Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mwenye Tai nyekundu
akiwa na viongozi wa Mataifa mbalimbali Aprili 7/2019 wakitoa heshima
katika eneo la kumbukumbu ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa akibadilishana Mawazo
na Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo walipo kutana leo Aprili
7/2019
katika Mji wa Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais
Dkt Magufuli katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari
yaliyotokea 1994 nchni Rwanda.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais
Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin Mkapa walipo kutana leo Aprili 7/2019 katika Mji
wa Kigali wakati waziri Mkuu alipokuwa anamuwakilisha Rais Dkt John Magufuli
katika kumbukumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 nchini Rwanda.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na mwenyeji wake Waziri
wa mambo ya Nje wa Rwanda Balozi Richard Sezibera aliyempokea katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa Kigali alipo wasili leo Aprili 7/2019 alipo fika
kumuwakilisha Rais Dr John Magufuli
katika kumbumbu ya miaka 25 ya mauji ya kimbari yaliyotokea 1994 Kkulia ni
Balozi wa Tanzania Nchini Rwanda Balozi Ernest Mangu.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU.
*Awasisitiza Watanzania kudumisha amani, umoja na mshikamano
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kudumisha amani, umoja na
mshikamano ambavyo ni tunu walizoachiwa na waasisi wa Taifa.
Ameyasema
hayo leo (Jumapili, Aprili 7, 2019) katika kumbukumbu ya miaka 25 ya
mauaji ya Kimbari iliyofanyika katika jiji la Kigali nchini Rwanda.
Waziri
Mkuu ambaye amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli katika kumbukumbu
hizo, amewasisitiza Watanzania kudumisha amani na utulivu.
Awali,Waziri
Mkuu alijumuika na viongozi kutoka nchi mbalimbali kutoa heshima kwenye
eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo la Gisozi lililopo jijini Kigali.
Baada
ya kutoa heshima kwenye eneo la kumbukumbu za mauaji hayo, Rais wa
Rwanda, Paul Kagame alitoa maelezo ya kina kuhusu mauaji hayo
yaliyotokea Rwanda 1994.
Viongozi
wengine waliohudhuria kumbukumbu hizo ni pamoja na Rais Mstaafu wa
Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Rais Mstaafu wa Nigeria, Ulusegun
Obasanjo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...