Na Agrey Evarist -Morogoro.

Bodi ya nyama nchini yafungia eneo linalotumika kama mauzio ya mazao ya mifugo katika manispaa ya morogoro na kutoa onyo kali kwa watakao endelea kufanya shughuli hiyo.

Bodi hiyo ya nyama iliyokua ikiongozwa na  imani sichwale kaimu msajili wa bodi ya nyama wamefika katika eneo maarufu kwa kuuza mazao ya mifugo kama miguu ya n'gombe (kongoro), mikia sambambana vichwa lililopo karibu na machinjio ya nyama ya morogoro ambapoa akabainisha eneo hilo si rasimi na wakaamua kulifunga ili kutoendelea kwa biashara hiyo.

Akielezea sababu za kufunga eneo hilo kaimu msajili wa bodi ya nyama tanzania imani sichwale ameeleza serikali ilishapiga marufuku uuzaji wa nyama maeneo ya wazi kwakua kuna uwezekano mkubwa wa kutokea magonjwa ya mlipuko kama kipindu pindu kutokana na inzi kuruka hovyo hivyo si vyema biashara hii kufanyika kiholela.

  "kuna kanuni na sheria ya nyama ya 10 ya mwaka 2006 inayo jieleza wazi na kupinga uuzaji wa nyama katika maeneo ya wazi'' alisema kaimu huyo,hata hivyo anabainisha tayari walisha mwandikia mkurugenzi wa manspaa ya morogoro juu ya kufungwa kwa eneo hilo na kubainisha kwamuda mrefu eneo hilo limekuwa likisababisha wananchi kulishwa nyama ya wanyama ambao tayari wamekufa (vibudu) kutokana na kutokua na usimamizi wa kutosha kukagua nyama inayouzwa katika eneo hilo.

''mkoa wa morogoro umekuwa na uwizi mkubwa wa mifugo na wezi wa mifugo wengi wamekuwa wakijificha katika eneo hili kwa kuchinja nyama kiholela za wizi porini na kuja kuuzia katika maeneo haya hivyo kufungwa kwake kutapunguza wizi wa mifugo mkoani hapa''

Kwa upande wake daktari wa mifugo wa manspaa ya morogoro peter lema akabainisha soko hilo limekuwa kero kwa muda mrefu na tayri walisha mwandikia barua mmiliki wa eneo hilo bila mafanikio hivyo wanaipongeza bodi ya nyama kwa kuweka nguvu katika swala hilo.

Kwa upande wao wafanyabiashara wa nyama katika eneo hilo wakiongozwa na mwenyekiti wao abedi makonya wameeleza eneo hilo kwa muda wamekuwa wakifanya biashara zao bila matatizo huku wakieleza wanachouza si nyama bali ni mazao ya nyama ambayo si rahisi kuuziwa buchani.

''unakuta unaenda buchani kununua nyama lakini unataka na mkia au kongoro, buchani huwezi washa moto ukaanza kwangua miguu ndio maana huwa tunakuja kuchomea huku hivyo serikali inapo fanya maamuzi yake iangalie na watu kama sisi alisema mmoja ya wafanyabiashara hao''

Latifa Ramadhani naye ni mjasiriamali anayejusisha na mama lishe amebainisha wao wanaendesha maisha yao kwa kutumia eneo hilo kununua baadhi ya mazao hayo ya mifugo kama utumbo  kupika  na kuuza chakula hivyo nao wakaiomba serikali kuandaa eneo lingine kwaajili ya kufanyia shughuli zao.
  Baadhi ya vifaa vinavyo tumika katika kukata na kusafishia mazao ya mifugo
 Baadhi ya uchafu wa kwato uliotupwa kiholela katika eneo maarufu kwa uuzwaji wa mazao ya mifugo katika kanispaa ya morogoro.

 Baadhi ya vifaa vinavyo tumika katika kukata na kusafishia mazao ya mifugo
Kaimu Msajili wa bodi ya nyama Tanzania Imani Sichwale akionyesha tangazo lililo amuru kufungwa kwa eneo la uuzwaji wa mazao ya mifugo ambalo lilipuuzwa.
Muonekano wa eneo la uuzwaji wa mazao ya mifugo kama miguu vichwa na mkia.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...