Msajili Mkuu-Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati (katikati) akizungumza na Wasaidizi wapya wa Sheria wa Majaji wa Mahakama ya Rufani (T) (hawapo pichani), wa pili kushoto ni Naibu Msajili Mwandamizi-Mahakama ya Rufani, Mhe. Elizabeth Mkwizu, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo-Mahakama ya Tanzania, Bi. Patricia Ngungulu, wa kwanza kulia ni Afisa Utumishi/Msaidizi wa Mtendaji-Mahakama ya Rufani, Bi. Vivienne Kishimbo na wa pili kulia ni Hakimu Mkazi na Msaidizi wa Msajili Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Upendo Ngitiri. 
Mhe. Mkwizu akiwaonyesha Maafisa hao Ofisi ya Mapokezi ya Mahakama ya Rufani.

Na Mary Gwera, Mahakama
JUMLA ya Wasaidizi wa Sheria 21 wa Majaji wa Mahakama ya Rufani (T) walioteuliwa hivi karibuni wamepatiwa utangulizi wa masuala muhimu ya kuzingatia katika ufanyaji kazi kwenye Mahakama hiyo.

Akizungumza na Maafisa hao mapema Agosti 15, 2019 katika Ukumbi ya Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Katarina Revocati amewaasa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Mahakama imewaamini, hivyo basi ni vyema mkafanye kazi kwa uadilifu na unyenyekevu,” alieleza Msajili Mkuu.

Mbali na masuala hayo, Mhe. Revocati aliongeza kwa kuwataka Maafisa hao kutojihusisha na vitendo vya upokeaji wa rushwa wanapotekeleza majukumu yao.

“Siku hizi hakuna rushwa isiyojulikana pindi unapojihusisha katika vitendo hivi utajulikana tu, hivyo ni vyema kutojihusisha ili kuwa salama,” alisisitiza Mhe. Revocati.

Wasaidizi hao wa Sheria ambao kwa taaluma ni Mahakimu wameteuliwa kutoka Mahakama mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuwasaidia Waheshimiwa Majaji katika kufanya tafiti ambazo zitawawezesha katika utoaji wa maamuzi ya rufaa mbalimbali.

Kabla ya kuanza kazi rasmi Maafisa hao watapatiwa Mafunzo elekezi yatakayowawezesha kuwapa kwa kina misingi ya ufanyaji kazi katika Mahakama hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...