Askari Polisi watatu wamefariki dunia na wengine tisa wamejeruhiwa baada ya gari dogo la polisi walilokuwa wakisafiria kwenda lindoni kugongana na basi la abiria la Sharom lenye namba za usajili T 349 CXB ambalo hufanya safari zake za Njombe kwenda Arusha na gari la polisi lenye namba za usajili TP 3437 land cluzer.

Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 12 asubuhi katika daraja la Mto Ruhiji mjini Njombe ambapo majeruhi wamepelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Akizungumzia ajali hiyo Mganga Mfawidhi Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe, Kibena Alto Mtega amesema imehusisha watu 12, na majeruhi hao wameanza kutibiwa.


Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issa amesema kuwa ajali hiyo imeokea Mkoani Njombe katika Mteremko unaoelekea katika Kituo cha Polisi Mkoani humo na kuligonga gari la Polisi.

Issa amesema kuwa basi la abiria liligonga gari la Polisi ambalo lilikuwa linaenda na polisi hao katika maeneo mbalimbali ya lindo.

"Kilichotokea basi hilo liligonga bodi ya gari ambalo polisi walikuwa wamebebwa, na bodi la gari liling'oka na kufumuka na kusababisha majeruhi kwa Askari waliokuwa nyuma ya hilo bodi". Amesema Issa.


Amesema kuwa nyuma ya bodi kulikuwa na Askari 11 ambao ni majeruhi na wamepelekwa katika hospitali ya Kibena na Askari watatu wakafariki dunia kabla ya kupata matibabu.

"Askali walio fariki dunia ni Askari namba H 4401 huyu anaitwa Malharusi Saidi Khamis Mkazi wa Lindi na Mwingine ni H 6802 PC, Michael Mwandu Mkazi wa Geita na Askari Mwingine ni H 7486 PC, Henry Athumani Soka huyu anaukazi wa Arusha na Kilimanajaro".Amesema Issa.

Katika tukio hilo Askari Henry  Athumani Soka utata umejitokeza na hawajapata usahihi ni wapi atapelekwa ingawa inaonyesha kwao ni Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha.

Amesema kuwa Askari Polisi watano walikuwa wamezidiwa sana mmoja aliyejulikana kwa jina la kijeshi la H 1839 amepata maumivu ya shingo na maumivu mengine ya mwili na amepewa rufaa ya kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwani hawezi kupanda gari labda usafiri wa ndege.

Issa amesema kuwa kwa sasa wanafanya utaratibu Askari huyo aweze kusafirishwa na kupelekwa Muhimbili MOI kwa matibabu na taratibu zote za kumsafirisha zimekamilika.

"Askari wengine kwa mujibu wa madaktari Askari hao wanne waliobaki wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Kibena na  kati ya Askari hao wanne,  wawili walitoka ngozi ya usoni na kwenda nyuma ya kichwa,lakini tunashukuru Madaktari wamefanya kazi yao vizuri ya kuwatibu hao na wanaendelea vizuri mpaka sasa".

Dereva wa basi la abiria ambalo liligonga gari la Polisi amekimbia, lakini mmiliki wa basi hilo amekamatwa kwa ajili ya kumhoji kuhusu taarifa na anuani halisi za dereva wa basi hilo lililokuwa likitokea Njombe kwenda Arusha.

Kamanda Issa amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi la kampuni ya Sharom.

Hata hivyo amewashauri madereva wa magari ya abiri wakipita mkoa wa njombe wapunguze mwendo kasi hasa katika eneo la mteremko ambapo imetokea ajali leo kwani ni mteremko mkali na wanatakiwa kuchukua tahadhali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...