Na Magreth Kinabo, Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma amekitaka Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kufanya tafiti katika baadhi ya Sheria ambazo zinahitaji marekebisho ili kuweza kuongeza uzito wa mabadiliko hayo.

Mhe. Jaji Mkuu aliyasema hayo mapema Agosti 17, alipotembelewa na wajumbe wapya wa Baraza la Uongozi wa TAWLA, ambao waliongozwa na Mwenyekiti wao, Bi. Athanasia Soka na Mkurugenzi wa TAWLA, Bi. Tike Mwambipile, waliofika kwa ajili ya kujitambulisha rasmi.

Akizungumzia kuhusu mabadiliko hayo ya Sheria, Jaji Mkuu alisema yanawezekana kufanyika endapo utatifi wa kina utafanyika ili kuongeza uzito wa mabadiliko hayo, “ni vizuri unapotaka kufanya mabadiliko kisheria kufanya utafiti ,tunaweza kufanya kwa kushirikiana,” alisema Jaji Mkuu.

Awali akizungumzia kuhusu mabadiliko ya Sheria yanayohitajika, Mkurugenzi huyo wa TAWLA, Bi. Tike Mwambipile, aliitaja Sheria ya ndoa.

“Katika sheria hii mathalani kumekuwa na mgawanyo wa mali usio sawa hususani pale ambapo mwanaume inapothibitishwa ndiye anamiliki mali hupata asilimia nyingi na mwanamke hupata asilimia chache wakati ikithibitika mwanamke ndiye anamiliki mali hugawanywa asilimia 50 kwa asilimia 50,” alisema Bi. Mwambipile. 

Mhe. Jaji Mkuu akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa TAWLA, Bi. Athanasia Soka. 
Mhe. Jaji Mkuu akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Mwenyekiti wa TAWLA, Mhe. Jaji Mkuu pia amewapatia nakala za Mpango Mkakati wa Mahakama. 
Mhe. Jaji Mkuu akikabidhi zawadi mbalimbali kwa Mwenyekiti wa TAWLA, Mhe. Jaji Mkuu pia amewapatia nakala za Mpango Mkakati wa Mahakama. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...