Na Ahmed Mahmoud,Arusha.

Mamia ya Wanyarandwa wamekusanyika na kuandamana katika viunga vya jiji la Arusha ikiwa ni ishara ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 tangu kutokea kwa mapigano na mauaji ya Kikabila Nchini na kusababisha mauaji ya maelfu ya Wanyarandwa.

Maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Arusha yanalenga kuhamasisha umoja na amani miongoni mwa wanyarandwa kuungana kama taifa bila kujali tofauti za kikabila .

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanyarandwa wanaoishi katika Mataifa mbalimbali duniani Murenzi Daniel amesema kuwa maadhimisho hayo yanalenga kuwakumbusha kudumisha amani na umoja kama nguzo muhimu ambayo kwasasa hawako tayari kuipoteza na wanawataka Wanyarandwa duniani kote kuungana

Tedy Shungushu ni Mnyarandwa anayeishi jijini Arusha amesema kuwa kumbukumbu hiyo ni ya muhimu kama taifa kujitafakari na kuona namna ambavyo wanawakumbuka watu waliowapoteza katika mauaji hayo na kuwaenzi kila mwaka.

Kwa upande wao Watanzania walioshiriki katika maadhimisho hayo Maurin Njobi na Omega Urio wamesema kuwa yanawakumbusha kama Watanzania kudumisha amani na upendo na mshikamano kama taifa ili kuondoa uwezekano wa matukio kama hayo kutokea nchini

Zaidi ya watu Laki nane wanatajwa kupoteza maisha kwenye mauaji hayo ya Rwanda nchi ambayo kwa sasa inaongozwa na Rais wake Paul Kagame.

 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Neno "Kuadhimisha" hapa halijatumika kwa usahihi. Hawajaandamana "kuadhimisha" kwani hiyo ina maana ya kufurahia, kufanya shangwe, kuwa na furaha kubwa; kwa Kiingereza ni "celebrate". Wanaadhimisha "kukumbuka kwa majonzi au kama kutotaka kusahau" na hapa neno ni "commemorate" Ni kufanya kwa ajili ya kukumbuka tukio zito kama hili. MM Mwanakijiji

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...