Charles James, Michuzi TV

WANANCHI nchini wameaswa kuacha tabia ya kula nyama zinazochinjwa kwenye machinjio rasmi ili kujiepusha na magonjwa yanayotokana na mifugo ikiwemo ugonjwa wa Brucelosis unaosababisha mimba kutoka.

Akizungumza wakati wa operesheni maalumu ya kukagua hali ya machinjio jijini Dodoma, Daktari wa Mifugo kutoka Wizara ya Afya, Meljory Malick amesema ipo mifugo ambayo ina magonjwa kama Kifua Kikuu, Kimeta na Bonde la Ufa.

Dk Mariki amesema jamii inashindwa kutambua umuhimu wa kupima wanyama kabla ya kuchinjwa kwani inasaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa hayo ambayo dalili zake hutokea baada ya mwezi mmoja au miwili.

Kwa upande wa Afisa Usajili wa Bodi ya Nyama Godfrey Kakuru amesema bodi hiyo haitomvumilia mtu yeyote ambaye atavunja sheria kwa kuchinja kwenye machinjio ambazo hazipo kisheria kwani kufanya hivyo kunachangia wimbi la magonjwa mengi yatokanayo na ulaji nyama.

Kakuru amesema katika operesheni waliyoifanya wamekamata zaidi ya wafanyabiashara 25 ambao wamekutwa na makosa mbalimbali ikiwemo uuzaji nyama isiyokubaliwa, usafirishaji wa nyama kwenye viroba na pia kubeba nyama kwenye pikipiki.

" Tukikukamata ukifanya biashara hii kiholela lazima tukuwajibishe. Tutakutoza faini isiyopungua Shilingi 50,000 na isiyozidi Milioni Moja. Lengo ni kuhakikisha wote wanafuata utaratibu, kanuni na sheria za Nchi yetu," Amesema Kakuru.

Naye Kaimu Meneja Mkuu wa machinjio ya Dodoma, Victor Mwita amewatakawafanyabiashara wa nyama kupeleka Ng'ombkwa ajili ya kuchinja katika Machinjio hayo kwa sababu ni salama na yana vigezo vyote badala ya kwenda kuchinjia vichochoroni.

" Toka serikali kupitia kwa Waziri Mpina kutoa agizo la machinjio hii kuendeshwa na serikali tumefanya mabadiliko makubwa ya kimfumo, kununua vifaa vya kazi, kuboresha Usafi, kuzingatia malipo ya wafanyakazi wetu.

Kupitia maboresho hayo tumeweza kuongeza idadi ya mifugo inayoletwa hapa ambapo Ng'ombe kwa sasa tunachinja kati ya 95-120 kutoka 35-50 kwa siku, ongezeko hilo ni sambamba na uchinjaji Mbuzi ambao umefika wastani wa 500-1200 kwa siku," Amesema Mwita.
 Wachinjaji wakiendelea na zoezi la uchinjaji nyama kwenye machinjio ya Dodoma.
 Kaimu Meneja Mkuu wa Machinjio ya Dodoma, Victor Mwita akizungumzia hali ya uchinjaji kwenye machinjio ya Dodoma wakati wa ziara ya Bodi ya Nyama leo.
 Afisa Usajili kutoka Bodi ya Nyama, Godfrey Nakuru akizungumzia operesheni waliyoifanya ya kukamata wafanyabiashara wanaochinja nyama kinyume na sheria.
Daktari wa Mifugo kutoka Wizara ya Afya, Meljory Mariki akizungumza na wandishi wa habari kwenye machinjio ya Dodoma leo.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...