Na  Bashir  Yakub.

 Wako  wasimamizi  wa  mirathi  wa  aina  mbili. Kwanza ni  yule  ambaye  marehemu  mwenyewe  amemteua  kabla  ya  kufa  kwake  na  akaandika/kusema  kwenye  wosia  kuwa  fulani  ndiye  atasimamia  mirathi  yangu  baada  ya  kuondoka.

Pili,  ni  yule  ambaye  hakuteuliwa  na  marehemu  mwenyewe  bali   ameteuliwa  na  wanafamilia  kwenye  kikao  cha  familia. Kwa  walio  wengi  huyu  ndiye  tunamjua  kuwa  ni  lazima  jina  lake  lipelekwe  mahakamani  kwa  ajili  ya  kuthibitishwa  ili  aweze kuwa  msimamizi  kamili.  Makala yatapitia Sheria  ya  Usimamizi  wa Mirathi, Sura ya 352  na kanuni zake.

1.      HAKI  NA  WAJIBU  WA  WASIMAMIZI  WA  MIRATHI.

Haki  na  wajibu  wa  msimamia  mirathi  aliyeteuliwa  na  marehemu kabla ya kifo na  ambaye  hakuteuliwa na marehemu ni  sawa. Awe  aliteuliwa  na  marehemu  mwenyewe  au  aliteuliwa  na  wanafamilia  bado  haki  na wajibu  alionao  ni  uleule. 

Wajibu  mkuu  wa  msimamia  mirathi  ni  kuwa  mwadilifu, na  kuenenda  kwa  mujibu  wa  sheria  katika  kila  hatua  anayopiga katika  kusimamia  kwake  mirathi.


2.    SIO  LAZIMA  MSIMAMIZI  WA MIRATHI  AWE  NDUGU/MWANAFAMILIA.

Hili ni  muhimu  zaidi  kulieleza.  Sio  kweli  kuwa  msimamizi  wa  mirathi  lazima awe  mtoto  wa  marehemu, shangazi, baba  mdogo/mkubwa,  mjomba kaka,dada nk.  Bali  msimamizi  wa  mirathi  anaweza  kuwa yeyote.  Suala  la  msingi  ni  atimize  sifa  za  kuwa  msimamizi  wa  mirathi. Na katika sifa hamna udugu.

Hakuna  haja  ya  kuwa  na  ugomvi  kuwa  msimamizi  wa  mirathi  lazima  atoke  katika  familia. Hakuna  ulazima  huo  ikiwa  mmeshindwa  kuaminiana  kwenye  familia. Mnaweza  kumteua  hata  kiongozi  wa  dini au  mtu  mwingine  yeyote  muadilifu  ambaye  mnadhani  ataweza  kutenda  haki  katika usimamizi.

Jambo  jingine  msimamizi  wa  mirathi  sio  lazima  awe  mmoja. Ikiwa  kuna  pande mbili  zinazozana  basi  sheria  inaruhusu  kila  upande  kutoa  msimamizi  wa  mirathi  ili  alinde  maslahi  ya  upande  wake.  Kwahiyo  wasimamizi  watakuwa  wawili   na  sheria  haikatazi.

Nyongeza ya  hapo ni kuwa hata kampuni  au taasisi  inaweza kuteuliwa kusimamia mirathi.


                   KUSOMA  ZAIDI  sheriayakub.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...