Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni wakiapata maelekezo kuhusu ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kutoka kwa Meneja wa Jengo hilo, Mhandisi Burton Komba

 Mabalozi wa Tanzania kutoka nchi mbalimbali Ulimwenguni wakiwasili katika Jengo la Tatu la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam na kupokewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Mhandisi Julius Ndyamukama na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mhandisi Patrick Mfugale wakati wa ziara yao ya kikazi katika miradi mbalimbali ya maendeleo nchini.




Mabalozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wilbroad Slaa na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza, Dkt. Asha-Rose Migiro wakisikiliza maelekeo ya Jengo la Tatu la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MABALOZI wa Tanzania katika nchi mbalimbali wamesifu juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwenye ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Mabalozi hao wametoa sifa hizo wakati wa ziara yao ya kikazi katika Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayoratibiwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Balozi wa Tanzania nchini India, Baraka Luvanda ambaye hivi karibuni Shirika la Ndege nchini (ATCL) imezindua safari zake nchini humo, amesema Jengo hilo la Tatu la Abiria linatuleta katika sura mpya ya Kimataifa na kututambulisha.

Balozi Luvanda amesema Wajumbe mbalimbali wa Mkutano wa Nchi wa Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wataondoka na sura nyingine ya kimaendeleo katika Taifa la Tanzania, amesema Uwanja huo umefunguliwa muda mwafaka na maboresho yanayoendelea kufanyika yataiweka Tanzania katika Ramani ya Dunia kwa inavyostahili.


"Kwanza ujio wa ATCL (Dream Liner) nchini India kutoka Dar es Salaam umepunguza muda wa safari, kulikuwa na Wagonjwa wanakuja India lakini wengine walikuwa watunia masaa 13 au 14 kwa sababu ya umbali, lakinj kwa sasa wanatumia masaa matano tu kufika Mumbai", amesema Balozi Luvanda.

Amesema atatumia fursa hiyo kuutangaza Uwanja huo nchini India kutokana na uwezo wake wakuchukua idadi kubwa ya abiria kwa mwaka ambao ni Milioni 6, ameahidi kutangaza ili kupata idadi kubwa ya Ndege na Mashirika mbalimbali.

Kwa upande wake, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dkt. Abdallah Posi amesema miradi hiyo ni muhimu kwa wageni wanaoingia nchini, amesema Ujenzi wa Jengo hilo utarahisisha usafiri kwa watu wa mataifa mbalimbali wanaoingia nchini, Dkt. Posi amesema anaona mafanikio makubwa zaidi kwa utofauti uliopo kati ya Jengo hilo la Tatu la Abiria pamoja na Jengo la Kwanza na la Pili la Uwanja wa Ndege.

"Wengi wetu tumefurahishwa sana na utekelezaji wa miradi hii, kwa yale tunayoyaona huko nje ni mafanikio, walichotuzidi wenzetu labda wao wana hela nyingi", amesema Dkt. Posi.

Naye, Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Dkt. Wibroad Slaa ametoa wito kwa Mabalozi hao kuitangaza zaidi Tanzania Kimataifa, amewataka kutoa woga katika kulitangaza Taifa katika maendeleo yanayofanyika chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

"Tusiogope kuitangaza Tanzania Kimataifa kama tunaendelea katika miradi mablimbali, wenzetu huko wanatumia sana Pesa katika masuala mbalimbali ikiwemo miradi ya ujenzi", amesema Dkt. Slaa.

Mabalozi hao wapatao 42 wametembelea Miradi mbalimbali ya Serikali ikiwemo Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Standard Gauge, Ujenzi wa Daraja la Surrender na Ujenzi wa Interchange ya Ubungo inayosimamiwa na Serikali Kuu ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...