Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Modesta Opiyo(aliyevaa mewani) akisikiliza jambo katika kikao cha wadaawa wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi. 
(Picha na Dhillon John na Magreth Kinabo) 
Mhe. Jaji Julius Mallaba wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi akifuatilia jambo kwenye kikao (kulia) ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Devota Kamuzora. 
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Modesta Opiyo(aliyevaa mewani) akisikiliza jambo katika kikao cha wadaawa wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi. Baadhi ya wajumbe wa kikao cha wadaawa wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi wakiwa katika kikao cha kujadili mashauri yatakayosikilizwa kuanzia Juni 24 hadi Julai 31. 

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi( aliyeketi mstari wa pili kulia), Bw. Benjamini Mlimbila akifuatilia kikao cha wadaawa cha kujadili usikilizaji wa mashauri yatakayosikilizwa kuanzia Juni 24 hadi Julai 31. 
…………………….. 

Na Lydia Churi-Mahakama 

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi inatarajia kusikiliza jumla ya mashauri 43 katika kikao maalum (Session) kinachotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 24 Juni mpaka tarehe 31 Julai, mwaka huu jijini Dar es Salaam. 

Hayo yamezungumzwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi Mhe. Issa Maige katika kikao cha Wadaawa kuhusu usikilizwaji wa mashauri hayo kilichowahusisha Majaji, Naibu Wasajili, Mtendaji na wasaidizi wa kumbukumbu na mawakili. 

Mashauri yatakayosikilizwa ni yanayohusu migogoro ya ardhi ambapo yanatarajiwa kusikilizwa na Waheshimiwa Majaji sita wa Mahakama hiyo wakiwemo Jaji Issa Maige, Jaji Dr. Modesta Opiyo, Jaji Julius Mallaba, Jaji Awadh Mohamed na Jaji Salma Maghimbi. 

Pia Mhe. Jaji Issa Maige aliwataka Mawakili kuendelea kujifunza kusajili mashauri kielektroniki; lakini kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mafunzo yanayotolewa na Mahakama hususani yale yanayohusu matumizi ya mfumo wa kielekitroniki wa kusajili mashauri mahakamani (JSDS). 

Awali, Afisa TEHAMA ya Mahakama hiyo Bw. Dhillon John alisema katika kusajili mashauri kwa njia ya kielekitroniki amekuwa akikutana na changamoto ambapo baadhi ya mashauri hukosa taarifa muhimu na sahihi jambo linalosababisha wateja kukosa baadhi ya haki zao. 

Aidha, akifunga kikao hicho, Mhe. Maige aliwashukuru wajumbe wa kikao hicho hususan Mawakili kwa kutoa mchango wao katika kuboresha hali ya usikilizwaji wa mashauri na kuwataka kufika kwa wingi kwenye vikao hivyo pindi wanapotakiwa kufika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...