Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala (katikati) akisisitiza jambo kwa timu za Mshauri Mwelekezi na Wajenzi wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la NCC, Kitalu na 18 na 19, jijini Dodoma. Walioketi, kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu na kushoto kwake ni Mkuu wa Timu ya washauri waelekezi wa Mradi, Dkt. Msanifu Majenzi, Isabela Mtani kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam wakati wa makabidhiano ya Mradi huo wa Ujenzi kati ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni mmiliki na SUMAJKT ambayo ni Mkandarasi.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala (katikati) na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu (kulia) kwa pamoja wakisikiliza maelezo ya vipengele vya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Uhamiaji eneo la NCC, Kitalu na 18 na 19, jijini Dodoma toka kwa Mshauri Mwelekezi wa Mradi, Dkt. Msanifu Majenzi, Isabela Mtani wa Chuo Kikuu cha Ardhi , Dar es Salaam (kushoto ) wakati wa tukio la makabidhiano ya Mradi huo wa Ujenzi kati ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni mmiliki na SUMAJKT ambayo ni Mkandarasi. Walioketi mbele, kulia ni Kamishna wa Uhamiaji (Utawala na Fedha), Kamishna Peter Chogero na kushota ni Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Kanali Mabele.

…………………..

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna P. Makakala jana alikabidhi Mradi wa Ujenzi wa jengo la ghorofa nane ambalo litakuwa Makao Makuu mpya ya Uhamiaji eneo la NCC, Kitalu na 18 na 19, jijini Dodoma kwa wakandarasi wa SUMAJKT.

Kamishna Jenerali alisema ” tunaijua sifa ya SUMAJKT kupitia mifano mbalimbali ya majengo bora ambayo wameyakamilisha kwa wakati, na kwa ukweli huu nina imani kubwa nao ya kwamba jengo letu litajengwa kwa ustadi wa hali ya juu na hivyo kuwa ni moja ya majengo ya kisasa yanayovutia hapa jijini Dodoma”.

Kwa upande mwingine tukio hili lilihudhuliwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu na Mkurugenzi Mtendaji wa SUMAJKT, Kanali Mabele ambaye aliahidi kuwa shirika lake litajenga jengo ambalo litakuwa ni kioo cha ubora wa kazi zao na kwamba watu hawata hitaji kwenda jijini Dar es Salaam kuona mifano ya kazi zao bali hapa Dodoma tu.

Aidha, tukio hili lilishuhudiwaa na Mkuu wa Timu ya washauri waelekezi wa Mradi, Dkt. Msanifu Majenzi, Isabela Mtani kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam ambaye alisema kuwa makabidhiano ya Mradi huo wa Ujenzi kati ya Idara ya Uhamiaji ambayo ni mmiliki na SUMAJKT ambayo ni Mkandarasi yatafuatiwa na shughuli nyingi ambazo zimepangwa kwenda kwa haraka sana na bila kuathili ubora wa kazi yenyewe na jengo linalojengwa.

Mradi wa jengo hilo ambalo litakuwa kubwa kuliko lile la Kurasini, Dar es Salaam na ambalo lilikuwa Makao Makuu ya zamani linatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi 18, na kuiwezesha Idara ya Uhamiaji kuanza kutumia jengo bora lenye hadhi ya kimataifa jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...