Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imesema kuwa imeanza kutekeleza mkakati wa serikali kusaidia kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati kupitia utekelezaji wa uchumi wa viwanda.

Mwenyekiti wa bodi ya TPB,Dk.Edmund Mndolwa alisema hayo katika futari ya mwezi mtukufu wa ramadhani iliyoandaliwa na benki hiyo kwa viongozi wa serikali na wateja wa benki hiyo wa mkoani Kigoma.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imeazimia kupitia dira ya taifa 2000 - 2025 ya kuifanya Tanzania kufikia uchumi wa kati na kwa namna ya usimamizi unaofanywa na Raisi John Magufuli ni wazi kila sekta lazima ijipange kuhakikisha inatekeleza majukumu ili kufikia lengo jambo ambalo TPB imeshaanza kulitekeleza.

Alisema kuwa moja ya mambo muhimu katika kutekeleza hilo ni kutoa mikopo kwa wateja ambayo itawafanya wawekezaji wa ndani na nje kushiriki kikamilifu kwenye mipango mbalimbali ya kiuchumi na tayari TPB inao mpango kabambe ambao utawawezesha Watanzania kupata mikopo ya aina mbalimbali ili kutekeleza shughuli zao za kiuchumi.

"Maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali katika benki hii imeifanya benki kukua kimtaji, kiuendeshaji na imeongeza wateja kwa kiasi kikubwa na kwa sasa ni benki ya tisa nchini kati ya mabenki ambayo yanajiendesha kwa faida, hivyo ni wakati mzuri kwa wateja kuitumia benki hii kwa kuwa na akaunti lakini pia kuchukua mikopo yenye masharti nafuu ambayo itawasaidia kuendesha shughuli zao za kiuchumi,"Alisema Dk.Mndolwa.

Akizungumza katika futari hiyo kwa wateja wa TPB mkoani Kigoma, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Sabasaba Moshingi alisema kuwa benki imeboresha huduma zake kwa kiwango kikubwa na ndiyo msingi wa ongezeko kubwa la wateja na kuifanya benki hiyo ifanye kazi zake kwa tija.

Moshingi alisema kuwa kwa kuthamini hilo ndiyo maana benki imekuwa ikiandaa hafla mbalimbali ambazo zinawakutanisha viongozi waandamizi wa benki hiyo na wateja na wadau wake ili kuweza kupokea maoni na ushauri mbalimbali ambao wanauchukua na kuufanyia kazi ikiwa ni sehemu ya kufanyia maboresho utoaji huduma katika benki hiyo. 

Mkuu wa mkoa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga alisema kuwa TPB ni benki kongwe ambayo haina budi kuungwa mkono na Watanzania wote kwani sehemu kubwa ya watumishi wa serikali kwa miaka ya nyuma ilikuwa inategemea benki hiyo. 

Maganga aliwakumbusha wateja wa benki hiyo waliohudhuria futari hiyo kwamba msingi wa kukua kwa biashara na shughuli za kiuchumi ni pamoja na kuchukua mikopo ambayo benki ya Posta imerahisisha kwa kuweka masharti nafuu kuweza wateja wake kupata mikopo hiyo.

Shekhe wa mkoa Kigoma, Alhaji Hassan Iddi Kiburwa amesema kuwa kitendo kilichofanywa na benki hiyo kufuturisha waislam na wasio wa islam kwa kupata chakula cha pamoja na kitendo cha kiimani kuwatendea wema wote hivyo kusanyiko hilo la futari limepata baraka za Mwenyezi mungu ambazo zinazidi kuifanya benki hiyo kufany vizuri kwenye shughuli zake.
Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya posta(TPB)Sabasaba Moshingi akizungumza baada ya futari pamoja na waumini wa dini ya kiislam na wateja wao wa Mkoa wa Kigoma futari iliyoandaliwa na benki hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigom Brigedia Mstaafu Emanuel Maganga akizungumza jambo na waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wateja wa benki ya posta(TPB)kwenye futari iliyoandaliwa na bank hiyo Mkoani Kigoma.
Shekhe wa mkoa wa Kigoma Hassan Iddi Kiburwa akiwaongoza waumini wa dini ya kiislam na wateja wa benki ya TPB katika futari iliyoandaliwa na banki hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...