Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Kiongozi wa Mradi, Richard Magwizi, wakati akikagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. Katikati ni Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akikagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na wananchi, baada ya kukagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizungumza na viongozi pamoja na watumishi wa Wilaya ya Mwanga, katika ukumbi wa Green Bird, wilayani hapo, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akisalimiana na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso, wakati alipowasili kukagua mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) na kuongea na wananchi, katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia mashine za kusukumia maji, kwenye mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiangalia chanzo cha maji, katika mradi wa maji wa Same, Mwanga, Korogwe (SMK) ,uliyopo katika kijiji cha Kinya-Nyumba ya Mungu, Julai 20.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 

…………………………………………………. 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe ulioko Kirya, wilayani Mwanga, na kukagua hatua mbalimbali za ujenzi wa mradi huo. 

Waziri Mkuu amekagua ujenzi huo jana (Jumamosi, Julai 20, 2019) na kutoa maelekezo kadhaa ili kuharakisha ujenzi wa mradi ambao umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu sasa. 

Akizungumza na wakazi wa Kirya, Nyumba ya Mungu na vijiji vilivyo jirani na eneo la mradi, Waziri Mkuu alisema Serikali itaendelea kutoa fedha hatua kwa hatua ili kukamilisha mradi huo. 

Waziri Mkuu amewataka wakazi hao waache kutumia uvuvi haramu na badala yake, wavue samaki kwa kutumia njia halali. “Bwawa la Nyumba ya Mungu linagusa wilaya tatu za Mwanga, Simanjiro na Moshi Vijijini. Ninataka Serikali za wilaya husika zisimamie jambo hilo,” alisisitiza. 

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemwagiza Afisa Elimu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Bibi Pauline Nkwama amsimamie Afisa Elimu wa Wilaya hiyo anayeshughulikia elimu ya msingi, Bibi Mariana Mgonja na kuhakikisha kuwa anawahamishia walimu kwenye shule mbili za Kirya ambazo zilikuwa na walimu wawili wakati zina wanafunzi zaidi ya 400 kila moja. 

“Afisa Elimu Mkoa hakikisha Afisa Elimu wa elimu ya msingi katika wilaya hii anahamisha walimu kutoka pale mjini na kuwaleta huku ili huku vijijini kuwe na walimu sita katika kila shule. Kesho Jumapili (leo) andika barua za uhamisho, Jumatatu wapewe ili Jumanne waje kuripoti huku,” alisema. 

Alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mwanga, Bw. Zephrin Lubuva awatafutie gari walimu watakaohamishiwa huko ili wafike mapema. 

Amechukua hatua hiyo, baada ya kuelelezwa na mbunge wa jimno hilo, Profesa Jumanne Maghembe kwamba katika eneo hilo kuna shule mbili ambazo zina walimu wawili wakati kuna madarasa nane, yaani la awali moja na ya msingi saba, na wanafunzi zaidi ya 400. Alizitaja shule hizo kuwa ni Kiti cha Mungu na Emangulai. 

Mapema, akitoa taarifa kuhusu mradi huo, msimamizi wa mradi huo Mhandisi Richard Magwizi alimweleza Waziri Mkuu kwamba Serikali inatekeleza mradi huo ili kuondoa kero ya maji inayowakabili wakazi wa miji ya Same na Mwanga na vijiji 38 vilivyo katika eneo la mradi. 

Alisema mradi huo utakapokamilika, unatarajiwa kunufaisha wananchi 438,931 katika Wilaya za Same (246,793), Mwanga (177,085) na Korogwe (15,053). Alisema mradi huo umegawanywa katika awamu mbili za utekelezaji na unakadiriwa kugharimu dola za Marekani milioni 300. 

“Awamu ya kwanza inahusisha ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji wa maji safi na kusambaza maji kwa wakazi wa Mji wa Same na Mji wa Mwanga na vijiji 9 vilivyo kandokando ya chanzo cha maji ambapo awamu ya pili itahusisha ujenzi wa miundombinu ya usambazaji wa maji katika vijiji 29,” alisema. 

Akielezea changamoto zinazowakabili, Mhandisi huyo alisema wana changamoto ya kuchelewa kwa malipo ya mkandarasi kutokana na uwiano wa uchangiaji ambapo Serikali inagharimia asilimia 50.18. “Malipo yanapochelewa, yanaathiri kasi ya utekelezaji,” alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...