WADAU wa habari mkoa wa Dodoma wameshauriwa kutumia wanahabari katika kuchochea mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye ngazi zote za utawala ili kuhabarisha umma.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino Athuman Masasi katika mkutano uliowakutanisha wadau wa habari mkoa wa Dodoma ambao ulilenga kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu uhusino baina yao na wanahabari na upatikanaji habari zinahusu maendeleo ya mkoa huo.

Mkutano huo uliandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC) kwa ufadhili wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa habari nchini(UTPC) ambao hufanyika kila mwaka.Akichangia majadiliano kwenye mkutano huo, Masasi alisema tasnia ya habari ni muhimu kwa ustawi wa Mkoa huo na Taifa kwa ujumla na kuwahakikishia wanahabari kuwa halmashauri za mkoa wa Dodoma kwa sasa zina mipango na shughuli nyingi za maendeleo hivyo zinahitaji wanahabari kufikisha taarifa hizo kwa wananchi.

Aidha aliwaomba wanahabari kuwasiliana na mamlaka za serikali hasa pale wanapopata taarifa za tatizo lolote ili kujua juhudi za serikali za kupambana nalo.Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Dodoma(CPC), Habel Chidawali aliwataka waandishi kuondokana na uandishi wa mazoea ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano.

Aidha aliwaomba wadau katika mkoa wa Dodoma kuvitumia vyombo vya habari katika kutangaza fursa zinazopatikana katika maeneo yao kwa kuwa vina uwezo wa kufikia kundi kubwa la wananchi.Naye, Mwandishi mkongwe nchini, Edna Ndejembi alisema kuwa ili Mkoa wa Dodoma uweze kufikia maendeleo yake hauna budi kuvitumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kwani kwa kufanya hivyo utatoa fursa kubwa kwa wadau kujitokeza na kuwekeza mkoani hapa.

Alisema mkoa wa Dodoma una fursa nyingi kwenye Nyanja mbalimbali ikiwemo kilimo cha zabibu ambazo zinahitaji kutangazwa ili kupata wawekezaji na kuwezesha mji huo kukua hasa ikizingatiwa tayari umepewa hadhi ya kuwa Jiji.Pamoja na hayo, Mlezi wa CPC Daniel msangya alisisitiza waandishi kujiendeleza kielimu na kujisoma vitabu na sheria mbalimbali ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma Habel Chidawali akifungua Mkutano wa wadau wa habari mkoani Dodoma.
Wajumbe wa mkutano
Mwanahabari Mkongwe Edna Ndejembi akizungumza katika mkutano wa wadau mkoani Dodoma.
Mlezi wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoa wa Dodoma(CPC) Daniel Msangya akichangia katika mkutano wa wadau wa habari wa mkoa huo.
Mwanahabari Idd Maalim akichangia kwenye mkutano wa wadau wa habari Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Chamwino akizungumza katika mkutano wa wadau wa habari Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...