Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
SERIKALI
imetoa tamko kuhusu ushiriki wa mwanariadha Alphonce Simbu katika
mashindani ya Jumuiya ya Madola yanayotarajiwa kufanyika April mwaka
huu.
Mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika
Gold Coast nchini Australia, ambapo Serikali na Kamati ya Olimpiki Taifa
(TOC) walipokea barua kutoka kwa Simbu ya kuomba ashiriki mashindano ya
London Marathon ambayo ni makubwa zaidi kuliko ya Jumuiya ya Madola.
Simbu
ambaye ni mshindi wa tatu wa London Marathon 2017, Serikali kwa
kushirikiana na Chama cha Riadha (RT) na kamati ya Olimpiki (TOC)
walikaa katika kikao cha pamoja Januari 13 mwaka huu na waliridhia ombi
la Simbu kuweza kushiriki huko na pia aweze kupata muda wa kujiandaa
zaidi ili kuiwakilisha vyema Taifa katika mashindano hayo.
Akitolea
ufafanuzi huo, Ofisa habari wa Baraza la Michezo Taifa (BMT) Najaha
Bakari amesema kuwa Watanzania wasiwe na hofu kwani wameshafanya
uchaguzi wa wawakilishi wa kwenda kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola
na wanaamini kuwa watafanya vizuri zaidi na kurudisha medali nyumbani.
Mbali
na hilo, Najaha amesema kuwa vyama vyote vya michezo nchini vilivyopo
chini ya BMT wanatakiwa kuwasilisha kalenda za mwaka kabla ya Februari
10 mwaka huu na kwa chama chochote ambapo hakitafanya hivyo
watachukuliwa hatua kali za kisheria.
"Kuna
vyama kila mwaka vinakuwa haviwasilishi kalenda yao ya mwaka ambapo
mfano wake ni Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) ambao wao
wanaona ni chama kikubwa sana ila wanatakiwa wajue kuwa wote ni wadogo
na wanatakiwa wawasilishe kalenda yao BMT,"amesema Najaha.
Najaha
amesisitiza kuwasilishwa kwa kalenda hizo kutasaidia katika kuandaa
miundombinu ya viwanja kwani kumekuwa na muingiliano wa baadhi ya
matukio ya michezo kutokana na kutokuwa na kalenda za vyama vyao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...