Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Freeman Mbowe anayekabiliwa na kesi ya Uchochezi namba 112 ya mwaka huu amesafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini akiwa mahututi kwa ajili ya matibabu ya moyo na shinikizo la damu.

Hayo yameelezwe leo Novemba Mosi mwaka huu na Wakili Peter Kibatala mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali, (PH).

Wakili Kibatala ameieleza Mahakama kuwa alimuhoji mdhamini wa Mbowe, Grays Celestine na akamueleza kuwa Mbowe amesafirishwa jana jioni akiwa mahututi kuelekea Afrika Kusini na nyaraka za usafiri na matibabu zitawasilishwa kwa barua mahakamani.

Kibatala alieleza kuwa Mbowe amekuwa akifika mahakamani mara kadhaa bila kukosa, hivyo adhabu kwamba kueleza anaidharau mahakama kwani hata kitendo cha kumtuma mdhamini wake si jambo la dharau.Kutokana na taarifa hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu Faraja Nchimbi ameiomba Mahakama itoe amri ya kumkamata mara moja Mbowe ili ajieleze kwani dhamana aliyopewa na mahakama isifutwe kwa kushindwa kuiheshimu.

Baada ya mdhamini huyo kueleza hayo, Hakimu Mashauri alimuuliza kama ana nyaraka ya kuithibitishia mahakama kuwa Mbowe amesafiri nje ya nchi kwa Matibabu lakini mdhamini huyo alidai kuwa hana na kwamba mshtakiwa akirejea atawasilisha nyaraka za safari na Matibabu kwa mahakama na upande wa mashtaka. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...