Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE, Imepongezwa na kushukuriwa na watu wenye ulemavu wa kutoona, kwa  kuwakomboa kutoka walemavu omba omba, na kuwageuza kuwa ni wajasiliamali wanaojitegemea na kuchangia maendeleo ya Taifa.

Pongezi hizo, zimetolewa na wahitimu wa kwanza, wa mafunzo ya kushona nguo kwa wasiona, yaliyofadhiliwa na TANTRADE na kuendeshwa na mtu asiyeona, Abdala Nyangarika,  wakati wa mahafali yaliyofanyika jana katika viwanja vya Tantrade, Kilwa Rd, jijini Dar es Salaam.

Wahitimu hao, wamezitoa pongezi hizo katika risala yao, iliyosomwa na mmoja wao, Philemon Isaka, ambao kwanza waliishukuru na kuipongeza TANTRADE kwa  kuwathamini watu wenye ulemavu, kisha kujitolea kuwakomboa kwa kuwajengea uwezo, wa  kujitegemea,  hivyo kuwaepusha kugeuka omba omba. Ila pia wametoa wito kwa jamii, kuungana na TANTRADE kuwapatia vifaa ili waweze kujitegemea. TANTRADE imejitolea kuwapatia mafunzo tuu, lakini ili waweze kujitegemea, jamii imeombwa kuwapatia vyerehani na mitaji, ili ujuzi walioupata, uweze kuwasaidia kujitegemea na kuchangia maendeleo.
Wahitimu wa mafunzo ya kushona nguo kwa wasiiona, wakiwa kwenye picha ya pamoja wakiwa na na nyuso za furaha, wakionyesha vyeti vyao vya kuhitimu mafunzo ya kushona kwa cherehani kwa watu wenye ulemavu wa kutoona, baada ya kuhitimu mafunzo haya ya miezi 6, , yaliyoendeshwa na mkufunzi mwenye ulemavu, Dr. Abdalah Nyangalio na kufadhiliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, TANTRADE. Wahitimu hao, wameomba jamii iwasaidie kupata cherehani ili waweze kuutumia ujuzi walioupata, kujitegemea badala ya kuendelea kuwa omba omba.

Kwa Upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Edwin Rutageruka, baada ya TANTRADE kugundua kipaji cha  kushona cha Abdala Nyangalio, mwenye ulemavu wa kutoona, ilimpatia fursa kushiriki maonyesho ya sabasaba, na maonyesho mbalimbali ya nje ya nchi, ndipo ikaamua kuanzisha mafunzo hayo ili kuutumia utaalamu wa Nyangalilo kuwasaidia wasiona wengine wenye vipaji vya ushonaji bila kujijua.

Rutageruka ametoa wito kwa Jamii kujitokeza kununua bidhaa za walemavu hawa, ili kuwaunga mkono, na kwa upande wake, amesema TANTRADE  itaendelea kuwafungulia fursa, watu wenye ulemavu, ili kuvitumia vipaji vyao mbalimbali kuzalisha mali,  kwa kuwaunganisha  na masoko kupitia maonyesho ya Saba Sana, na kuwapeleka soko la Afrika ya Mashariki hatimaye kuzitumia fursa za soko la AGOA.

Mgeni rasmi  ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, aliyewakilishwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke, Mafuku Kabeya, ameipongeza TANTRADE kwa kuanzisha mafunzo hayo, na kutoa wito kwa  jamii na taasisi ziunge mkono juhudi za TANTRADE  ili kutanua wigo wa mafunzo hayo kuwafikia  walemavu wengine mbalimbali wenye vipaji, kuwafundisha wengine kujitegemea na kuchangia maendeleo ya taifa.
Mkufunzi wa mafunzo ya kushona kwa wasiiona, ambaye yeye mwenyewe haoni, Dr. Abdalah Nyangalio akimuonyesha Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke Mafuku Kabeya, (katikati), nguo zilizoshonwa na watu wenye ulemavu wa kutoona, walizoshona kwa cherehani, baada ya kuhitimu mafunzo haya ya miezi 6, yaliyo fadhiliwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania, Tantrade. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TANTRADE, Edwin Rutageruka. Wahitimu hao, wameomba jamii iwasaidie kupata cherehani ili waweze kuutumia ujuzi walioupata, kujitegemea badala ya kuendelea kuwa omba omba.

Mwenyekiti wa Chama cha Wasiona cha Mkoa wa Dar es Salaam,Alex Lwimbo, ameiomba jamii na taasisi kujitolea  kusaidia uwezeshaji ya watu wenye ulemavu, ili waweze kujitegemea, kwa hoja kuwa walemavu wakiwezeshwa, wanaweza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...