Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

MCHEZAJI maarufu wa zamani wa Timu ya Arsenal ya Uingereza Robert 
Pires amewasili nchini Tanzania leo Novemba 1,2018 kwa mwaliko maalum wa Benki ya Barclays kwa lengo la kushiriki uzinduzi wa Kampeni ya benki hiyo inayoitwa Superfans.

Pires akiwa nchini kwenye kampeni hiyo ambayo itampa nafasi mteja mwenye akaunti ya biashara au anayetumia kadi kufanya manunuzi mara nyingi kipindi cha kampeni fursa ya kujishindia bahati nasibu ya safari ya Uingereza kushuhudia mechi moja mubashara ya ligi Kuu ya Uingereza.

Akizungumza leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya Pires kutua nchini, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Barclays Tanzania Aron Luhanga amesema ujio wa mchezaji huo ni maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni hiyo na atakuwa nchini kwa siku tatu.

"Gwiji wa zamani wa timu ya Arsenal Robert Pires amekuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuzindua kampeni ya wateja iitwayo Superfans inayomwezesha mteja anayemiliki akaunti ya biashara au anayetumia kadi ya Barclays kufanya manunuzi mara nyingi kuzawadiwa safari ya Uingereza kushuhudia mechi mubashara ya Ligi Kuu ya Uingereza,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...