NA TIGANYA VINCENT

UJENZI wa Hospitali ya Wilaya ya Uyui unatarajia kukamilika mwishoni mwa Mwezi ujao tayari kwa ajili ya kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya wakati akielezea maendeleo ya ujenzi wa majengo saba ya Hospitali hiyo.

Alisema kwa upande wa jengo la Utawala tayari yameezekwa na kuwekewe miundo ya umeme na maji na kwa jengo la kufulia limeshaezekwa.

Msuya alisema kwenye jengo la wagonjwa wa nje(OPD) , jengo la uchunguzi wa mionzi, na , maabara iko kwenye lenta na jengo la stoo ya dawa liko katika hatua ya upauaji baada ya kumaliza hatua ya kufunga lenta.

Alisema kwa upande wa jengo la mama na mtoto liko katika hatua ya kuanza kufungwa lenta. Mkuu huyo wa Wilaya alisema wanatarajia kumaliza ujenzi katika kipindi kilichopangwa.

Kaimu Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora Akwilin Mwachali alisema hivi wanakwenda kwa kasi baada ya kuvunja mkataba na baadhi ya mafundi wa awali na kukabidhi shughuli kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Alisema mafundi wa awali walikuwa wakifanyakazi pole pole na wakati mwingine wakishindwa kufika kazini kwa visingizio mbalimbali na ndio waliona wachukue hatua ya kusitisha mkataba ili waweze kumaliza kazi hiyo kwa wakati.

Mkazi wa Ilalansimba wilayani Uyui John Kulwa ameishukuru serikali kwa kuwajengea Hospitali ya Wilaya kwa kuwa imesaidia kutokwenda mbali kufuata huduma za ngazi ya Hospitali ya Wilaya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...