Majengo ya shule ya msingi Nkenja, kulia na kushoto ni vyumba vya madarasa, katikati ni ofisi ya mwalimu mkuu. |
Uongozi wa CCM wilaya ya makete ukishangaa kuona jinsi wanafunzi wanavyopata tabu kusomea kwenye pagale. |
Madarasa ambayo hayajakamilika lakini yanatumiaka kwa ajili ya darasa la kwanza na la pili. |
Turubai likining'inia kwenye chumba ambacho wanasomea wanafuzni wa darasa la kwanza na la pili ambalo hulitumia kama bati kuzuia jua. |
Na Edwin Moshi, Makete
Mazingira
magumu hasa kwa elimu ya msingi nchini bado yanazidi kuonekana baada ya
shule ya msingi Nkenja iliyopo kata ya Kitulo wilayani Makete mkoani
Njombe kuonekana ina vyumba viwili tu vya madarasa ambavyo vina hadhi ya
kutumiwa kama madarasa
Hali
hiyo si imeacha hoi mtandao huu tu bali pia viongozi mbalimbali
waliofanya ziara ya kukagua shule hiyo ambayo ilijengwa kwa makusudi ya
kuwapunguzia wanafunzi mwendo mrefu wa kilomita 14 wanaotembea kwenda
kusoma shule ya msingi Ujuni iliyopo kijiji cha jirani cha Ujuni
Mbali
na shule hiyo kuwa na vyumba viwili vya madarasa, chuma kimoja
wanasomea wanafunzi wa darasa la tatu na la nne kwa kuchanganywa pamoja,
na chumba kimoja wanatumia darasa la tano tu peke yao
Hayo
yamebainika baada ya ziara ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete
Francis Chaula kufanya ziara katika shule hiyo kukagua hali ya ujenzi na
maendeleo kwa ujumla katika shule hiyo ikiwa ni muendelezo wa ziara
yake katika kata mbalimbali wilayani hapo
Viongozi
hao wa CCM wamezidi kushuhudia maajabu katika shule hiyo kwa kujionea
chumba ambacho wanasomea wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kikiwa
hakina paa, bati wala sakafu ambapo wakati mwingine waalimu hukifunika
kwa turubai ili kuwakinga na jua na wakati wa mvua havitumiki
"kama
mnavyojionea ndugu viongozi wa CCM hali ni ngumu kwa kweli,
tunaupungufu wa vyumba vitano vya madarasa, watoto wa darasa la kwana na
la pili wanasomea kwenye chumba hiki ambacho hakina bati muda wote,
wakati wa mvua hakitumiki kabisa, na wote tunawachanganya kwenye chumba
hiki kimoja" alisema mwalimu mkuu Hester Mahenge
Viongozi hao ambao walikagua vyumba vyote vya shule hiyo pia waligundua shule hiyo ina upungufu wa madawati 50
Akizungumza
shuleni hapo katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu amewapongeza
wananchi wa Nkenja kwa kujitoa kwa gharama zao hadi hapo madarasa
mawili yanayojengwa yalipofikia, na kuwaomba kushirikiana na kutilia
mkazo suala hilo ili ujenzi huo ukamilike ndani ya mwaka huu
Amesema
pamoja na wananchi hao kukabiliwa na michango mingi lakini watoe
kipaumbele kwa ujenzi huo ili wanafunzi hao wasome kwa raha ukizingatia
wanafunzi wanaosomea pagalani ni wa darasa la kwanza na pili ambao ndio
wachanga wanaohitaji msaada kwa ukaribu zaidi
Naye
mwenyekiti wa CCM wilayani hapo Francis Chaula amewataka kuandika
bajeti ya vitu vinavyohitajika na gharama zake ili kukamilisha miradi
hiyo na waipeleke kwa mkurugenzi mtendaji wa wilaya na nakala kwa chama
chake ili kutilia mkazo zaidi namna ya kuboresha mazingira ya shule hiyo
Diwani
wa kata ya Kitulo ilipo shule hiyo Mbosa Tweve amesema serikali kupitia
halmashauri ya wilaya kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2013/2014 imetoa sh.
