MAWAKILI wa upande wa Mashtaka na wa utetezi katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi wa Chadema akiwemo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe wamejikuta wakirushiana maneno mahakamani kufuatia kitendo cha wakili wa utetezi, Hekima Mwasipo kunyanyuka mahali alipokuwa amekaa na kwenda kumchungulia shahidi mahali alipokuwa amekaketi wakati akitoa ushahidi wake.

Baada ya kuona kitendo hicho, wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliyekuwa akimuongoza shahidi huyo, alitoa taarifa kwa Hakimu

Mkazi Mkuu Thomas Simba juu ya tukio hilo akidai kuwa mawakili wa utetezi wanamtisha shahidi ambapo, wakili Peter Kibatala alidai walidhani shahidi huyo anasoma ushahidi wake kwenye simu ndio maana akaenda kumchungulia huku wakili Matata akihama mahali alipokuwa amekaa na kwenda kukaa karibu na kizimba cha shahidi kutolea ushahidi wake.

Baada ya wakili Wankyo kudai hayo, Wakili wa utetezi Peter Kibatala alisimama na kutaka kutoa maelezo lakini wakili wa Serikali Faraja Nchimbi alionekana kutokubaliana na hilo na kuwafanya wrote kuanza kurushiana maneno hali iliyopelekea Hakimu kumuita askari aliyekuwa mahakamani hapo na kuwaambia mawakili hao "Nitaagiza askari awakamate" 

Hata hivyo, Hakimu Simba alifanikiwa kumaliza vurugu hiyo kwa kuwataka mawakili wote kukaa kimya na kumuonya Mwasipo kuwa haruhusiwi kusimama mahakamani bila ruhusa ya mahakama na Mwasipo akaomba msamaha. 

Hata hivyo, shahidi alilazimika kutoka kwenye kizimba na askari polisi aliamuriwa kumkagua shahidi na kukagua sehemu alipokuwa amekaa kama kuna simu au kitu chochote.

Askari polisi aliiambia mahakama kuwa hakuna kitu chochote na hivyo shahidi alirudi na anaendelea kutoa ushahidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...