Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu Rukia Ally, (18) kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kukiri kosa la kumuua bila ya kukusudia kaka yake wa tumbo moja.

Mshtakiwa, mapema mahakamani hapo alisomewa kosa la mauaji ya kukusudia na kulikana lakini upande wa mashtaka ulidai kuwa kutokana na ushahidi walionao waliomba kubadirisha hati ya mashtaka na mshtakiwa huyo akasomewa kosa la kuua bila kukusudia ambapo amekiri kosa hilo na ndipo akakumbushwa shtaka lake.

Akisoma Hukumu hiyo, Msajili wa Mahakama Kuu Pamela Mazengo amesema, mahakama imemkuta mshtakiwa na hatia na inamuhukumu kutumikia kifungo cha miaka mitatu gerezani.

Awali mshtakiwa hiyo alikuwa akikabiliwa na shtaka la mauaji ya kukusudia lakini kufuatia ushahidi uliopokelewa na upande wa mashtaka, wameona kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kosa la mauaji ya bila kukusudia.

Akimsomea upya shtaka lake, Wakili wa serikali Mwasiti Ally, amedai, Januari 23,2015 huko Mivumoni eneo la Madale, katika Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa bila ya kukusudia alimuua kaka yake Said Ally.

Hats hivyo, kabla ya kusomewa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Mwasiti Ally, alimsomea mshtakiwa Maelezo ambapo alidai:

Marehemu alikuwa ndugu wa damu na mshtakiwa na wote walikuwa wakiishi na wazazi wao huko Mivumoni Madale ambapi Siku ya tukio majira ya jioni marehemu alirudi nyumbani kwao na kumkuta dada yake (mshtakiwa), ambae aliondoka nyumbani hapo kwa siku tatu bila kuonekana akiwa chumbani kwake.

Ameeleza kuwa, marehemu alimgongea mlango mshtakiwa (dada yake) chumbani humo na akamfungulia mlango na kutoka nje ambapo alimuuliza siku tatu zilizopita alikuwa wapi lakini hakumjibu kitu kitendo ambacho kilipelekea marehemu kukerwa na kwa kuwa alikuwa ameshika fimbo alianza kumchapa Mshtakiwa miguuni.

Ameendelea kueleza kuwa, wakati tukio hill linatokea marehemu alikuwa ameshikilia kisu mkononi, hivyo Mshtakiwa akampokonya na bahati mbaya akakumchoma nacho kifuani upande wa kushoto ndipo marehemu akadondoka chini huku damu nyingi zikimtoka huku mshtakiwa akakimbia

Mama wa marehemu baada ya kusikia purukushani ile alitoka na kwenda kumsaidia marehemu kwa kuomba msaada kwa majirani pamoja na ndugu ambapo baada ya hapo walienda polisi kutoa taarifa ndipo wakampeleka Hosp. Lakini walipofika wakathibitishiwa kuwa alikuwa amekwishafariki na walielezwa kuwa sababu ya kifo cha marehemu ni kutokwa na damu nyingi kulikosababishwa na kuchomwa kisu.

Ameeleza kuwa, Mshtakiwa baada ya kukamatwa alipelekwa kwa mlinzi wa amani mahakamani ya Mwanzo Kawe.Mshtakiwa kabla ya kusomewa adhabu yake, amekiri kuwa hivyo ndivyo ilovyotokea. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...