Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imekwama kuendelea na usikilizwaji wa kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake, inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa (Takukuru),Godfrey Gugai kutokana na kuchelewa kupatikana kwa kibali cha kuwaita mashahidi kutoka mikoani.

Wakili wa serikali kutoka Takukuru Vitilis Peter ameeleza hayo leo Februari 20.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, pindi kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kusikilizwa.

Amedai,  waliomba kibali cha kuwaita mashahidi kutoka mikoani lakini wamepata taarifa kuwa kibali hicho kimepatikana leo na kusababisha wao kushindwa kuandaa mashahidi.

Amedai,  ili shahidi aweze kutoa kuleta kutoa ushahidi akiwa anatokea mkoani ni lazima kipatikane kibali kwa sababu atatakiwa kulipwa.

Haya hivyo,  wakili wa utetezi, Alex Mgongolwa ameuomba upande wa mashitaka kuwataja mashahidi watakaowaleta ili kuweka kumbukumbu ili asipokuja mmoja aletwe shahidi mwengine.

Akijibu hoja hiyo, Wakili Peter amedai hawawezi kutaja majina ya mashahidi hao ila mahakama itambue kuwa mashahidi wawili wanatokea Mwanza na watatu wanatokea Musoma. 

Kufuatia hayo,  Hakimu Simba amewataka upande wa mshitaka kuhakikisha wanaleta mashahidi ili kesi hiyo iweze kuendelea.

Kesi hiyo, imeahirishwa hadi Hakimu hadi Machi 4 na 6, mwaka huu kwaajili ya kuendelea na ushahidi kwa upande wa mashitaka.

Mbali na Gugai, washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni George Makaranga, Leonard Aloys na Yasin Katera.

Gugai na wenzake wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo, makosa 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Katika kesi ya msingi, Gugai na mwenzake, wanakabiliwa na makosa 43, kati ya hayo 19 ni ya kughushi, 23 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali, ambalo linamkabili Gugai.

Gugai anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo alitenda kosa hilo kati ya January 2005 na Decembea 2015.

Inadaiwa kuwa akiwa Takukuru Dar es Salaam, Gugai alikuwa akimiliki mali za zaidi ya Sh bilioni 3.6 ambazo hazilingani na kipato chake huku akishindwa kuzitolea maelezo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...