Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiwasha umeme katika moja ya
saloni za kiume katika kijiji cha Nyange wilayani Kibondo mkoani Kigoma
alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini( REA) 
Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu( mwenye kilemba cheusi) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Lois Peter Bura (mwenye Kaunda suti) mara baada ya kuwasha umeme katika kijiji cha Nyange na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa usambazaji umeme vijijini( REA) katika wilaya hiyo.

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu( kushoto) akiteta jambo na Meneja
wa Shirika la Umeme mkoani Kigoma, Mhandisi Masingija Lugata(kulia)
wakati wa mkutano na wananchi wa kijiji cha Nyange hawapo
pichani,Naibu Waziri alifika kijijini hapo kuwasha umeme na kukagua
maendeleo mradi wa usambazaji umeme vijijini( REA).
Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Lois Peter Bura, akizungumza na wananchi
wa Kijiji cha Nyange hawapo pichani wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa
Nishati ya kukagua utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme katika
Wilaya ya Kibondo na kuwasha umeme katika kijiji cha Nyange. 



Na Zuena Msuya, Kigoma 


Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu,amesema haridhishwi na kasi ya
usambazaji wa umeme vijijini inayofanywa na mkandarasi wa Kampuni ya
Urban and Rural Engineering Services, wilayani Kibondo mkoani Kigoma. 

Mgalu ametoa kauli hiyo,kwenye mkutano na wananchi wakati alipofanya
ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini wilayani
humo na kuwasha umeme katika kijiji cha Nyange. 

Mgalu alisema kuwa, mkandarasi huyo amekuwa akitekeleza mradi huo
kwa kusuasua na hivyo kusababisha hofu kwa wananchi pamoja na
kuwakatisha tamaa kuwa huenda mradi huo usikamilike licha ya wananchi
hao kujiandaa kuupokea. 

Hata hivyo Mgalu aliongeza kuwa, mkandasi huyo tayari alikwisha lipwa
fedha zake ili kutekeleza mradi huo na kwamba endapo atashindwa
kutekeleza kwa muda uliopangwa basi sheria itachukuwa mkondo wake
kulingana na mkataba. Sambamba na hilo amemtaka mkandarasi huyo kuwepo eneo la mradi muda wote,pia kuongeza nguvu kazi katika kutekeleza mradi huo. 

Alifafanua kuwa Mkandarasi huyo anatakiwa kukamilisha mradi huo ifikapo mwezi Juni mwaka 2020 kwa kuunganisha vijiji 40 katika wilaya ya
Kibondo vilivyo umbali wa kilometa 283, lakini mpaka sasa ameunganisha
vijiji 3 tu, na kusimamisha nguzo umbali wa kilometa 90 zililovutwa nyaya
umbali wa kilometa 50 tu. 

“Kasi ya mkadarasi huyu katika kutekeleza mradi wa usambazaji wa
umeme vijijini hapa Kibondo hairidhishi kabisa, idadi ya vijiji vilivypo na
vilivyounganishwa ndogo mno,pia anafanya kazi kwa kusuasua na
akiendelea hivi serikali haitamvumilia itafanya maamuzi magumu, tunataka
wananchi wote wapate umeme kwa wakati, fedha alishalipwa,” Alisisitiza
Mgalu. 

Mbali ya kuwepo kwa changamoto hiyo, Mgalu aliwatoa hofu wananchi kwa
kuwataka kutokata tamaa na kwamba waendelee kusuka nyaya katika
nyumba zao kwakuwa mradi huo utatekelezwa kama ulivyopangwa wote
wataunganishiwa umeme. 

Pia aliwasisitiza kuwa malipo ya kuunganisha umeme katika nyumba zao ni
shilingi 27,000 tu na wasikubali kulipa zaidi na endapo itatokea mtu anadai
fedha zaidi basi watoe taarifa sehemu husika ili watu hao waweze
kushughulikiwa.Vilevile wananchi hao wasikubali kuuziwa vifaa vya umeme kama vilenguzo pamoja LUKU kwa kuwa vifaa hivyo hutolewa bure kwa wananchiwote. 

Kwa upande wake Meneja mradi wa kampuni ya ukandarasi ya Urban and
Rural Engineering Services, amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na
kueleza sababu kubwa ilikuwa ni kukwama kwa vifaa bandarini. 


Hata hivyo amesema kuwa sasa wamepata suluhisho hivyo muda wowote
vifaa hivyo vitafika katika eneo la mradi na watanzaa kufanya kazi usiku na
mchana kufidia muda waliopoteza. Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Lois Peter Bura, amewataka wananchiwa Kibondo kuendelea kuilinda miundominu ya umeme iliyopo katikamaeneo yao na kwamba mradi huo utatekelezwa kulingana na mkataba. 


Vilevile amemtaka mkandarasi kushirikiana na ofisi ya Wilaya na kueleza
pale walipokwama ili kutatua changamoto zilizopo kwa manufaa ya
wananchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...