MKAZI wa Mtoni Mtongani jijini Dar es Salaam Mirajdin Tajdin (32), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka ya  kusafirisha dhahabu bila kuwa na kibali.
Akisoma hati ya mashtaka, Wakili wa Serikali Ester Martin amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega, kuwa,  Wakili Martin alidai kuwa, April 30, 2019 huko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, (JNIA) mshtakiwa alikutwa na vipande vya dhahabu vyenye uzito wa gramu 98, vikiwa na thamani ya USD  3636.92, sawa na Sh 8, 364,914 Mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo,  mshtakiwa alikutwa akisafirisha dhahabu hiyo bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka husika.
Mshtakiwa amekiri kutenda makosa hayo lakini amerudishwa rumànde kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo mahakama imemtaka mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka Serikali ya Mtaa, atakayesaini bondi ya Sh.milioni nane.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na kesi hiyo itatajwa Julai 4, mwaka huu kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...