RAIS wa Ufaransa Emmanuel Macron ameyatembelea maziara ya Wayahudi baada ya makaburi 80 ya Wayahudi kuharibiwa kwa makusudi ambapo wanasiasa wa pande zote wanalaani vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi.

Imeelezwa kuwa Rais Macron jana Jumanne alikwenda kwenye jimbo la Alsace mashariki mwa Ufaransa ambapo makaburi 80 ya Wayahudi yaliharibiwa kwa makusudi na kukashifishiwa kwa kaulimbiu za kifashisti.

Rais Macron alikutana na viongozi wa Wayahudi wa sehemu hiyo na kusisitiza dhamira ya kupambana na chuki dhidi ya Wayahudi katika kila namna itakayojitokeza na kwamba vitendo 541 vya chuki dhidi ya Wayahudi viliripotiwa mwaka jana nchini Ufaransa. Takwimu hizo zinawakilisha ongezeka la aslimia 74, kulinganisha na mwaka 2017.

Pia Rais Macron amelaani uharibifu uliofanywa kwenye makaburi hayo ya Wayahudi, ambapo amesema  chuki dhidi ya Wayahudi ni kinyume na maadili ya Ufaransa na kwamba taifa lote la Ufaransa, linapaswa kupinga kadhia hizo. 

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amelaani vitendo hivyo vya kushtusha vilivyomfanya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Israel atoe mwito kwa Wayahudi wa nchini Ufaransa kurejea nyumbani, Israel. 

Waziri Mkuu Netayahu amesema jambo lililotokea ni la kushtusha nchini Ufaransa.Makaburi 80 ya Wayahudi yameharibiwa na kubandikwa nembo za Manazi na watu wanaowachukua Wayahudi. 

Hata hivyo jamii ya Waislamu nchini Ufaransa wamefanya maandamana kupinga chuki dhidi ya Wayahudi. Wakati huo huo waziri mkuu wa Poland alibatilisha mpango wa nchi yake wa kupeleka ujumbe kwenye mkutano wa mjini Jerusalem baada ya waziri wa mambo ya nje wa Israel, Israel Katz kusema kwamba Poland ilishirikiana na mafashisti na kuongeza kuwa Wapolish walinyonya maziwa ya kuwatia chuki dhidi  ya Wayahudi.

Naye Balozi wa Marekani nchini Poland amemtaka waziri huyo wa Israel aombe radhi. Balozi huyo  Georgette Mosbacher amesema Israel na Poland ni washirika thabiti wa Marekani na kwamba hawapaswi  kujibizana. Balozi huyo wa Marekani nchini Poland amesema ushirika wao ni muhimu na kwamba matatizo  yote yanaweza kutatuliwa baina ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa tahtmini ya msomi Jürgen Ritte, mhadhiri kwenye chuo kikuu cha Sorbonne mjini Paris vitendo vya chuki dhidi ya Wayahudi vimeongezeka nchini Ufaransa. Msomi huyo amesema chuki hiyo  inatoka sehemu mbalimbali. 

Msomi huyo Ritte amesema chuki hiyo inatokana na itikadi kali za kidini na kisiasa. Pia amesema kwamba miongoni mwa wanaharakati wa vizibao vya manjano pia wapo watu  wanaowachukia Wayahudi.CHANZO DW(Mwandishi:Zainab Aziz).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...