoja tu ilihali kijiji kina vitongoji vinne na kusema hali hiyo inachangia mradi huo kusuasua, huku hoja hiyo ikijibiwa na mwenyekiti wa kijiji hicho Zablon Chengula kuwa amesawaita wenyeviti wa vitongoji vyote kuzungumzia suala hilo na wapo wananchi ambao wameshapelekwa kwa mtendaji wa kata kushughulikiwa kutokana na kugoma kushiriki zoezi hilo

Shule hiyo ina madarasa matano (I-V) ina jumla ya wanafunzi 51 wanaofundishwa na waalimu watatu tu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mimi ningekuwa Mwenyekiti wa Wilaya wa CCM ningefanya yafuatayo
    1. ninegoma kuendelea na ziara yangu hadi hizo milioni nane zilizoahidiwa na Halmashauri zitoke
    2. Kabla ya kuondoka ningeitisha hio mikutano na vitongoji vingine ili nipate ahadi zao za kuchangia
    3. Ningehamasisha wapenda maendeleo walioko mjini Makete wajitolee mabati yanayohitajika kuezekea hilo darasa moja
    4. Ningesaidia kuezeka hayo mabati
    5. Nikifika makete ni kuwachangisha wadau wangu kwa ajili ya hayo madawati 50
    Baada ya kumaliza hayo ndio ningeendelea na msafara wangu nikiwa na uhakika nimekiacha chama changu imara
    Che

    ReplyDelete
  2. Hii imenisikitisha sana.....yaani kumbe Tanzania kuna majengo kama haya ya shule! Hawa watoto wanasoma kwa shida sana and then walimu pia wanamazingira mabaya.... I hope serikali inafanya hima kumalizia haya manyengo.

    ReplyDelete
  3. Mdau kwa kwanza wa maoni.

    Kwa nini wajitolee wananchi haliyakuwa pesa ya kuwanunuliwa watoto wao uniform hanala leo uwambie watoe mabati ? watoto wao hana hata malapa, wanaenda shule, hawana ma book na vitabu vya kusomea, huko skool hakuna hata chaki ya kuandikia ubaaoni.

    Nauliza

    Haya ndio maendeleo ambayo ccm inajisifia maiaka 50 kwa maisha bora ya mwananchi ? Unajua sisi tulioko mijini tunaona poa nchi iko fresh sana, lakini hali iko vijijini, sio kijiji hicho tu viko vingi sana pande ya tanganyika.

    Ushauri wangu kwa wananchi.

    Sasa imefika wakati kubadilika, wachague viongozi ambao watakao waletea maendeleo badala kutumia siasa kama mtaji wa chakula, ukapewa 5000 uipigie kura ccm au mbunge iwe chadema wa cuf.

    Pili kutoa tamko mara moja kwa wanakijiji serikali kutoa mchango haraka au kufanya maandamano kuongesha msisito kwa serikali kuchukizwa kwao kwa kutowathamini.

    Nne suala la kujenga shule sio la mwananchi, ni suala la serikali kuhakikisha kwamba kila mwananchi anaata elimu bora na bure, kuwakamua wananchi sio haki, nchii hii imejaaliwa na rasilimali nyingi na uchumi mzuri, kwa nini washindwe kuwajengea watanzania mashule yalio bora ?

    ccm imeshindwa kuleta mageuzi, aibu aibu kwenu, Miguloooo

    ReplyDelete
  4. Wadau ya nini mtoane kamasi na majasho bure hapa Jamvini wakati muhusika mwenye Jimbo hilo ameshakula Mafao ya Ubunge na anakula maisha Dodoma?

    Kama sija kosea Shule hiyo ipo katika Jimbo la Mhe.Peter Msigwa wa Chadema!!!

    ReplyDelete
  5. Kazi kwenu wana CCM na CHADEMA !!!

    Siasa sio tu ule wakati wa Kampeni za Uchaguzi kwa kuwaomba Kura wananchi.

    Fedha zimesha liwa na Halmashauri limebaki jukumu lenu ili mambo kuwa hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...