Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Januari Msofe akisoma hotuba yake kabla ya kukabidhi ripoti tatu za mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya Ufilisi, Sheria ya Ushahidi na Sheria ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga katika Ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Januari Msofe akimkabidhi Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga moja ya ripoti tatu za mapendekezo ya marekebisho ya sheria.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Balozi Augustine Mahiga akiongea na baadhi ya watumishi wa Tume ya kurekebisha Sheria na wageni mbalimbali baada ya kupokea ripoti za mapendekezo ya marekebisho ya sheria.
………………….
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Balozi Augustne Mahiga apokea ripoti tatu za Mapendekezo ya kurekebisha Sheria tatu kutoka Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Wizara ya Katiba na Sheria Jijini Dodoma leo.

Katika makabidhiano hayo Waziri Mahiga amepokea ripoti ya kurekebisha Sheria ya Ufilisi, sheria ya ushahidi na sheria ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro.

Sheria hizo zimeonekana kuwa na mapungufu mbalimbali ikiwemo ulipishwaji wa faini ndogo, lugha ngumu isiyoeleweka kwa urahisi, matumizi yasiyo sahihi ya ardhi ikiwemo usajili wa vijiji kwenye eneo la hifadhi.

Akizungumzia ripoti alizopokea leo Waziri Mahiga amesema katika eneo la utoaji ushahidi Mahakamani ni vizuri kwa sasa Tanzania ikaanza kupokea ushahidi kwa njia ya video ili kurahisisha utoaji wa ushahidi kutoka sehemu mbalimbali pasipo shahidi kuwepo mahakamani na hili linaweza kufanikishwa kwa kushirikiana na Balozi mbalimbali ambazo zinaonekana kuunga mkono utawala wa sheria uliopo nchini kwa kuchangia vifaa na kutoa mafunzo kwa watendaji.

Aidha, Waziri Mahiga aipongeza Tume ya kurekebisha Sheria kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya ya utafiti wa sheria kabla ya kutoa mapendekezo ambayo yanawezesha sheria mbalimbali kurekebishwa na kuendana na wakati kwani sheria nyingi zinaonekana kupitwa na wakati
Pia Waziri Mahiga amesifu utawala wa sheria uliopo nchini ambao Tume ya Kurekebisha Sheria imesaidia uwepo wa Utawala huo, amesema “ Utawala wa Sheria ili uwe halisi ni vizuri kuwa na Tume
ambayo inapitia na kufanyia tafiti sheria mbalimbali”.

Awali kabla ya kumkabidhi ripoti hizo Waziri Mahiga, Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania Mhe. Januari Msofe alielezea majukumu ya Tume ikiwemo kufanya mapitio na kutoa mapendekezo namna ya kuziboresha sheria mbalimbali ili ziendane na wakati.

Alisema sheria nyingi zimepitwa na wakati na hivyo Taasisi mbalimbali za Serikali zinazosimamia sheria husika huiomba Tume hiyo kuzipitia na wao baada ya kuzifanyia utafiti na kubaini mapungufu hutoa mapendekezo ambayo huyawasilisha Serikalini na baadae Bungeni kwa ajili ya kupitishwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...