MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, kuongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga. Akizungumza katika mkutano na wanahabari, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Mwanasha Tumbo alisema kuwa hafla hiyo itakayoanza Kesho Ijumaa saa 12 jioni kwenye Hoteli ya Golden Tulip ya Masaki, Dar es Salaam itaambatana na chakula cha usiku kwa wageni waalikwa.

Hivi sasa Wilaya hiyo haina Hospitali ya Wilaya na wananchi wanaohitaji huduma za afya wamekuwa wakitumia hospitali teule ya Kanisa la Anglikana ambayo imeingia mkataba na Serikali na kutokana na idadi ya wananchi wa wilayani hapo hospitali hiyo imezidiwa.


Hayo yamesemwa leo na Mhandisi Tumbo wakati akizungumzia harambee ya kuchangisha fedha inayotarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanasha Tumbo (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya Harambee ya uchangiaji wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga. Kutoka kushoto ni Katibu wa Kamati ya Harambee hiyo, Hassan Msumari na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hamis Mgoda. IMeandaliwa na Richard Mwaikenda.
Wajumbe wa Kamati ya Harambe hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mkutano na wanahabari kwenye Hoteli ya Golden Tulip, katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Juma Mgazija, Mwenyekiti wa Kamati, Hamis Mgoda, Mkuu wa Wilaya, Mhandisi Mwanasha Tumbo, Katibu Tawala wa Wilaya, Desderia Haule na Katibu wa Kamati, Hassan Msumari.


Mhandisi Tumbo amesema kutokana na Wilaya ya Muheza kutokuwa na Hospitali ya Wilaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974, wananchi wamekuwa wakiteseka pindi wanapohitaji huduma za afya na hivyo wakaamua kuchanishana fedha ili kuanza ujenzi wa hospitali hiyo.

Amefafanua tayari wananchi na wadau wa maendeleo wilayani Muheza mkoani Tanga na Watanzania kwa ujumla wameanza kuchingiaa ujenzi huo na hadi kukamilika kwake zinahitajika fedha Sh.bilioni 11.1, hivyo wakati wakisubiri fedha za Serikali Kuu na zile za kwenye bajeti wameamua kuanza kwa kuchangisha fedha hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...