Na Editha Karlo,wa blog ya jamii,Kigoma.

HATIMAYE aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma kwa zaidi ya miaka 30,  Taufiq Malilo amezikwa huku sehemu kubwa ya wananchi wa mkoa Kigoma wakijitokeza kuhudhuria mazishi hayo.

Shekhe Malilo ambaye alifariki Ijumaa jioni ya wiki iliyopita kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kisukari na moyo amezikwa juzi jioni katika makaburi ya Kazaroho Ujiji mjini Kigoma.

Katika mazishi hayo yaliyofanyika majira ya saa 11 jioni yaliacha vilio na simanzi kwa mamia ya waislam waliohudhuria msiba huo, wengi wakikumbwa mafundisho ya dini ya kislam katika kuishi maisha ya kumcha Mwenyezi Mungu.

Akisoma Wasifu wa marehemu Katibu wa BAKWATA wilaya ya Kigoma vijijini ,Sheikh Yassin Kabunguru alisema kuwa Alhaji Malilo alichaguliwa kuwa Sheikh wa mkoa Kigoma mwaka 1979 hadi mauti yalipomfika akiwa pia Ulamaa wa Taifa.

Sheikh Kabunguru alisema kuwa katika uhai wake Alhaji Malilo alifundisha dini na kutembelea misikiti zaidi ya 600 mkoani Kigoma akiweka kambi kwa ajili ya kufundisha dini na kufungua shule mbalimbali za kiislam mkoani Kigoma kwa juhudi kubwa ambayo aliifanya binafsi.

Akitoa mawaidha kabla ya kuelekea makaburi Sheikh Uwesu Mohamed alisema kuwa Alhaji Malilo aliishi katika misingi sita ya kiislam ambayo ilimfanya kuwa mcha Mungu,mnyenyekevu anayewapenda wengine,asiye na tamaa wala kujilimbikizia mali na kwamba Marehemu amekufa akiwa hana hata gari kutokana na sehemu kubwa ya kipato chake kutumia kuendeleza masuala ya dini.
 Waumin wa dini ya Kiislam wakisalia mwili wa Marehemu Sheikh Taufiq Malilo aliyekuwa Sheikh wa mkoa Kigoma kabla ya mwili huo kupelekwa makaburi ya Kazaroho kwa mazishi.
 Mamia ya waumini wa dini ya kiislam na wananchi wa mkoa Kigoma waliojitokeza nyumbani kwa Marehemu Taufiq Malilo aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma Muda mfupi kabla ya mwili kuzikwa
 Mamia ya waumini wa dini ya kiislam na wananchi wa mkoa Kigoma waliojitokeza nyumbani kwa Marehemu Taufiq Malilo aliyekuwa Shekhe wa mkoa Kigoma Muda mfupi kabla ya mwili kuzikwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...