Charles James, Globu ya Jamii

MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amempa siku tatu mchekeshaji, Emmanuel Mgaya 'Masanja' kuripoti Ofisini kwake au Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dodoma.

DC Katambie ametoa agizo hilo kwa Masanja baada ya kusambaa kwa video ya kipindi chake ambacho hurushwa na Kituo cha Televisheni cha Kimataifa cha DW, ambapo alikua akihoji wananchi wa Dodoma kuhusiana na virusi vya Covid19 ambavyo huchangia maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Akizungumza na wandishi wa habari, DC Katambi amesema mchekeshaji huyo alikua akiufanyia mzaha ugonjwa wa Corona ilihali serikali inafanya kazi kubwa ya kuhamasisha wananchi kujikinga na ugonjwa huo.

" Licha ya viongozi wetu wa Kitaifa wakiongozwa na Rais Magufuli kuwataka wananchi kufuata ushauri wa watalaamu katika kujikinga na ugonjwa huu, kumetokea utani wa kuufanyia mzaha ugonjwa huu akitaka kuthibitisha kuwa wananchi wetu hawana uelewa wowote wa Corona.

Sasa kwa mzaha huo tunataka kujua malengo yake na kwanini amefanya hivyo Dodoma wakati hata Kituo chake cha DW nchini Ujerumani wameuchukulia serious, sasa kwanini hawajafanya utani huo sehemu nyingine zaidi ya Tanzania na haswa Dodoma. Sasa nimtake afike Ofisi ya Mkuu wa Wilaya au Vituo vyetu vya Polisi ndani ya siku tatu," Amesema DC Katambi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...