milioni 8 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na muda wowote kuanzia sasa
zitapelekwa shuleni hapo na kuahidi kushirikiana kukamilisha ujenzi huo
baadhi
ya wananchi wa kijiji hicho wamelalamikia michango ya ujenzi huo
kuchangwa na kitongoji kimoja tu ilihali kijiji kina vitongoji vinne na
kusema hali hiyo inachangia mradi huo kusuasua, huku hoja hiyo ikijibiwa
na mwenyekiti wa kijiji hicho Zablon Chengula kuwa amesawaita wenyeviti
wa vitongoji vyote kuzungumzia suala hilo na wapo wananchi ambao
wameshapelekwa kwa mtendaji wa kata kushughulikiwa kutokana na kugoma
kushiriki zoezi hilo
Shule hiyo ina madarasa matano (I-V) ina jumla ya wanafunzi 51 wanaofundishwa na waalimu watatu tu
mimi ningekuwa Mwenyekiti wa Wilaya wa CCM ningefanya yafuatayo
ReplyDelete1. ninegoma kuendelea na ziara yangu hadi hizo milioni nane zilizoahidiwa na Halmashauri zitoke
2. Kabla ya kuondoka ningeitisha hio mikutano na vitongoji vingine ili nipate ahadi zao za kuchangia
3. Ningehamasisha wapenda maendeleo walioko mjini Makete wajitolee mabati yanayohitajika kuezekea hilo darasa moja
4. Ningesaidia kuezeka hayo mabati
5. Nikifika makete ni kuwachangisha wadau wangu kwa ajili ya hayo madawati 50
Baada ya kumaliza hayo ndio ningeendelea na msafara wangu nikiwa na uhakika nimekiacha chama changu imara
Che
Hii imenisikitisha sana.....yaani kumbe Tanzania kuna majengo kama haya ya shule! Hawa watoto wanasoma kwa shida sana and then walimu pia wanamazingira mabaya.... I hope serikali inafanya hima kumalizia haya manyengo.
ReplyDeleteMdau kwa kwanza wa maoni.
ReplyDeleteKwa nini wajitolee wananchi haliyakuwa pesa ya kuwanunuliwa watoto wao uniform hanala leo uwambie watoe mabati ? watoto wao hana hata malapa, wanaenda shule, hawana ma book na vitabu vya kusomea, huko skool hakuna hata chaki ya kuandikia ubaaoni.
Nauliza
Haya ndio maendeleo ambayo ccm inajisifia maiaka 50 kwa maisha bora ya mwananchi ? Unajua sisi tulioko mijini tunaona poa nchi iko fresh sana, lakini hali iko vijijini, sio kijiji hicho tu viko vingi sana pande ya tanganyika.
Ushauri wangu kwa wananchi.
Sasa imefika wakati kubadilika, wachague viongozi ambao watakao waletea maendeleo badala kutumia siasa kama mtaji wa chakula, ukapewa 5000 uipigie kura ccm au mbunge iwe chadema wa cuf.
Pili kutoa tamko mara moja kwa wanakijiji serikali kutoa mchango haraka au kufanya maandamano kuongesha msisito kwa serikali kuchukizwa kwao kwa kutowathamini.
Nne suala la kujenga shule sio la mwananchi, ni suala la serikali kuhakikisha kwamba kila mwananchi anaata elimu bora na bure, kuwakamua wananchi sio haki, nchii hii imejaaliwa na rasilimali nyingi na uchumi mzuri, kwa nini washindwe kuwajengea watanzania mashule yalio bora ?
ccm imeshindwa kuleta mageuzi, aibu aibu kwenu, Miguloooo
Wadau ya nini mtoane kamasi na majasho bure hapa Jamvini wakati muhusika mwenye Jimbo hilo ameshakula Mafao ya Ubunge na anakula maisha Dodoma?
ReplyDeleteKama sija kosea Shule hiyo ipo katika Jimbo la Mhe.Peter Msigwa wa Chadema!!!
Kazi kwenu wana CCM na CHADEMA !!!
ReplyDeleteSiasa sio tu ule wakati wa Kampeni za Uchaguzi kwa kuwaomba Kura wananchi.
Fedha zimesha liwa na Halmashauri limebaki jukumu lenu ili mambo kuwa hapo.