Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

WAFANYABIASHARA wawili pamoja na Mkuu wa Kitengo cha mauzo cha Ramada Hoteli William Mgatta (36) wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka matatu likiwemo la kujifanya maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na kushawishi rushwa ya Sh. milioni 300.

Mbali na Mgatta washtakiwa wengine ni, ambao Mohammed Abdallah (25) na Daniel Ileme (35) ambao wote kwa pamoja wamesomewa mashtaka yao leo Juni 20,2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde.

Akisoma hati ya mashtaka Wakili wa Serikali, Aneth Mavika amedai kati ya Juni Mosi 2019, na Juni 10, mwaka huu, katika maeneo tofauti tofauti ya Jiji la Dar es Salaam na Arusha, mshitakiwa Abdallah na Ileme wakiwa wafanyabiashara na mshtakiwa Mgatta akiwa Mkuu wa Kitengo cha mauzo cha Ramada hoteli walishawishi rushwa ya Sh. Milioni 300 kutoka kwa Francis Matunda kama kishawishi ili wasimchukulie hatua za kisheria kwa kukataa kuwalipa wafanyakazi wake kiasi cha Sh. Bilioni moja.

Aidha imedawa siku na mahali hapo, washtakiwa hao walikula njama ya kutenda kosa la kujifanya ni watumishi wa umma. Katika shtaka la tatu imedaiwa, Juni10, mwaka huu katika eneo lisilojulikana jijini Dar es Salaam na Arusha washtakiwa hao walijifanya kuwa ni watumishi wa Takukuru huku wakijua kuwa siyo kweli.

Hata hivyo, washtakiwa wamekana kutenda makosa hayo na wamerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ambapo imemtaka kila mshtakiwa kuwa na mdhamini mmoja, kuwalisilisha Sh.Milioni 50 au hati ya mali isiyohamishika ya kiwango hicho cha fedha.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na kesi imeahirishwa hadi Julai 4, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...