Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, akizungumza na Uongozi wa Jeshi la Polisi Wilayani Mpwapwa wakati wa ziara ya kikazi wilayani hapo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mpwapwa, Mrakibu wa Polisi, Cosmas Mboya, akitoa Taarifa ya Ulinzi na Usalama kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati wa ziara ya kikazi wilayani hapo.

Na Mwandishi Wetu, Mpwapwa
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameupongeza uongozi wa Jeshi la Polisi wilayani Mpwapwa kwa kudhibiti matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo wizi wa mifugo, mauaji, ubakaji, wizi wa pikipiki, uchomaji moto nyumba, dawa za kulevya, kuzini na maharimu na kupoatikana na silaha kinyume cha sheria.
Waziri Simbachawene ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika wilaya hiyo ambapo alipokea Taarifa ya Polisi ya wilaya hiyo yenye jumla ya wakazi 303,202 wakiwemo wanaume 153,415 na wanawake 158,331 kwa mujibu wa sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 huku mpaka sasa ongezeko la watu ni asilimia 2.1. %
“Nakupongeza OCD Mboya na askari wote walioko chini yako kwa jinsi mnavyoendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika wilaya hii,muendelee na moyo huo huo na sisi kama serikali tutaendelea kuwapa na kuwaongezea nguvu ili muweze kufanya kazi hii ngumu ya kuzuia uhalifu na kuwalinda wananchi ili waweze kufanya shughuli za maendeleo kwa amani na salama” alisema Simbachawene
Awali akisoma takwimu za uhalifu mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,George Simbachawene,Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mpwapwa,Mrakibu wa Polisi, Cosmas Mboya aliweka wazi kupungua kwa makosa mbalimbali ikiwemo wizi wa pikipiki kutoka pikipiki 27 mwaka 2018 hadi pikipiki 7 mwaka 2019, wizi wa njia ya mtandao matukio 28 mpaka 17,kuchoma moto nyumba matukio 7 mpaka 2,dawa za kulevya tukio 1 huku hakuna tukio lilitokea mwaka 2019,ulimaji wa bangi tukio 1 huku hakuna tukio lililoripotiwa mwaka 2019.
Aidha akielezea suala la matukio ya usawa wa kijinsia Mrakibu wa Polisi,Cosmas Mboya alisema kumekuwa na upungufu wa matukio hayo yamepungua kutokana na kuwepo kwa dawati la jinsia wilayani hapo.
“Dawati la Jinsia na watoto limeendelea kufanya kazi kwa kushauri na kusimamia kesi zinazohusu unyanyasaji wa kijinsia na watoto,huku likiwa msaada mkubwa kwa wakazi ikiwemo wanaume wanaonyanyaswa na wake zao kufika kwenye dawati hilo na kuleta malalamiko huku jumla ya kesi hizo kwa mwaka 2018 ni 874 zikishuka mpaka 718 kwa mwaka 2019” alisema Mboya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...