NJOMBE


Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA kimesema kinakwenda mahakamani kupinda utaratibu uliyotumika kumvua ubunge aliyekuwa mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Antipas Lissu ambaye yupo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu .

Siku kadhaa zimepita tangu Spika wa bunge atangaze bunge kuvuliwa ubunge kwa Lissu kwa sababu ya kutojaza fomu ya maadili na utoro wa vikao vya bunge kwa zaidi ya miezi kumi sasa jambo ambalo limeibua hisia tofauti kwa wanasiasa na watanzania kwa kuwa inafahamika kuwa mbunge huyo yupo nje kwa matibabu baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana mwaka jana katika eneo la eria D jijini Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mboye ambaye amewasiri mkoani Njombe akitokea Songwe ukiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya mikutano ya ndani katika mikoa ya kanda ya Nyasa mkurugenzi wa itifaki, mawasiliano na mambo ya nje wa chama John Mlema amesema chama kinaendelea na mikutano ya ndani ambayo imebebwa na agenda kuu tatu ikiwemo ya ya kuvuliwa ubunge kwa Lissu na kudai mapema baada ya mikutano hiyo chama kitafungua kesi ya kupinga kuvuliwa ubunge huo.

Agenda nyingine ambazo zimewekwa bayana katika ziara ya Mboye katika kanda ya Nyasa ni pamoja uchaguzi wa serikali za mitaa,kuwashukuru viongozi na wana chama kwa kazi kubwa waliyofanya wakati akiwa mahabusu kwa zaidi ya miezi minne huku agenda nyingine kubwa ikiwa ni kutoa ufafanuzi wa sheria mpya ya vyama vya siasa ambayo imeonyesha kubadili kwa kiasi kikubwa utendaji wa vyama nchini.

Nao baadhi ya viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo Rose Mayemba kiongozi wa chadema msingi na Alatanga Nyagawa ambaye ni katibu wa mkoa wakifafanua jitihada ambazo wamezichukua katika kuimarisha chama wamesema wameanza kuandikisha wanachama katika daftari la maalumu la A3 kuanzia ngazi ya chini na kwamba wanatanzania wategemee chama hicho kupata ushindi mkubwa kwa kuwa kimejihimarisha katika utunzaji wa taarifa.

Katika ziara hiyo Mboye ambayo amekagua na ujenzi wa jengo la ofisi za chama ameongozana na mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa na mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi huku kesho akitegemea kuhitimisha ziara yake katika mkoa wa Iringa na kukamilisha ziara ya kanda ya Nyasa yenye mikoa ya Mbeya,Rukwa,Songwe,Iringa na Njombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...