Mkoa
wa Mbeya ni moja kati ya Mikoa 32 ya Tanzania, unapatikana nyanda za
juu kusini mwa nchi yetu hii. jina la mkoa wa Mbeya ni neno la kiasili
la kabila la Kisafwa lilikuwa likitamkwa ‘Ibheya’ likiwa na maana
chumvi. Inaelezwa kuwa wafanyabiashara wengi walikuwa wakifika eneo hilo
kwa biashara ya kubadilishana chumvi na mazao yao.
Inaelezwa
kuwa mji wa sasa wa Mbeya ulianzishwa na wakoloni Waingereza mnamo
mwaka 1927 kufuatia kushamiri kwa upatikanaji wa dhahabu kwenye milima
ya Loleza na mkondo wake uliokwenda mpaka kufika mji wa Chunya.
Wakazi wenyeji wa mkoa wa Mbeya ni wa kabila la Wasafwa ambao
wamekuwa wakihamia milimani kupisha wageni. Kukua kwa kasi kwa jiji la
Mbeya kumepelekea wenyeji hao kuuza maeneo yao na wao kurudi maeneo ya
milimani wakiendelea kujishughulisha na kilimo pamoja na ufugaji kidogo.
Mkoa
wa Mbeya kwa sasa una wilaya nne, hii ni baada ya kugawanywa kwa mkoa
huo na Mkoa wa Songwe ambao nao pia umebakiwa na wilaya nne ambazo ni
Ileje, Chunya, Mbozi na Momba.
Leo hii eneo la wilaya
ya Mbeya ambako ndipo jiji lilipo limetawaliwa zaidi na Wanyakyusa na
Wakinga wakiwa ndiyo wafanyabiashara wakubwa na Wahindi pia.
Wenyeji wengine wa Mbeya ni watu wa kabila la Wamalila, Wenyeji
wa wilaya za Rungwe na Kyela ni Wanyakyusa Wenyeji wa
wilaya ya Mbarali ni Wasangu, Wawanji, Wabena na Wakinga.
Wenyeji wa wilaya ya Ileje
ni Wandali, Wenyeji wa wilaya ya Chunya ni Wabungu ingawa watu waishio
huko zaidi ni Wanyiha. Wenyeji wa wilaya ya Mbozi ni Wanyiha na
Wanyamwanga, lakini mji wa Tunduma umetawaliwa zaidi na Wakinga ambao
ndiyo wafanyabiashara wenye kumiliki uchumi wa mji huo mdogo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...