Anaandika Abdullatif Yunus - Michuzi TV Kagera.
                  
 Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Gen. Marco Gaguti amekabidhi vifaa vya Ujenzi vyenye Thamani ya Sh. Milioni Mbili kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi, ikiwa ni kuunga mkono Juhudi zinazofanywa na Jeshi la Polisi Mkoani Kagera.       

Vifaa hivyo ambavyo ni bati na saruji, vimekabidhiwa mapema 13, Juni wakati ambapo Rc Gaguti akiwa njiani kuelekea Katika Ziara yake ya kikazi Wilayani Kyerwa,  ambapo pamoja na mambo mengine, Rc Gaguti amepongeza juhudi zinazofanywa na jeshi la Polisi Mkoani Kagera kwa jinsi wanavyoendelea kupambana na uhalifu wa kila aina, na kuendelea kutunza amani ya Nchi na Mipaka yake, hivyo Serikali ya Mkoa iko tayari kuhakikisha askari wanaishi katika mazingira bora.
 Pichani ni majengo ya Nyumba za Askari Polisi zinazojengwa eneo la Rwamishenye Manispaa ya Bukoba, Jumla ya nyumba Tatu zenye uwezo wa kubeba familia sita.
 Pichani Rc Gaguti akizungumza na maafsa wa Polisi Mara baada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi kama juhudi za kuunga mkono kile kinachofanywa na Jeshi hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...