Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willium Lukuvi ametatua mgogoro mkongwe wa ardhi huko Boko kata ya Dovya maarufu kama kwa Somji jijini Dar es salaam.
Akizungumza na wananchi Lukuvi ameeleza Rais John Magufuli amempa maelekezo sambaba na kumaliza mgogoro huo.
Amesema kuwa ardhi hiyo ni mali ya Serikali na wananchi waliojenga makazi yao ni wavamizi kwani eneo hilo la hekari 366 lilichukuliwa na serikali rasmi mwaka 1975 kutoka kwa Somji ambaye alikuwa mmiliki wa eneo hilo.
Aidha ameeleza kama Serikali haiwezi kuvunja majengo ya wakazi hao ila lazima wafuate taratibu zilizowekwa ili kupata umiliki halali wa viwanja hivyo.
Lukuvi ameeleza lazima mipaka yote ya shamba la Somoji la mwaka 1952 ipimwe ili iweze kujulikana pia ofisi za mipango miji za wizara na Manispaa iangalie kama kuna mipango yoyote ilitokea kuhisiana na eneo hilo.
Ameeleza kwa wenye hati na michoro lazima ihakikiwe kama ipo sahihi sambamba na maelezo ya ya wamiliki kuhusiana na umiliki wao.
Lukuvi ameeleza kuwa kamati iliyoundwa itashirikiana na wataalamu wa wizara ambao watapima maeneo hayo na kugaiwa kwa wananchi na kuanza kuyalipia kodi rasmi na zoezi limalizike mwezi Septemba mwishoni ili wananchi wakabidhiwe hati zao rasmi.
Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi, akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Boko ambapo ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 katika eneo la Somji lenye hekari 366 jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka wa Globu ya jamii)
Mbunge wa Kawe Halima Mdee akizungumza na wananchi katika mkutano huo wa kutatua mgogoro wa ardhi ambapo ameishukuru serikali kwa kutatua mgogoro huo.
Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Boko ambapo ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 katika eneo la Somji lenye hekari 366 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Mhe. William Lukuvi akijibu maswali mabalimbali aliyoulizwa na wananchi wa Boko ambapo ametatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 katika eneo la Somji lenye hekari 366 jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuele Massaka wa Globu ya jamii)
Baadhi ya wananchi wa Boko wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi katika mkutano huo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...