Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

MKURUGENZI Mkuu wa bank M nchini Tanzania, Sanjeev Kumar (64) amehukumiwa kulipa faini ya sh.milioni mbili baada ya mahakama kumtia hatiani katika mashtaka mawili yaliyokuwa yakimkabili likiwemo la kuisababishia serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hasara ya zaidi ya sh. Bilioni sita.

Pia mahakama imemuamuru mshtakiwa huyo kulipa fidia ya sh. 6,039,103,579 ambazo anatakiwa kumaliza kuzilipa ndani ya miezi ishirini na nne.  ambapo leo Oktoba 8/2019 amemriwa kulipa USD,300,000 ambazo ni sawa na zaidi ya sh. Milioni 690  na amezilipa.

Akisoma adhabu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi amesema, mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya sh. Milioni moja kwenye kila kosa na kulipa fidia ya sh. 6,039,103,579.Akifafanua adhabu hizo, Hakimu Shaidi amesema, mshtakiwa anapaswa kulipa USD 300,000 leo leo na pia fedha itakayobaki inapaswa kulipwa katika kipindi cha miezi 24 kuanzia tarehe ya leo (8/10/2019) na fedha zinazobaki kiasi cha sh. 5,349,103,579 anapaswa kila mwezi kulipa sh. 222 ,879,315 ambazo anatakiwa kulipa kabla aka tarehe 8 ya Kalenda ya kila mwezi mpaka atakapomaliza..

Pia mahakama imeamurui hati ya kusafiria ya mshtakiwa huyo ibaki katika Ofisi za DPP  na safari zake zote zitafatiliwa na ofisi hiyo. 

Kabla ya kusomwa kwa adhabu hiyo, Wakili wa serikali Jackiline Nyantori  alidai, hawana kumbukumbu za nyuma za mshtakiwa hivyo, ameiomba mahakama itoe adhabu kulingana na makubaliano ili iwe  fundisho kwake na  wengine.

Akisoma makubaliano hayo, Wakili Nyantori amedai, DPP na mshtakiwa  wameingia makubaliano baada ya kukiri makosa yake hivyo wameamua kuondoa mashtaka ya  kughushi,  ya kutakatisha fedha, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Baada ya kusoma makubaliano hayo, Hakimu Shaidi  alimuapisha mshtakiwa na kumuuliza  kama alisaini kwa hiari yake na kudai alifanya hivyo kwa hiari yake.

Akisoma mashitaka mapya, Wakili Nyantoru alidai katika shtaka la kwanza, Januari 20,2016 mshtakiwa hiyo akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki M Tanzania alishindwa kusimamia majukumu yake vizuri na kuisababishia Serikali kupata hasara ya Sh. 6, 039, 103,579.

Katika shtaka la pili,  imedaiwa, siku na mahali hapo mshtakiwa Kumar, akiwa kwa njia ya ulaghai ndani ya Benki M Tanzania na huku akijia akijua kuwa ni udanganyifu alijipatia USD  287,000.
 MKURUGENZI Mkuu wa bank M nchini Tanzania, Sanjeev Kumar (64) amehukumiwa kulipa faini ya sh.milioni mbili baada ya mahakama kumtia hatiani 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...